Uchaguzi wa NEC Hanang': Sumaye abwagwa na mama Nagu

Let us hope for the best that your prophesy will be true, otherwise it will be Mwandosya's catastrophic end to his political career!! Please do not underestimate Kikwete's machinations against his political enemies inspite of his appointing them to his cabinet!!

Habari kutoka Rungwe;Prof Mwandosya KASHINDA na Kasesera kakubali matokeo!
 
Ama kweli Lowassa ana nguvu sana ndani ya CCM. Anaweza kustopishwa tu nje ya CCM kwa kura za wananchi kwenye uchaguzi wa urais (maana inaonekana wazi ni de facto nominee tayari).
 
Duh, siasa za CCM mnaambiwa zaina wenyewe, sasa leo unaweza kuwa mmoja wao, lakini kesho sio mmoja wao
 
Kweli Lowassa ananguvu kisawasawa ndani ya CCM,

Na kweli Lowassa hakukutana na Kikwete barabarani.
 
...Idadi ya kura please?...

Nipo mbali na sehemu ya tukio lkn Prof Mwandosya kashinda tena kwa kura za kutosha tu!Habari hizi ni za ukweli kwa 100% na sikuweza kupewa idadi ya kura kwa sababu watu 3 nilio ongea waliokuwa wajumbe kwenye mkutano huo sauti zao zilikuwa za furaha mno kiasi kwamba nilichoambulia kutoka kwao ni"TUMESHINDA KWA KISHINDO"!

Worry not Butola and surely put this into your account;Prof Mwandosya(as usual)has emerged as a clear-cut winner on one-sided Rungwe's election!He won by landslide margin!
 
Safari ya Sumaye kutaka kujaribu kuingia Ikulu huenda ndio imefikia mwisho, hata kwa maajabu ya kiCCM haiwezekani tena.
 
Habari kutoka Rungwe;Prof Mwandosya KASHINDA na Kasesera kakubali matokeo!
Kambi ya Lowassa haina muda wa kupoteza kupambana na mzee wa watu aliyejichokea kiumri na kiafya!

Kwa sasa inajipanga kumweka mrithi wake mara tu Professor Mwandosya atakapoachia ngazi yaani 2015 na wakati huo ukifika akigoma tu kung'atuka yatamkuta kama Mallecela, Msekwa,Sitta.
 
huyu mzee anajisumbua tu..kama alishindwa kuwa rais alipokuwa waziri mkuu,ndiye aje kuwa rais 2015?
 
Baada ya Sumaye kushindwa vibaya, huu unaweza ukawa ni wakati wake mzuri kujikita zaidi kwenye ufugaji wake wa ng'ombe wa kisasa kuliko kuendelea na siasa.
 
Huyo ndio JK anajua kuangamiza wapinzani wake kiana. Nagu hakutoa rushwa, bali usalama wa Taifa umefanya kazi yake.
 
Ndoto ya Sumaye kuingia magogoni 2015 naona imeingia nyongo mapema. Sasa kazi imebaki kwa Lowasa kupambana na atakayeteuliwa na kambi ya bagamoyo!
 
aibu sana, ex-PM kwenda kushinana huko vijijini simply kuendeleakupata ulaji

jamaa amejidhalilisha sana
 
Ndoto ya Sumaye kuingia magogoni 2015 naona imeingia nyongo mapema. Sasa kazi imebaki kwa Lowasa kupambana na atakayeteuliwa na kambi ya bagamoyo!

Angalia vizuri karata zako. Kwa wote walioshindwa ama kukatwa katika uchaguzi ndani ya CCM ama waliojiuzulu ama kuamua kupumzika, ni jambo jema sana kwao kuliko wengi wa waliopitishwa ama kushinda ndani ya CCM. Kwa hali ya sasa, yeyote anayebebwa na CCM ama JK ana matatizo na kwa hili mafisadi waliopitishwa ndio kaburi lao na CCM yao. Sumaye hana cha kujutia hasa kama hajatoa rushwa kama Nagu.
 
Inasemekana Jk 2005 aliingia madarakani kwa kugawa bahasha za takrima toka uarabuni, tutegemee nini kwa Mawaziri wake? Mliopokea takrima ya shs 500000@ Hanang' ndio mnasababisha upungufu dawa hospitalini na kuikumbatia rushwa Hanang'. Roho za Wanahanang' zinazopotea kwa kukosa dawa mtadaiwa siku moja. Inasemekana takrima aliyotoa Nagu zimetoka kwa Lowasa na usiku wa kuamkia uchaguzi alikuwa Katesh, kaondoka alfajiri, fisadi mtoto hilo nalo lina ukweli?
 
TAKUKURU yawafuata Sumaye, Nagu Hanang

na Mwandishi wetu, Katesh
Tanzania Daima



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imeingia kwa siri wilayani Hanang' kukabiliana na vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa kutafuta wajumbe wa halmashauri kuu yake ya Taifa (NEC), wilayani humo, imefahamika.

Hatua hiyo ya TAKUKURU imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika kampeni, vinavyodaiwa kufanywa na mmoja wa wanaowania nafasi ya mjumbe wa NEC kutoka wilayani Hanang'
CCM imewapitisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dkt. Mary Nagu na Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye kuwania nafasi ya mjumbe wa NEC katika wilaya hiyo.

Kumekua na madai mazito kuhusiana na ugawaji fedha unaofanywa na mgombea huyo na kwamba anatumia mbinu ya kugawa fedha hizo kwa njia ya mtandao.

Akizungumzia madai hayo ya rushwa, Kaimu Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Hanang' Samson Sanga alikataa kuzungumzia kuhusu taasisi yake kufanya kazi zake kwa siri kwa maelezo kwamba kwa sasa ofisi yake haiwezi kuzungumzia suala hilo.

Wiki hii, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah alinukuliwa akisema taasisi yake inafuatilia kwa karibu uchaguzi huo ndani ya CCM ili kubaini watu wanaotumia rushwa.

Dk. Hoseah alitoa kauli hiyo akijibu hoja mbalimbali za washiriki wa kongamano la kujadili utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango wa kupambana na rushwa nchini na mapendekezo yanayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya tatu (2012 – 2016).

"Tatizo ni kwamba wagombea wengi wa nafasi ya uongozi wamekuwa wakijiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi na kwa bahati mbaya hata wananchi ambao ni wapiga kura ni kama wanajiandaa kupokea rushwa kila uchaguzi unapokaribia, hili ni tatizo kubwa," alisema Dk Hosseah na kuongeza:

"Tunaendelea kufuatilia, lakini ni kazi kubwa kwelikweli kwa mfano, sasa tunafuatilia uchaguzi wa ndani wa CCM na tunafanya hivi ili kuhakikisha kwamba hatupati viongozi wanaotokana na rushwa, maana tukiwa na viongozi wa aina hii hatuwezi kushinda vita hivi."

Katika kikao kilichofanyika Jumapili ya Septemba 2, mwaka huu na kuongozwa na katibu wa CCM Wilaya ya Hanang' Allan Kingazi, wajumbe wa kikao hicho walipitisha jina la Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Leonsi Marmo huku Dkt Nagu akitoswa kufuatia kudaiwa kuwa na majukumu mengi ya kikazi ikiwemo ubunge na uwaziri.

Wakizungumzia maamuzi ya vikao vya juu vilivyopitisha jina la Dk. Nagu kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo, baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya ya Hanang' walioomba kutotajwa majina yao gazetini walisema kamati hiyo haikuwatendea haki.

"Kamati kuu haikutenda haki kabisa, kwa kuwa imepuuza maamuzi yetu, haiwezekani sisi tufanye maamuzi tena kwa kufuata kanuni za CCM ilizotunga yenyewe halafu maamuzi yetu yabadilishwe na kuonekana sio sahihi, huku ndio kunakopeleka pabaya hiki chama,"alisema mmoja wa wajumbe waliodaiwa kupigia kura jina la Dkt.Nagu kutopitishwa katika kikao kilichofanyika Septemba 2 mwaka huu.



 
Back
Top Bottom