Uchaguzi wa CCM wazazi Tanga vimbwanga

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimesikiza TBC asubuhi hii nijisikia kukata tamaa. Ati uchaguzi wa Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Tanga umeahirisha baada ya kura zilizopigwa kuzidi idadi ya wapiga kura!

Wagombea wa nafasi hiyo walikuwa nia Henry Shekifu RC Manyara (Mtetezi wa kiti), Dk. Mohammed Mhita (mgombea), M. Risherd (Mgombea). Habari zinasema kuwa katika awamu ya kwanza hakuna mgombea alifikia idadi ya kura zinazohitajika. Kwa kuwa Dk Mhita alishika mkia, wagombea wa juu- Shekifu na Risherd walipigiwa kuwa awamu ya pili na ndipo kindumbwendumbwe kilitokea pale ilipobainika kuwa jumla ya kura zilizopigwa zilikuwa ni zaidi ya wajumbe waliopiga kura!

Nilijisikia kutishwa na Ufisadi unaofanyika kwa kiwango hicho katika Uchaguzi huo wa CCM Wazazi na kusababisha nijiulize kama wagombea hawa (Shekifu na Risherd) ni waadilifu kuaminiwa kupewa nafasi za Uongozi katika nchi hii.
 
Hili jambo si geni kwa CCM kuiba kura angalia sasa wao kwa wao ndani humo wanajiibia je kwenye chaguzi hizi zingine iwa inakuwaje?Si balaa tupu!
CCM navyo jua wakija waangalizi wa kimataifa wasimamie uchaguzi mbona ni vioja vitupu tutashuhudia.
 
Hivi hiki cheo cha mwenyekiti wa wazazi kina manufaa gani binafsi, maana mpaka akina mkono nao eti wnakitaka, madaktari wa falsafa, maprof.....

Hivi hizi jumuiya kazi zake ni zilezile kama tulivyokuwa tukisoma kwenye siasa enzi zetu????????
 
Hivi hiki cheo cha mwenyekiti wa wazazi kina manufaa gani binafsi, maana mpaka akina mkono nao eti wnakitaka, madaktari wa falsafa, maprof.....

Hivi hizi jumuiya kazi zake ni zilezile kama tulivyokuwa tukisoma kwenye siasa enzi zetu????????


Nyambala, kumbuka ule msemo "ukitaka biashara zako zifanikiwe...".
 
Nisiasa zakiafrica na sio CCM tuu.. Freeman did the same thing kwenye Ubunge wa Hai. I was there and i saw what he did.. its politics aka mchezo mchafu
 
Back
Top Bottom