Uchakajuaji wa pembejeo za Kilimo

luvara

Senior Member
Apr 9, 2011
170
40
Ni zipi sababu za msingi zinazoifanya serikali iendelee kuwalea wachakachaji wa pembejeo za kilimo? Mchakachuaji wa pembejeo za kilimo kwangu mimi ni mhujumu uchumi namba moja na anastahili kutupwa gerezani mara moja anapobainika na si kunyang'anjwa leseni ambayo anaweza kuomba na kupata nyingine hata kwa kupitia kwa rafiki yake. Kimsingi kumyanyang'a leseni mhujumu uchumi sio adhabu ni upuuzi mtupu. Nisaidieni kiwazo ndugu zangu na hapohapo muishauri serikali yetu namna bora ya kuwashughulikia wahujumu uchumi kupitia pembejeo za kilimo ambao wengi wao walituhujumu msimu ulipita wanafahamika.
 
Suala hili ni gumu sana, sio jepesi kama unavyodhani. Kuna mtu serikalini aliwaambia viongozi wenzake wamwage ugali na yy atamwaga mboga, habari ikaishia pale. Katika hili nani atamfunga au kumshitaki mwenzake?

Pembejeo zinaibiwa kwa mfumo maalumu tokea juu mpaka chini kwa wakala. Wanaokamatwa ni wale walioshindwa kupeleka kidogodogo kwa wahusika. Wale jamaa wanaovaa nguo nyeupe jinsi wanavyopokea kitu kidogo na kukipeleka kwa bosi wake na bosi huyu naye hupeleka kwa bosi wake naye hupeleka kwa bosi wake, sasa huyu wa chini ukimkamata na kumpeleka kwa bosi wake, utaambiwa andika maelezo kisha uje kesho saa nne. kinachofuata jamaa anapewa likizo au transfer kituo/mkoa mwingine.

Msimu uliopita walipeleka mbolea feki wilaya fulani, hakuna aliyeshitakiwa, kwingine walipeleka mbolea baada ya msimu kupita, jamaa bado yuko ofisini na cheo juu, huko kwa Wasukuma walipeleka mbegu bomu za pamba, mbona kuko kimyaaaaaaaaa.

Dawa ni kuwatoa hawa Magamba madarakani kwanza ili tusuke upya mfumo wetu baada ya kuufumua kabisa.
 
Back
Top Bottom