Suala la kuchakachua mafuta ni baya sana, tena ni uuwaji. Ni simu inayotuua kwa kufanya kazi taratibu. Kwanza mafuta bei juu. Halafu yamechakachuliwa. Hii maana yake inaua magari. Sina haja kuelezea athari zake kiuchumi kwa mtu na taifa. Serikali imebaki kushangaa tu na kusema wahusika watafutwe na kuchukuliwa hatua. Soma hii habari iliyotoka kwenye gazeti la nipashe.
Sasa mambo ninayoshindwa kuelewa:
1. Hao vigogo walio serikalini, wako juu ya mawaziri? makatibu wakuu wa wizara? Juu ya waziri mkuu? Yote tisa, kumi wako juu ya sheria?
2. Wanajulikana kwa majina, kwa hiyo tuwasujudie tuombe wapungeze ukali wa uchakachuaji. Maana serikali haiwezi, sababu ndio hao hao wanaoendeleza hiyo biashara.
3. Makamba anashauri serikali iweke mkazo, nani kwenye serikali afanye hivyo? wakati ameambiwa wanajulikana wanaofanya huo mchezo.
Sasa tukisema kazi imewashinda, unajibiwa unahatarisha amani na utulivu nchini.
PHP:
Waagizaji mafuta wawaumbua wachakachuaji
Na Joseph Mwendapole
31st March 2011
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta (Ewura)
Waagizaji wa mafuta nchini wameieleza Kamati ya Nishati na Maduni kuwa wachakachuaji wa mafuta ni watu hatari na [COLOR="red"]wamekuwa wakilindwa na vigogo serikalini wanaonufaika na uchakachuaji huo kwa kuwa wanajulikana kwa majina[/COLOR].
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na wadau hao wa mafuta wakati wa kikao cha pamoja baina yao na kamati hiyo.
Walisema watu hao wana fedha nyingi kuliko kawaida na wamekuwa wakiwatishia maisha pindi wanapowakemea kuachana na vitendo hivyo.
[COLOR="red"]Mmoja wa waagizaji wa mafuta, Zacharia Hanspope, aliieleza kamati hiyo kuwa watu hao wanamtandao mkubwa ambao umeshindikana [/COLOR]kwa kuwa inaonekana wamekuwa wakiwahonga baadhi ya viongozi ili waendelee na biashara hiyo haramu.
Alisema wahusika wakuu wa vitendo hivyo ni madereva wa magari ya mafuta ambao wamekuwa wakilagaiwa na watu kuchakachua mafuta hayo na kuwalinda.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Mafuta (Ewura) Haruna Masebu, alikiri kuwa hilo ni tatizo kubwa ingawa wamekuwa wakijitahidi kukabiliana nalo.
Kweli kufanya kazi kwenye sekta ya mafuta kuna changamoto nyingi na ni hatari sana, lakini pamoja na hayo tunaendelea kupambana, tumeshawaadhibu watu wengi waliokutwa na hatia na kila anayemjua mhusika wa vitendo hivi atuambie sisi hatutaacha kumwadhibu kwa kuwa wengi tumeshawadhibu hatumwogopi mtu, alisema Masebu.
[COLOR="red"]Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Januari Makamba alihoji kwanini wahusika hawachukuliwi hatua kali wakati wanajulikana.[/COLOR]Alishauri serikali iweke mkazo kuwatafuta wahusika wa vitendo hivyo kwani licha ya kuharibu magari ya watu vinalitia aibu taifa.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Kigoma Malima, alisema tatizo hilo ni kubwa na Ewura wanapaswa kufanya jitihada zaidi kukabiliana na hali hiyo na ikishindwa ipeleke orodha ya wahalifu hao serikalini.
Mbunge wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage, alisema kwa kuwa wadau wakubwa wa uchakachuaji wanajulikana haoni sababu kwanini wasikamatwe na kuchukuliwa hatua kali.
Alisema kuna taarifa kuwa polisi wamekuwa wakiwalinda wahusika wa vitendo hivyo kwa kuwa wamekuwa wakinufaika nao.
Makamba alisema kupanda kwa bei ya mafuta kunasababishwa na tozo ya kodi kunakofanywa na taasisi nyingi, jambo ambalo linaendelea kumuumiza mlaji.
CHANZO: NIPASHE
Sasa mambo ninayoshindwa kuelewa:
1. Hao vigogo walio serikalini, wako juu ya mawaziri? makatibu wakuu wa wizara? Juu ya waziri mkuu? Yote tisa, kumi wako juu ya sheria?
2. Wanajulikana kwa majina, kwa hiyo tuwasujudie tuombe wapungeze ukali wa uchakachuaji. Maana serikali haiwezi, sababu ndio hao hao wanaoendeleza hiyo biashara.
3. Makamba anashauri serikali iweke mkazo, nani kwenye serikali afanye hivyo? wakati ameambiwa wanajulikana wanaofanya huo mchezo.
Sasa tukisema kazi imewashinda, unajibiwa unahatarisha amani na utulivu nchini.