Elections 2010 Uchakachuaji wa kura unaanzia mbali: Taasisi ya takwimu nayo imo

Ruge Opinion

JF-Expert Member
Mar 22, 2006
1,838
701
Jamani maandalizi ya wizi wa kura yanaanzia mbali. Labda ndiyo sababu CCM huwa wanajitapa kuwa mbinu zao ni za kisayansi. Gazeti la THE CITIZEN la Ijumaa, tarehe 29/10/2010 lilichapisha takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu (National Bureau of Statistics - NBS) ambapo NBS ilidai ni makisio ya Watanzania ambao wamefikisha umri wa kupiga kura katika kila Mkoa Tanzania Bara kutokana na takwimu zao za population ya nchi. Jumapili, tarehe 31/10/2010 Gazeti la MWANANCHI lilichapisha takwimu za wapiga kura kimkoa na kwa kila Jimbo la Uchaguzi (mikoa 21 ya Tanzania Bara) kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi. Nimelinganisha hizi takwimu na nilichokiona kinashangaza sana. Ni katika mikoa sita (6) tu ndiyo takwimu za Tume zinatofautiana na zile za NBS. Mikoa hiyo ni Manyara, Shyinyanga, Kagera, Mwanza, Mara na Lindi. Mikoa kumi na tano (15) iliyiobaki makisio ya NBS yanakubalina kabisa kabisa na takwimu za Tume. Kitakwimu hili jambo siyo rahisi. Lazima kuwepo margin of error (kiwango cha kukosea makadilio) ya angalao 2% mpaka 5% hivi. Lakini ukichukulia umakini wetu katika takwimu mimi ningetegemea hicho kiwango kiwe hata zaidi ya 5%. Ninachokisoma hapa ni kwamba takwimu za wapiga kura hazikutokana na Daftari la Wapiga Kura bali ni uchakachuaji kati ya Tume na NBS. Vinginevyo Tume au NBS watupe maelezo nini maana yake. Na kama magazeti ya THE CITIZEN na MWANANCHI nayo yametafsiri takwimu isivyo nayo yatwambie.

Katika mikoa ambayo takwimu zimetofautiana mingi ni ya Kanda ya Ziwa ambapo kitakwimu ndiko kuna wapiga kura wengi (mbali ya Dar es Salaam). Katika mikoa hiyo Tume imeonyesha wapiga kura wachache ukilinganisha na takwimu za NBS. Hii inaweza kuwa ishara ya kujaribu kupunguza idadi ya kura kutoka Kanda ya Ziwa.
 
I dont believe NEC at all. the plan of playing with votes started long time. But those who still support CHADEMA should keep hope alive. We are goimg to be more powerful than b4.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom