commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,952
hatimae kamati kuu ya Ccm imempitisha rasmi Bw sioi sumari kuwa mgombea rasmi wa ubunge jimbo la arumeru mashariki,kupitia chasma hicho.
Tukio hili limetokea huku kukiwa na sintofahamu ya nini kinaendelea kuhusu sakata la kukamatwa kwa baadhi ya wana CCM kadhaa jimboni humo wakihusishwa na tuhuma za rushwa ,katika kinyang'anyiro hicho na mpaka sasa inasemekana wako chini ya ulinzi wa jeshi la polisi mjini arusha.tuhuma hizi zimehusishwa rasmi na mgombea sioi sumari
My take!
Kitendo cha Nape kujitokeza katika vyombo vya habari jioni hii kuutangazia umma kwa mbwembwe kuwa kampeni hizo zitaongozwa na Mhazini wa ccm Bw mwigulu nchemba,na akijitapa kuwa chama chake kitashinda.ni sawa na KULAMBA MATAPISHI YAKE,
Sioi sumari,mbali ya kuwa na mahusiano ya kifamilia na mtuhumiwa mkuu wa tuhuma za ufisadi,lakini pia hata zoezi lenyewe limechafuliwa na tuhuma lukuki za Rushwa.
Nape amekuwa akijitambulisha kama mpinga ufisadi namba moja ndani ya ccm na nilitarajia kuwa asingejitokeza hadharani kuyasema hayo aliyoyasema kama kweli ni mpiganaji wa kweli wa ufisadi ndani ya chama hicho
Naomba kuwakilisha ....