Uchaguzi wa Kiteto: Taarifa mbalimbali

Status
Not open for further replies.
thanks Kichuguu, na wengine tuendelee.. what do we know about Kiteto the place, the people, the natural resources, etc.. ni mahali pa kuhamia... ?

Mwanakijiji

Hata usisusumbuke kwenda huko Kiteto, Lowasa amemtafuta padri wa kanisa katoliki kugombea- anaitwa Nanyaro. Hivyo Olaiboni Kimesera pamoja na kuwa mmasai wa kwanza kupata shahada na mwenyekiti wa wamasai Dar es salaam ataambulia patupu. CCM Kiteto wanalalamika kwa kuletewa mgombea na mtu wa Monduli na wanasema akheri wampe Kimesera ambaye ni mlezi wa familia ya marehemu Sokoine. Lakini CCM inakabiria kuwa weka mambo sawa huko. Hivyo usisumbuke. Mzee Kimesera amekuwa akipata zaidi ya asilimia 40 kila uchaguzi lakini sasa anaweza hata asipate asilimia 10, alikuwa akishindana na nguvu ya waziri Mkuu Sumaye, sasa ni Lowassa- sokoine mpya.

PM
 
Inawezekana Tyson akapewa u PM hasa ukizingatia kuwa mtu aliyechaguliwa kwa sura huku akiwa na zero accomplishment na utekelezaji wake ukiwa mbovu lazima amweke mtu mwenye sura mbaya akihofia mwenye sura nzuri kumpindua akiamini kabisa kuwa alichaguliwa kwa kuuza kura. .....maoni
 
Inawezekana Tyson akapewa u PM hasa ukizingatia kuwa mtu aliyechaguliwa kwa sura huku akiwa na zero accomplishment na utekelezaji wake ukiwa mbovu lazima amweke mtu mwenye sura mbaya akihofia mwenye sura nzuri kumpindua akiamini kabisa kuwa alichaguliwa kwa kuuza kura. .....maoni

..duh! hii perspective........kiboko!
 
Baada ya CCM kuvuruga sana, mimi kipimo cha nguvu ya upinzani ni haya majimbo matatu. Ningetegemea wachukue yote, sana sana mawili. Wakiishia kuchukua jimbo moja maana itakuwa moja tu kwamba mikakati yao haifanyi kazi.[/QUOTE]

Nina wasiwasi na kipimo hiki hasa kwa Jimbo la Kiteto kwa sababu ya Jiografia na miundombinu kwenda huko. Usafiri wa kwenda huko ni mgumu na watu wengi hawako informed juu ya mambo yanayoendelea katika nchi hii. Asilimia kubwa ya wananchi wa Kiteto hawajui BoT nini? Hivyo watapiga KURA kwa msisimko wa Sisiem imeleta Amani. Nadhani tuwasaidie WANANCHI WAPIGA KURA kwa ku-photocopy data nyingi za magazeti na jamboforums kisha ziwafikie wanachi wa majimbo haya kama VIPEPERUSHI.Hii itawafanya wafanye maamuzi wakijua kinachoendelea.
 
Mugo, ndio maana nataka mtu anisaidie kufanya utafiti mdogo tu wa Kiteto kuna shule ngapi (za msingi na sekondari), kuna chuo chochote, potential mineral resources, etc. Haya mengine yataendelea mbele ya safari
 
kichuguu good narration kuhusu stephen wassira tyson...je unajua ugomvi wake na warioba usioisha unatokana na nini??

baada ya kujitoa upinzani alikula waya sana ..mara nyingi alipenda kushinda kwenye ofisi ya samaki pale msasani..jk kamuinua kweli..

juzi kaoa mke wa nne...mama mmoja aliyekuwa mke wa mfanyabiashara maarufu wa masuala ya bima ambaye alifariki...wanayetoka sehemu moja..
 
Yaani hata wapinzani hawana habari zozote zinazohusu Kiteto wakatuwekea hapa tuzichambue? Jamani, tutafanyaje kazi bila ya kuwa na pa kuanzia?
 
Yeah, halafu jana Chadema walikuwa wanakutana sasa wameshaamua mgombea wao ni nani? Binafsi sijali chadema watamsimamisha nani kwani hata wakisimamisha chungwa mimi nitataka watu walipigie kura chungwa.
 
Ninashauri vyama vya upinzani viungane kutoa mgombea mmoja tu kwenye jimbo hilo. Halafu waendeshe kampeini ya nguvu sana kutumia skendo ambazo bado zinakumbukwa na watu kama zile Buzwagi, na BOT.
 
Kuhusu Kiteto,ni kuwa vyama vilivyoko kwenye ushirikiano wa vyama vimekubaliana kumsimamisha mgombea wa CHADEMA ambaye ni ndugu Victor Kimesera.

Kuonyesha ushirikiano huo ni kuwa viongozi wote wa kitaifa wa vyama hivyo wanategemewa kuhudhuria uzinduzi wa kampeni hizo na kufungua rasmi kampeni hizo.

Kuhusu JIMBO LA KITETO.

1.Ni kuwa jimbo hili lim,egawanyika kwenye makundi matatu makubwa ,ambayo ni wafugaji hawa wakiwa ni wazawa wa jimboni humo.

kundi la pili linahusisha wakulima wadogowadogo -hawa walkiwa ni wahamiaji kutoka mkoani Tanga ambao wameishi humo kwa muda mrefu tangu wakati wa ukoloni na hawa walipelekwa na wakoloni kwa ajili ya kwenda kulima mashamba yao ta mpunga baada ya wakoloni kushindwa kuwapata wamasai kufanya kazi hiyo.

kundi la tatu ni la wakulima wakubwa ambao wanatokea mikoa ya Dodoma na haswa kondoa na kule mkoani Iringa ambao ni wakulima wakubwa na wanamiliki mashamba makubwa .

2.Jimbo la kiteto linao wapiga kura waliojiandikisha 74,0000+, na kwa historia ni kuwa mgombea wa CHADEMA mzee kimesera ambaye sasa anakuwa mgombea wa ushirikiano alipata 42% ya kura za ubunge za 2005.

3.Makao makuu ya jimbo yanaitwa KIBAYA ambako inawezekana watu wakashangaa kuwa makao makuu ya wilaya yana idadi ya wapiga kura 3000 tuu ,ni kitu cha ajabu kidogo kwani wengine wote wako vijijini.

4.kuhusu idadi ya watu na mgawanyo wa watu hawa ni kuwa wakulima ni wengi kuliko wfugaji kwani wafugaji wapo 40% na wakulima wapo 60% ya watu wote .

5.Nitawaletea taarifa za idadi za shule n.k hapo baadae mara nikizipata .

na leo CHADEMA wametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uteuzi huo wa Kimesera n.k.
 
Its time now we get wabunge wenye meno (Slaa, Zitto etc) katika kiota chetu cha Dodoma........ Kura zetu zote kwa Victor Kimesera!! Na hii sio kwa vile ni upinzani, bali ni kwa vile tunataka mabidiliko ya kweli na sio kigeugeugeu na viini macho vya sasa kwenye "ruzuku/takrima/fadhila"!!!
 
Mgawanyo wa maeneo ni kama ifuatavyo;

1.Makami,Ndendo,Olboloti na Laiseri ni maeneo ambayo wamasai wanaishi wengi.

2.Kibaya ni mjini na wanaishi makabila tofauti ilia pako domineted na warangi,wangukwe.

3.Kiperesa,chekanao,matui na njoro ni eneo la warangi ndio wengi.

4.kijungu ,lengatei,sunya,na ndilali wapo kabila ama watu wanaitwa wanguu hawa wametokea tanga na ndio waliletwa na wakoloni.

5.dongo na songombele ni mchanganyiko wa watu tofauti tofauti.

ukubwa wa jimbo zima kijiografia ni kilimita 940.

mengine baadae.
 
Mpaka Kieleweke-ubarikiwe sana kwa habari na mchanganuo huo. Kila la heri kwenye haya mapambano.
 
Taarifa za kiserikali ni kama ifuatavyo;
ENEO.36,685 kilomita za mraba.

idadi ya watu;152,296 kwa mujibu wa sensa ya 2002.

kwenye idadi hiyo ya watu ni kuwa ,
WANAUME 76,291.
WANAWAKE 76,005.

Mgawanyo wa kiumri ni 65,597 kati ya 15-44.
86,699 kati ya 45-80+.

ENEO LA KIUTAWALA .
KATA; 15.,VIJIJI;51,NA VITONGOJI ,234.

ELIMU NI KUWA 26% NDIO WANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA NA HII NI KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA HALI YA ELIMU.

Mengineyo nitawaletea taarifa kama nitazipata na haswa kuhusiana na idadi ya shule pamoja na zahanati zilizopo ,pia hali ya kiuchumi na haswa kujua aina za rasilimali zilizopo zaidi ya mifugo na kilimo.
 
Mpaka kieleweke asante sana hayo ndiyo ninayoyazungumzia.. very helpful.. ! Usisahau kutuletea matatizo na changamoto ambazo watu wa Kiteto wanazipata kila kukicha..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom