uchambuzi wa magazeti

mutua12

Member
Aug 20, 2008
39
2
Nina omba kueleweshwa hivi ni sawa redio kutumia takribani saa nzima inachambua magazeti mawili tu tena ya jioni ? Hapo biashara ipo kweli kama hata barua za wasomaji inasomwa.Kuna sheria yeyote inayohusiana na hili.
Mwenye uelewa atueleweshe.
 
ndugu ahsante kwa kuleta mada hii inaonyesha kabisa kwamba hiyo radio haina waendelezaji na wafanyakazi imara ambao wanaweza kuletea wasikilizaji vipindi vizuri na mambo mengi zaidi kwa ajili ya radio zao wewe angalia radio zote vipindi vinafanana fungulia asb ea radio , radio one ,clouds vitu vinafanana kasoro lugha na jina la kipindi tu yaani hawana mpya lazima watu wabadilike watafute masoko na wawe creative katika shuguli zao
 
Mkuu Shy nakubaliana na wewe kabisa, ila kwa Radio One nafikiri imekaa sawa maana sidhani kama huwa inakuwa ni uchambuzi bali ni dondoo za Vichwa vya Habari na nafikiri kwa ajili ya kuuza magazeti dondoo ni nzuri zaidi kuwavutia wasomaji kwenda kununua, ila kwa radio nyingine NO COMMENT
 
ndugu ahsante kwa kuleta mada hii inaonyesha kabisa kwamba hiyo radio haina waendelezaji na wafanyakazi imara ambao wanaweza kuletea wasikilizaji vipindi vizuri na mambo mengi zaidi kwa ajili ya radio zao wewe angalia radio zote vipindi vinafanana fungulia asb ea radio , radio one ,clouds vitu vinafanana kasoro lugha na jina la kipindi tu yaani hawana mpya lazima watu wabadilike watafute masoko na wawe creative katika shuguli zao

Nakubaliana nawe, kwa hiyo hii iwe changamoto kwao wasipoteze muda mwingi kusoma habari za watu walioziandika. utakuta mtu ananza kusoma ukurasa kwanza hadi wa mwisho .kuwa creative ni muhimu, watu hawatanunua magazeti wakisubiri kifike kipindi cha magezeti.
 
Back
Top Bottom