Uchaguzi wa CCM na mbio za urais 2015

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Ni ukweli usiopingika kuwa, mchakamchaka wa uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM unatawaliwa zaidi na makundi hasimu mawili ambayo yanatajwa kutaka watu wao wachaguliwe na kujiweka katika mazingira mazuri ya ushindi ndani ya chama. Angalia: ziara za Nape mikoani hivi karibuni, zilikuwa na lengo la kudhoofisha na kuharibu nguvu za kundi la LOWASA na kujenga kundi la MEMBE. Wakati Lowasa akitajwa kuwa amejiimarisha vilivyo ndani ya chama, Membe anaelezwa kuwa ana fuko kubwa la fedha maarufu kwa jina la "mabilioni ya Gaddafi". TUJADILI: NANI YUPO UPANDE WA LOWASA Na NANI YUPO UPANDE WA MEMBE na makundi mengine
 
Ni mada nzuri. Kwa kuanzia tu kwa Dsm, John Guninita ni mtu wa Lowasa. Arusha, Ole nangole nae ni wa lowasa. Bashe (Nzega), Kabourou na Premji hawa wote ni wa EL. Kusila(Dom) ni lowasa. Membe anao kigwangala, makongoro nyerere. Naendelea kutafuta wengine
 
Mimi na kiongozi yeyote asiye mnafiki atakuwa upande wa Lowassa

Ila mbona naona kama kunajitihada za kuuaminisha umma kuwa CCM ni hao wawili tuu ndio wanaweza kupewa wengine hamna au?Magufuli je......?Sumaye..?mie naona hawa ndio wanaweza lete ushindani kwa lowassa na hata Dr. slaa
 
Back
Top Bottom