Uchaguzi wa Madiwa,Wabunge na Rais Utenganishwe

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,765
4,033
Imekuwa ni kawaida ya chaguzi zetu zinapofanyika kuambatana na dosari nyingi sana ambazo zinakatisha tamaa kwa wapenda demokrasia nchini.Kwa mfano uchaguzi mkuu mwaka huu uliyofanyika tarehe 31 octoba 2010,baadhi ya majimbo uchaguzi uliahilishwa kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza ,zikiwemo za kukosekana kwa karatasi za kupigia kura,baadhi ya majina ya wapiga kura kukosewa,nembo za vyama kuingiliana kwenye majina ya wagombea ubunge na kukosekana kwa majina ya baadhi ya wagombea kwenye karatasi za kupigia kura. kutokana na dosari hizi ziliilazimu tume ya uchaguzi kupanga tarehe tofauti ya kufanyika uchaguzi katika majimbo mbalimbali ya uchanguzi.Tarehe ambapo 14/11/2010 ulifanyika uchaguzi katika majimbo ya Mpanda mjini,mpanda vijijini,Nkenge,mwanakwerekwe,mtoni,magogoni na wete.na leo tarehe 28/11/2010 unafanyika uchaguzi wa madiwani katika halmashauri za Newala kata ya (Mtonya),Mbulu(Endegikot),manyoni(Kitaraka),Sama(Kisiwani),Kibaha(Janga),Rufiji(Kibiti),(chemchem),(ngorongo),(kipugira) na (Mjawa).
Katika halmashauri ya Uyui ni kata za kigwa na Ibelamilundi.Sikonge ni kata ya Kisanga na Halmashauri Njombe ni kata ya Mji mwema.Katika halmashauri ya ulanga ni kata ya msogezi.Katika halmashauri ya karangwe ni kata za kimuli na kamuli,Kasulu ni kata ya Kitagira,Chato ni kata ya Buseresere na Katika halmashauri ya Mwanza ni kata za mbuyuni na milongo.Hli hii pia ilijitokeza katika uchaguzi wa 1995 ambapo uchaguzi wa jiji la Dar es salaam uliailishwa na kufanyika baadaye,baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.
Inavyoonekan kwa kifupi ni kuwa tume ya uchaguzi haina uwezo wa kusimamia uchaguguzi wa madiwani,wabunge na rais kwa wakati mmoja kwa ufanisi wa kutosha na hivyo kusababisha manunguniko mbalimbali kutoka kwa wapiga kura.Historia inaonyesha hamasa ya wapiga kura hupungua sana pale uchaguzi unapofanyi muda tofauti na uchaguzi mkuu unapofanyika,hii ni sumu kubwa katika mkakati wa kuboresha hali ya demokrasia katika nchi yetu.Kama hii ndiyo hali halisi tuliyoishuhudia kwa tume yetu ya uchaguzi na ikiwa nia yetu ni kuboresha demokrasia na kuondokana na tatizo hili ni vyema uchaguzi wa madiwa na ubunge ungekuwa unafanyika kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais ili kuboresha utendaji wa tume ya uchaguzi.

Nawasilisha,
Tukutuku
 
Back
Top Bottom