Uchambuzi: Dhana ya Serikali kushawishi watu wajiajiri na Uhalisia

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,602
Serikali imekuwa ikishawishi watu wasitegemee kuajiriwa bali wajiajiri. Hii imeonekana katika Awamu zote kuanzia Elimu ya Ujamaa na kujitegemea mpaka leo katika Elimu ya Ujasiliamali. Sitaenda ndani kuonesha hili ni kweli zaidi ya kuweka nukuu ya mteule wa Rais anayeshughulikia mambo ya Vijana na Ajira, mh. Anthony Mavunde.

"Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde Jumamosi hii amekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kujadili changamoto za ajira nchini lililoandaliwa na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM na kuwahusisha wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu mbalimbali nchini.

Akiongea kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, mheshimiwa Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao."

Kauli hizi za kuhimiza vijana kujiajiri ni kauli njema kabisa zenye nia njema kabisa ya kuhakikisha tatizo la ajira linapungua kama sio kutokomea kabisa. Kwa hiyo hili ni tamko la kupongezwa kwa maana ya tamko jema.

Falsafa ya Kujiajiri
Kwa kuwa awamu zote zilitamani Watanzania kwa wingi tujiajiri basi hebu tujadili kwa ufupi falsafa nzima ya kujiajiri.

Kujiajiri sio tu kufanya kazi zako mwenyewe. Ni kweli unapojiajiri unafanya kazi zako mwenyewe, lakini falsafa ya kujiajiri hasa ni kule kutengeneza nafasi ya watu wengine kupata chanzo cha mapato kupitia wewe. Mathalani umeanzisha kampuni ya kutengeza viatu vya ngozi, hapo si tu utakuwa umetengenza chanzo cha mapato kwa wafugaji na madalali wa ngozi, bali pia utakuwa umeajiri watu kukusaidia kuendesha biashara yako. Na inawezekana mabaki-taka (waste product) ya kiwanda chako yakaazisha kiwanda kingine jirani ambacho malighafi yake ni hayo mabaki ya kiwanda chako.

Falsafa ya kujiajiri ina madhara mzidisho (multiplier effect) ambapo mtu mmoja akithubutu kuanzisha jambo faida zake ni kwa watu wengi sana.

Kwa jicho la kiserikali kuna mapato mengi hapo. Kuna PAYE, kuna kodi za mapato kwa kiwanda lakini pia uwezo wa Wananchi waajiriwa na wanufaika wa biashara hiyo kununua unaongezeka. Kwa kuwa wana mtaji, sio ajabu kukuta waajiriwa au wanufaika hawa kuanzisha biashara nyingine.

Hii ndio falsafa ya kujiajiri kama ikifuatwa kwa ukamilifu wake.

Jinsi ya Kuchochea Watu wajiajiri.
Akitangaza vita ya Tanzania dhidi ya nduli Idd Amin, Mwalimu Nyerere alisema mambo muhimu sana ili kufanikiwa katika vita. Baada ya kuelezea alichokifanya Idd Amin mwalimu alisema maneno haya ninanukuu:

"...na sasa tunayo kazi moja tu, ni kumpiga. Uwezo wa kumpiga tunao. Sababu ya kumpiga tunayo. Na nia ya kumpiga tunayo"

Katika vita yeyote, kama huna Uwezo wa kumpiga adui, ni bora uachane naye na ukubaliane na matakwa yake tu, hata kama yana maumivu. Lakini pia hata kama uwezo upo lakini hauna sababu basi usilianzishe kwa kuwa anayefanya mambo bila sababu hufanya hovyohovyo tu, kama kiziwi achezaye muziki au kipofu anayeangali runinga. Na hata kama una uwezo na sababu bila nia utapigwa tu. Sasa hebu tuangalie mambo haya matatu katika uhalisia wake ili kuona kama vita hii ya ajira kwa silaha ya kujiajiri inapiganwa kiuhalisia.

Tuangalie hili kwa wananchi kwanza kisha kwa ufupi tuangalie upande wa serikali.

1. Je Tuna Uwezo wa Kujiajiri?
Jibu la swali hili ni rahisi sana, Ndio! Watanzania wana uwezo wa kujiajiri. Kuna sehemu nyingi sana za kujiajiri hazijaguswa na Watanzania wana uwezo wa kuzigusa na kutengeneza ajira na manufaa kwa wengine wengi. Naomba ninukuu sehemu ya report yangu binafsi ya utafiti katika suala fulani (Ni private report kwa hiyo sitaiambatanisha) sehemu ya ajira.

"Another NBS report on same year puts “about two thirds again (66.3 percent) of currently employed persons were agricultural workers”, and of the remaining portion only 10.9 percent is contributed by formal jobs including the Information Technology sector [6]"

Kwa maana nyingine kati ya Watanzania 100, 67 ni wakulima. na katika 33 waliobakia ni 11 tu ndio wako katika kazi zinazoeleweka/tambulika ikiwemo fani ya Teknohama. Kwa hiyo ukiangalia karibia fani zote kuna uhaba wa huduma na hivyo nafasi za kujiajiri.

Kuonesha umuhimu wa hizi nafasi ambazo hazijatumika hebu tuchukue mfano ambao umo katika ripoti hii.

"In 1994, when Internet was at its infancy, Jeff Bezos lent his parents pension payments to invest in what would become Amazon.com in 1995. The presence of solid payment platform (in this case credit/debit cards), provided a way for Amazon to flourish. Today, just only 21 years later, Amazon employs about 240,000 people in US alone [7]."

Jeff Bezos aliiona fursa ya kutoa huduma za manunuzi kwa internet na leo marekani pekee kaajiri watu laki mbili elfu arobaini. Kuna fursa nyingi sana Tanzania hasa nikiongelea fani yangu ya Teknohama. Watanzania wana uwezo wa kutoa hizi huduma na zikaleta mapinduzi pengine zaidi ya Bezos, Gates, Jobs, Dell na wengineo.

Kuna mapungufu namna elimu yetu inatengeneza watu ila Watanzania wamenonesha waa uwezo wa kuiruka mipaka ya elimu yetu na kufanya zaidi. Katika hili Mh. Mavunde aliona sawa aliponukuliwa akisema "Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao"

2. Je Tuna Sababu ya Kujiajiri?
Jibu ni ndio kabisa. Ajira ni tatizo. Kulingana na NBS, katika vijana wenye uwezo wa kufanya kazi mil 25 ni mil 22 pekee wanafanya kazi na mil 2 hawana ajira kabisa. Hizi ni takwimu za 2014. Kwa sasa tatizo hili ni kubwa zaidi na tunatarajia NBS wakifanya sensa majibu yatakuwa hasi zaidi.

Kwa sababu hii pekee tunahitaji kutengeneza ajira. Kujiajiri ndio mpango pekee utatutoa hapa tulipo kwenye tope la mkwamo. Lakini ni kweli pia kuwa ajira serikalini hazina mwelekeo mzuri. Mpaka sasa hakuna ajira mpya na watu wanaomaliza vyuoni wanaongezeka. Pia nyongeza za mishahara zimesitishwa na nani ajuaye kitakachofuata? Sababu zilizotolewa zimetolewa na aliyeridhika karidhika na asiyeridhika hajaridhika. Ila ukweli utabakia kuwa hata waajiriwa wa serikali wanahitaji kujiajiri kwa namna moja au nyingine. Kuna mengi ya kusema hapa ila itoshe kusema kuwa tuna sababu za kutosha kuamua kujiajiri.

3. Je Nia ya Kujiajiri Tunayo?

Hapa ndipo kuna tatizo. Watu wengi wana uwezo na sababu za kujiajiri ila hawana nia ya dhati. Wengi wakifikiria majeraha ya kupigana vita hii na mazingira yaliyopo, hiyo nia iliyoanza kujengeka inakufa kama sio kuzimia kabisa. Kama nitakavyoonesha chini ni kuwa wengi wanaanza wakiwa na nia ya kuingia huko, ila wakipata shuhuda na kuona mazingira husika nia zinakufa.

Kujibu swali ni kuwa nia tunazo japo wengi sana wa Watanzania ni nia mfu. Zinahitaji kufufuliwa upya!

Sasa hebu tuangalie maswali haya kwa upande wa serikali.

1. Je Serikali ina Uwezo wa kuwafanya watu wajiajiri?
Jibu ni ndio. Kwanza serikali ikiamua kubadili mfumo wa elimu wetu kutoka kuzalisha wataalamu waongeaji mpaka kuzalisha wataalam watendaji, itasaidia sana kutengeneza watu wenye uwezo wa kufanya vitu bila kuingia gharama kubwa ya kujifunza tena baada ya shule. Hapa nina mengi ya kushauri ila kwa leo itoshe kusema Elimu yetu inahitaji mapinduzi kabisa na sio mabadiliko.

Lakini pia serikali ina uwezo wa kuwavuta watu kujiajiri na kufufua upya nia zilizokufa kwa kuweka mazingira rafiki kwa Watanzania. Mfano mmojawapo ni kodi. Kuna tatizo gani kutoa punguzo la kodi kwa mfano kwa miaka miwili toka 30% mpaka 10% kwa kampuni inayoanza ambayo inamilikiwa na Watanzania asilimia 100? Hii itawasaidia kujipanga na kuiweka sawa ili ipate faida na baada ya miaka miwili watalipa kodi ya kawaida.

Pia sheria za maeneo mbalimbali si rafiki kabisa (Nitatoa mfano baadae). Kuna sheria nyingi za Teknohama zimetungwa na watu wasiojua teknohama bila kuwashirikisha wadau wa Teknohama.

Niseme tu katika hili serikali ina uwezo mkubwa sana wa kulifanya gurudumu la Kujiajiri likimbie mara elfu nyingi kuliko kitu kingine duniani. Si wafadhili wala misaada itaongeza chochote kama serikali haitaamua makusudi kabisa kuwekeza katika hili.

2. Je Serikali ina Sababu ya Kusaidia kusukuma watu wajiajiri?
Jibu ni ndio kabisa! Kama nilivyoonesha juu tuna tatizo la ajira na tatizo hilo ni mzigo kwa serikali. Kwa sababu hiyo pekee serikali ina kila sababu ya kulivalia njuga suala hili.

3. Je Serikali ina Nia ya Kuhakikisha watu wanajiajiri?
Hapa napata shida kusema ndio. Mazingira na uhalisia vinakataa kama serikali imewahi kuwa na nia hiyo. Tuone machache kati ya mengi yanayoonesha hili:
  • Serikali imetunga sheria nyingi zinazofanya kujiajiri kuwe kugumu. Nitatoa mfano wa upande wa fani yangu ya Teknohama. Kuanzisha project yoyote ya kusimamia fedha (financial technology) unatakiwa na sheria uwe na mtaji wa chini wa milioni 500. Hii ni bila kujali wigo wa fedha unayotakiwa kuisimamia. Kwa hiyo kama unataka kuanzisha System ambayo itasimamia fedha si zaidi ya Mil 50 bado utatakiwa kuwa na mil 500 kama kiwango cha chini cha mtaji usiotumika (floating balance). Kwa sheria hii pekee, tutegemee kutumia huduma za kifedha za kielektroniki toka nje. Hii ni kwa sababu hakuna Mtanzania ambaye ni wa kizazi cha kielektroniki atakuwa na kiasi hicho cha fedha. Wakati wenzetu wanalegeza sheria ili kusaidia kukua kwa sekta ya Teknohama sisi tunafanya mambo yawe magumu. Hii sheria ilipaswa kuweka kiwango cha chini affordable na kuwa kuwe na leseni za amadaraja tofauti ambapo mtu akifikia kiwango fulani cha floating balance (threshold) anatakiwa ku upgrade leseni yake
  • Sheria ya kulazimisha kila kampuni iwe na .tz domain haifai. Hata Marekani hawalazimishi watu kutumia .us, India hawalazimishi .in inakuwaje sisi wachanga kulazimisha .tz? Ujue matumizi ya domain sio kuweka tu website. Kuna makampuni yapo nchi nyingi au yanapanga kuongezeka nchi nyingi na yana infrastructure zao katika domain zao. Kuwalazimisha wawe na .tz ni kuwaongezea mzigo usio na tija. Kulitakiwa kuwe na kampeni ya kushawishi wazawa kutumia .tz na sio kulazimisha kwa sheria.
  • Serikali kudharau wajasiliamali na ku- encourage monopoly. Unakuta serikali (au moja ya mashirika yake) inahitaji suluhisho la tatizo fulani. Kuna wajasiliamali wengi (Wamoja wamoja au makampuni) ya Kitanzania yanazo hizo solution. Lakini serikali kwa sababu ya mazoea au sababu nyingine tusizozijua wanaamua kuwapa watu ambao ni incompetent kwa sababu wanazojua wao. Matokeo yake ni kushindwa kwa project nyingi na kuishia kuwapaka rangi ya utapeli watanzania wajasiliamali wote. Thread hii nimeongelea pia mfano halisi wa kesi kama hii.
Kwa maelezo haya na utafiti mwingi ambao sijauweka hapa kwa sababu ya nafasi, nina sababu ya kusema serikali ndio inapaswa kuingilia kati ili kuhakikisha suala la kujiajiri linakuwa halisia. Nimshauri Naibu Waziri Mavunde kama ana nia ya dhati ya kuacha alama katika uongozi wake (na Waziri wake) basi waangalie upya serikali imefanya nini kati ya iliyopaswa kufanya ili kujiajiri.

Kwa leo niwashukuru tu mliosoma mpaka mwisho!
Wasalaam!
 
Tunapoandika ripoti huwa tunashauriwa kuandika "executive summary". Pengine ingekuwa vyema na wewe ukafanya hivyo.
 
Everything here is FACT. Hongera sana Stephano naamini wanapita huku na watafanyia kazi.Mada hii irushwe kila mahali na ikiwezekana uitoe kama makala kwenye Gazeti ili maoni haya yasomwe na watanzania wote.
 
Everything here is FACT. Hongera sana Stephano.
Shukrani Boss.

naamini wanapita huku na watafanyia kazi.
Ni matumaini yangu pia kwamba itawafikia na wataifanyia kazi kwa manufaa ya Umma!

Mada hii irushwe kila mahali na ikiwezekana uitoe kama makala kwenye Gazeti ili maoni haya yasomwe na watanzania wote.
Hehehee! Hapo nawaachia wenye media wakiona inafaa wani contact tu. Hii nimeandika haraka haraka wakati wa break ya majukumu mengine :)
 
Everything here is FACT. Hongera sana Stephano naamini wanapita huku na watafanyia kazi.Mada hii irushwe kila mahali na ikiwezekana uitoe kama makala kwenye Gazeti ili maoni haya yasomwe na watanzania wote.
Kwa kuwa binafsi nimeipenda, naiprint then naiweka sehemu yangu ya biashara ili yeyote atakkayehitaji atoe copy akasome na wengine wasiokuwa na access ya internet!
 
Permission is Granted hereby. Only content should not change :)
 
Silicon Valley leaders meet with Trump

Leaders of some of the biggest Silicon Valley companies descended on Trump Tower on Wednesday afternoon, as the tech industry and President-elect Donald Trump tried to reboot their relationship following a contentious election that often saw tech execs standing in opposition to the Republican's campaign.

Trump told the gathered executives that he was "here to help you folks do well" and specifically promised "to make it a lot easier for you to trade across borders."

"We want you to keep going with the incredible innovations," Trump said. "There's nobody like you in the world."

Wary Silicon Valley leaders meet with Trump
 
Serikali imekuwa ikishawishi watu wasitegemee kuajiriwa bali wajiajiri. Hii imeonekana katika Awamu zote kuanzia Elimu ya Ujamaa na kujitegemea mpaka leo katika Elimu ya Ujasiliamali. Sitaenda ndani kuonesha hili ni kweli zaidi ya kuweka nukuu ya mteule wa Rais anayeshughulikia mambo ya Vijana na Ajira, mh. Anthony Mavunde.

"Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Kazi na Ajira, Antony Mavunde Jumamosi hii amekuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la kujadili changamoto za ajira nchini lililoandaliwa na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM na kuwahusisha wanachuo wa vyuo vya elimu ya juu mbalimbali nchini.

Akiongea kwenye kongamano hilo lililofanyika kwenye hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam, mheshimiwa Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao."

Kauli hizi za kuhimiza vijana kujiajiri ni kauli njema kabisa zenye nia njema kabisa ya kuhakikisha tatizo la ajira linapungua kama sio kutokomea kabisa. Kwa hiyo hili ni tamko la kupongezwa kwa maana ya tamko jema.

Falsafa ya Kujiajiri
Kwa kuwa awamu zote zilitamani Watanzania kwa wingi tujiajiri basi hebu tujadili kwa ufupi falsafa nzima ya kujiajiri.

Kujiajiri sio tu kufanya kazi zako mwenyewe. Ni kweli unapojiajiri unafanya kazi zako mwenyewe, lakini falsafa ya kujiajiri hasa ni kule kutengeneza nafasi ya watu wengine kupata chanzo cha mapato kupitia wewe. Mathalani umeanzisha kampuni ya kutengeza viatu vya ngozi, hapo si tu utakuwa umetengenza chanzo cha mapato kwa wafugaji na madalali wa ngozi, bali pia utakuwa umeajiri watu kukusaidia kuendesha biashara yako. Na inawezekana mabaki-taka (waste product) ya kiwanda chako yakaazisha kiwanda kingine jirani ambacho malighafi yake ni hayo mabaki ya kiwanda chako.

Falsafa ya kujiajiri ina madhara mzidisho (multiplier effect) ambapo mtu mmoja akithubutu kuanzisha jambo faida zake ni kwa watu wengi sana.

Kwa jicho la kiserikali kuna mapato mengi hapo. Kuna PAYE, kuna kodi za mapato kwa kiwanda lakini pia uwezo wa Wananchi waajiriwa na wanufaika wa biashara hiyo kununua unaongezeka. Kwa kuwa wana mtaji, sio ajabu kukuta waajiriwa au wanufaika hawa kuanzisha biashara nyingine.

Hii ndio falsafa ya kujiajiri kama ikifuatwa kwa ukamilifu wake.

Jinsi ya Kuchochea Watu wajiajiri.
Akitangaza vita ya Tanzania dhidi ya nduli Idd Amin, Mwalimu Nyerere alisema mambo muhimu sana ili kufanikiwa katika vita. Baada ya kuelezea alichokifanya Idd Amin mwalimu alisema maneno haya ninanukuu:

"...na sasa tunayo kazi moja tu, ni kumpiga. Uwezo wa kumpiga tunao. Sababu ya kumpiga tunayo. Na nia ya kumpiga tunayo"

Katika vita yeyote, kama huna Uwezo wa kumpiga adui, ni bora uachane naye na ukubaliane na matakwa yake tu, hata kama yana maumivu. Lakini pia hata kama uwezo upo lakini hauna sababu basi usilianzishe kwa kuwa anayefanya mambo bila sababu hufanya hovyohovyo tu, kama kiziwi achezaye muziki au kipofu anayeangali runinga. Na hata kama una uwezo na sababu bila nia utapigwa tu. Sasa hebu tuangalie mambo haya matatu katika uhalisia wake ili kuona kama vita hii ya ajira kwa silaha ya kujiajiri inapiganwa kiuhalisia.

Tuangalie hili kwa wananchi kwanza kisha kwa ufupi tuangalie upande wa serikali.

1. Je Tuna Uwezo wa Kujiajiri?
Jibu la swali hili ni rahisi sana, Ndio! Watanzania wana uwezo wa kujiajiri. Kuna sehemu nyingi sana za kujiajiri hazijaguswa na Watanzania wana uwezo wa kuzigusa na kutengeneza ajira na manufaa kwa wengine wengi. Naomba ninukuu sehemu ya report yangu binafsi ya utafiti katika suala fulani (Ni private report kwa hiyo sitaiambatanisha) sehemu ya ajira.

"Another NBS report on same year puts “about two thirds again (66.3 percent) of currently employed persons were agricultural workers”, and of the remaining portion only 10.9 percent is contributed by formal jobs including the Information Technology sector [6]"

Kwa maana nyingine kati ya Watanzania 100, 67 ni wakulima. na katika 33 waliobakia ni 11 tu ndio wako katika kazi zinazoeleweka/tambulika ikiwemo fani ya Teknohama. Kwa hiyo ukiangalia karibia fani zote kuna uhaba wa huduma na hivyo nafasi za kujiajiri.

Kuonesha umuhimu wa hizi nafasi ambazo hazijatumika hebu tuchukue mfano ambao umo katika ripoti hii.

"In 1994, when Internet was at its infancy, Jeff Bezos lent his parents pension payments to invest in what would become Amazon.com in 1995. The presence of solid payment platform (in this case credit/debit cards), provided a way for Amazon to flourish. Today, just only 21 years later, Amazon employs about 240,000 people in US alone [7]."

Jeff Bezos aliiona fursa ya kutoa huduma za manunuzi kwa internet na leo marekani pekee kaajiri watu laki mbili elfu arobaini. Kuna fursa nyingi sana Tanzania hasa nikiongelea fani yangu ya Teknohama. Watanzania wana uwezo wa kutoa hizi huduma na zikaleta mapinduzi pengine zaidi ya Bezos, Gates, Jobs, Dell na wengineo.

Kuna mapungufu namna elimu yetu inatengeneza watu ila Watanzania wamenonesha waa uwezo wa kuiruka mipaka ya elimu yetu na kufanya zaidi. Katika hili Mh. Mavunde aliona sawa aliponukuliwa akisema "Mavunde aliwaasa vijana kuacha kulalamikia ajira wakati uwezo wa kujiajiri wanao"

2. Je Tuna Sababu ya Kujiajiri?
Jibu ni ndio kabisa. Ajira ni tatizo. Kulingana na NBS, katika vijana wenye uwezo wa kufanya kazi mil 25 ni mil 22 pekee wanafanya kazi na mil 2 hawana ajira kabisa. Hizi ni takwimu za 2014. Kwa sasa tatizo hili ni kubwa zaidi na tunatarajia NBS wakifanya sensa majibu yatakuwa hasi zaidi.

Kwa sababu hii pekee tunahitaji kutengeneza ajira. Kujiajiri ndio mpango pekee utatutoa hapa tulipo kwenye tope la mkwamo. Lakini ni kweli pia kuwa ajira serikalini hazina mwelekeo mzuri. Mpaka sasa hakuna ajira mpya na watu wanaomaliza vyuoni wanaongezeka. Pia nyongeza za mishahara zimesitishwa na nani ajuaye kitakachofuata? Sababu zilizotolewa zimetolewa na aliyeridhika karidhika na asiyeridhika hajaridhika. Ila ukweli utabakia kuwa hata waajiriwa wa serikali wanahitaji kujiajiri kwa namna moja au nyingine. Kuna mengi ya kusema hapa ila itoshe kusema kuwa tuna sababu za kutosha kuamua kujiajiri.

3. Je Nia ya Kujiajiri Tunayo?

Hapa ndipo kuna tatizo. Watu wengi wana uwezo na sababu za kujiajiri ila hawana nia ya dhati. Wengi wakifikiria majeraha ya kupigana vita hii na mazingira yaliyopo, hiyo nia iliyoanza kujengeka inakufa kama sio kuzimia kabisa. Kama nitakavyoonesha chini ni kuwa wengi wanaanza wakiwa na nia ya kuingia huko, ila wakipata shuhuda na kuona mazingira husika nia zinakufa.

Kujibu swali ni kuwa nia tunazo japo wengi sana wa Watanzania ni nia mfu. Zinahitaji kufufuliwa upya!

Sasa hebu tuangalie maswali haya kwa upande wa serikali.

1. Je Serikali ina Uwezo wa kuwafanya watu wajiajiri?
Jibu ni ndio. Kwanza serikali ikiamua kubadili mfumo wa elimu wetu kutoka kuzalisha wataalamu waongeaji mpaka kuzalisha wataalam watendaji, itasaidia sana kutengeneza watu wenye uwezo wa kufanya vitu bila kuingia gharama kubwa ya kujifunza tena baada ya shule. Hapa nina mengi ya kushauri ila kwa leo itoshe kusema Elimu yetu inahitaji mapinduzi kabisa na sio mabadiliko.

Lakini pia serikali ina uwezo wa kuwavuta watu kujiajiri na kufufua upya nia zilizokufa kwa kuweka mazingira rafiki kwa Watanzania. Mfano mmojawapo ni kodi. Kuna tatizo gani kutoa punguzo la kodi kwa mfano kwa miaka miwili toka 30% mpaka 10% kwa kampuni inayoanza ambayo inamilikiwa na Watanzania asilimia 100? Hii itawasaidia kujipanga na kuiweka sawa ili ipate faida na baada ya miaka miwili watalipa kodi ya kawaida.

Pia sheria za maeneo mbalimbali si rafiki kabisa (Nitatoa mfano baadae). Kuna sheria nyingi za Teknohama zimetungwa na watu wasiojua teknohama bila kuwashirikisha wadau wa Teknohama.

Niseme tu katika hili serikali ina uwezo mkubwa sana wa kulifanya gurudumu la Kujiajiri likimbie mara elfu nyingi kuliko kitu kingine duniani. Si wafadhili wala misaada itaongeza chochote kama serikali haitaamua makusudi kabisa kuwekeza katika hili.

2. Je Serikali ina Sababu ya Kusaidia kusukuma watu wajiajiri?
Jibu ni ndio kabisa! Kama nilivyoonesha juu tuna tatizo la ajira na tatizo hilo ni mzigo kwa serikali. Kwa sababu hiyo pekee serikali ina kila sababu ya kulivalia njuga suala hili.

3. Je Serikali ina Nia ya Kuhakikisha watu wanajiajiri?
Hapa napata shida kusema ndio. Mazingira na uhalisia vinakataa kama serikali imewahi kuwa na nia hiyo. Tuone machache kati ya mengi yanayoonesha hili:
  • Serikali imetunga sheria nyingi zinazofanya kujiajiri kuwe kugumu. Nitatoa mfano wa upande wa fani yangu ya Teknohama. Kuanzisha project yoyote ya kusimamia fedha (financial technology) unatakiwa na sheria uwe na mtaji wa chini wa milioni 500. Hii ni bila kujali wigo wa fedha unayotakiwa kuisimamia. Kwa hiyo kama unataka kuanzisha System ambayo itasimamia fedha si zaidi ya Mil 50 bado utatakiwa kuwa na mil 500 kama kiwango cha chini cha mtaji usiotumika (floating balance). Kwa sheria hii pekee, tutegemee kutumia huduma za kifedha za kielektroniki toka nje. Hii ni kwa sababu hakuna Mtanzania ambaye ni wa kizazi cha kielektroniki atakuwa na kiasi hicho cha fedha. Wakati wenzetu wanalegeza sheria ili kusaidia kukua kwa sekta ya Teknohama sisi tunafanya mambo yawe magumu. Hii sheria ilipaswa kuweka kiwango cha chini affordable na kuwa kuwe na leseni za amadaraja tofauti ambapo mtu akifikia kiwango fulani cha floating balance (threshold) anatakiwa ku upgrade leseni yake
  • Sheria ya kulazimisha kila kampuni iwe na .tz domain haifai. Hata Marekani hawalazimishi watu kutumia .us, India hawalazimishi .in inakuwaje sisi wachanga kulazimisha .tz? Ujue matumizi ya domain sio kuweka tu website. Kuna makampuni yapo nchi nyingi au yanapanga kuongezeka nchi nyingi na yana infrastructure zao katika domain zao. Kuwalazimisha wawe na .tz ni kuwaongezea mzigo usio na tija. Kulitakiwa kuwe na kampeni ya kushawishi wazawa kutumia .tz na sio kulazimisha kwa sheria.
  • Serikali kudharau wajasiliamali na ku- encourage monopoly. Unakuta serikali (au moja ya mashirika yake) inahitaji suluhisho la tatizo fulani. Kuna wajasiliamali wengi (Wamoja wamoja au makampuni) ya Kitanzania yanazo hizo solution. Lakini serikali kwa sababu ya mazoea au sababu nyingine tusizozijua wanaamua kuwapa watu ambao ni incompetent kwa sababu wanazojua wao. Matokeo yake ni kushindwa kwa project nyingi na kuishia kuwapaka rangi ya utapeli watanzania wajasiliamali wote. Thread hii nimeongelea pia mfano halisi wa kesi kama hii.
Kwa maelezo haya na utafiti mwingi ambao sijauweka hapa kwa sababu ya nafasi, nina sababu ya kusema serikali ndio inapaswa kuingilia kati ili kuhakikisha suala la kujiajiri linakuwa halisia. Nimshauri Naibu Waziri Mavunde kama ana nia ya dhati ya kuacha alama katika uongozi wake (na Waziri wake) basi waangalie upya serikali imefanya nini kati ya iliyopaswa kufanya ili kujiajiri.

Kwa leo niwashukuru tu mliosoma mpaka mwisho!
Wasalaam!
Nchi hii dhana ya kazi ni zaidi ya mama kumwambia mtoto atamnunulia ndege wakati hana uwezo wa kununua baiskeli
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom