Uchaguzi wa Rais na wabunge vitenganishwe

Mzee wa Changamoto

New Member
May 25, 2009
2
0
Nimekuwa nikiwaza mara kwa mara juu ya sababu ya nchi yetu kuwa tulivyo hasa kwa siasa tulizonazo. Nahisi tatizo kubwa kwetu ni kwa kuwa tunachagua watu ambao tunawapa dhamana ya kutuongoza kwa miaka mitano na kisha tunasahau. Kwa bahati mbaya, hakuna mwaka ama muhula ambao Rais ametoka katika chama ambacho kina wabunge wengi. Mara nyingi nyakati hizi ndizo ambazo hupima uwezo wa Rais na Bunge na kuonesha makali halisi katika kusimamia na kutekeleza ILANI za uchaguzi.

Tumeona ambavyo wingi wa wabunge walio upande mmoja na Rais usivyo na manufaa kwa nchi yetu na naamini ni wakati ambao tunaweza kuiga siasa za wenzetu ambazo zimeonesha kuleta manufaa kiasi. Kama kuna mwenye shida na kuiga siasa za nje, nikumbushe tu kuwa hata hizi tulizonazo, tusizozimudu na zisizoonesha tija kwa wananchi wetu ni za kuiga na kama kuna linaloweza kuleta maendeleo hakuna ubaya wa kulifuata.

Nchi kama Marekani wana utaratibu ambapo "wabunge" wao wanachaguliwa katikati ya muhula Rais na kinakuwa kipimo tosha kujua kama rais anahitaji wabunge wa aina gani kuipeleka nchi inakotakiwa kwenda. Katika uchaguzi huu wauitao mid-term election, wananchi huangalia msimamo wa wawakilishi wao na kuangalia wanavyosimamia maslahi yao kulingana na sera za serikali na hapo huwachagua ama kuwaweka kando ili kuendeleza ukamilisho wa mahitaji yao.

Naamini hili ni moja kati ya yanayohitajika nyumbani Tanzania. Kwa sasa tunaona miaka minne ya Rais Kikwete ikielekea kumalizika na hatuna hakika na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi wa 2005. Labda ukamilishaji ama utekelezaji huo unazuiwa na baadhi ya wabunge ambao wanapinga baadhi ya mambo, ama unazoroteshwa na baadhi ya wabunge ambao wakishaingia madarakani wanajipa miaka kama mitatu ya "kula shushu" kabla ya "kufufuka" mwaka wa nne na "kuzibuka" ule wa tano tayari kututimulia vumbi (wakidai wanatengeneza barabara), kuweka oda za khanga, vitenge na vi-Tshirt tayari kuwapumbaza wananchi kuwachagua tena. Kwa kuwa na uchaguzi wa nusu muhula, wananchi wataweza kuangalia kama Rais anahitaji wabunge wa kutosha kumsaidia kuendeleza maendeleo kwa wananchi wake, ama kama anahitaji wabunge wenye kuona uozo wake na kwenda kumwamsha katika usingizi wa kutotekeleza aliyoahidi.

Gharama za kutenganisha chaguzi haziwezi kuwa kubwa kuliko gharama za kutotekeleza lolote lililoahidiwa na wabunge kwa wananchi na pia kutoshughulikia mambo mengi ambayo yanaweza kuwawezesha wananchi kujishughulisha na mambo ambayo yanaweza kuwasaidia wananchi kujiendeshea maisha yao bila kutegemea msaada wa serikali.

Wananchi wanateseka na kupoteza maisha na hata matumaini kwa kuwa watu wenye dhamana ya kushirikiana nao kunyoosha njia zao za mafanikio, wanatumia nafasi hiyo kujinufaisha na kwa hakika yahitajika namna ya kuwaamsha hawa WATAWALA. Na ndio maana NIONAVYO MIMI... UCHAGUZI WA RAIS NA WABUNGE UTENGANISHWE

Hivi ndivyo nionavyo tatizo, na pengine namna nionavyo tatizo ndio tatizo.
 
Mawazo mazuri sana ila ukilinganisha na UCHUMI WA TANZANIA ambapo hata hizo pesa zenyewe za uchaguzi wanaomba msaada itakuwa taabu kidogo.

KIFUPI MAWAZO MAZURI SANA ILA ITAKUWA TAABU KUYAIMPLEMENT KUTOKANA NA HALI HALISI YA UCHUMI WA TANZANIA
 
Tuliwachagua kwa Mafiga matatu sasa wanatekeleza Ilani yao ni Sisi Watanzania ndio wameshindwa kuwaza na kujua
 
Lakini kutokana na mawazo yako naona ni bora kufanya kama wanavyofanya india. Yaani kuwa na kura a kutokua na imani na kiongozi (vote of no confidence).

Hii itakua kama mbunge ameshindwa kutekeleza ahadi zake basi wananchi atamuengua na nafasi ile kuchukuliwa na yule aliegombea nae na kushika nafasi ya pili.

Lakini kwa tanzania njia bora ni kubadilisha katiba. Kani kwa mujibu wa katiba ya tanzania, mbunge anawakilisha chama na sio wananchi waliomchagua kule bungeni.
 
Back
Top Bottom