Elections 2010 Uchakachuaji na ushindi wa kishindo wa ccm

mdoe

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
433
102
Mbinu inayotumiwa na CCM katika kuchakachua matokeo ya urais, haikabiliwi vilivyo na wagombea ubunge wa CHADEMA. Mathalani, kwa uwezo wangu wa kuona mambo, sehemu nyingi ambapo CHADEMA wameshinda, kwanza matokeo hucheleweshwa, na yakitoka tofauti kati ya Dr. Slaa na JK sio kubwa, na tunaambiwa kulikua na mchuano mkali. Ukitazama kwa umakini, ubungo CCM haikuwa na nguvu kabisa, lakini CCM ina kura 50,000, na chadema iliyokuwa ina nguvu sana msimu huu ina kura 66,000. Sikutegemea tofauti ndogo kiasi hicho. Nawashauri wagombea wa ubunge wazilinde kura za dr. Slaa, na wasiishie kupigania kuingia bungeni tu. Tulipiga kura zetu kutoka mioyoni mwetu, kwa hisia kali za kutaka mabadiliko. Inaniuma sana kuona zikipotea kwa kuchakachuliwa.
 
Back
Top Bottom