Uchaguzi wa bububu una siri nzito

bagwell

Senior Member
Sep 19, 2012
113
25
1. MTIHANI KWA GNU.
Ulimwengu unataka kuangalia mabadiliko yoyote katika mienendo ya siasa za Zanzibar baada ya kuundwa mfumo mpya wa serikali. uchaguzi huu unaweza ukaleta taswira gani hasa vile uchaguzi ulivyoendeshwa ,uingiliaji wa vyombo vya ulinzi kupita kiasi na kwa upande wa pili tetesi za mamluki na upendeleo mambo haya yanaifanya GNU kuwa katika mtihani na kunaweza kurudisha ile imani ya kuaminiana baina ya wadau wa GNU. Huu ni ikiwa hayo ni kweli huu ni mtihani kwa Dr shein na wasaidizi wao na watu wote waliojitahidi kuwaunganisha wazanzibari. Kwa HAPA RAIS WANGU ANA KAZI KUBWA NA SIJUWI IKIWA KULIKUWA NA CONCESUS YOYOTE YA SERIKALI JUU YA HADHARI YA KUENDESHA UCHAGUZI HUU NA MWELEKEO WA UTENGAMANO WA GNU HUKO MBELE. Napata wasiwasi isije ikawa wahafidhina walitia mguu wao hasa kwa ule mwenendo wa kampeni ulivuyokuwa. ngoja tuone wakuu watachukuwa hatua gani.
2. MTIHANI KWA CUF na CCM.
Kwa CUF waangalie wasije wakapoteza imani wananchi wao. wananchi wanataka kuona mabadiliko ya mwenendo wa mambo likiwemo hili la siasa . Si wengi wanaojuwa kwamba mabadilko huja taratibu na mzoweya vya kunyonga vya kuchicha haviwezi. Jee mtihani huu CUF watakabiliana nao vipi huko mbele ? na ilihali wao ni wadau katika GNU tena wadau muhimu hapa kuna siri itafichuka ama chama kipoteze kwa kuleya GNU au CCM wakubali mabadiliko jambo ambalo ni gumu mno kwa histiria ya vyama tawala vya kiafrika kukubali hilo labda ile ajenda ya Zanzibar kwanza kuwe na wazito (CCM ) iwe wameibeba. Tutaona. Kwa upande wa CCM nao wana mtihani wao wakubali mabadiliko na wakifanya hivyo wakubali kupoteza pia . Mabadilko yanapokuja lazima yataathiri baadhi ya mambo ukiwemo uluwa. Dunia hii hakuna kitakachodumu. Sasa kwenye CCM mpaka sasa kuna kambi kuu mbili Wahafidhina na wanamambo leo ( nchi kwanza) sijuwi ni kwa kiasi gani hili kundi la pili lina nguvu .mtihani uliopo hapa jee hawa wanamambo leo wataendelea na msimamo huo hata ikibidi kukiharimu chama chao au watakubali chama na kuiharimu Zanzibar huko mbele ya safari ? maana madai yao yanaungwa mkono na kila mzanzibarimwenye angalau chembe ya uzalendo naamini wakiwa na msimamo hawatajuta hata kidogo kuna siku wataingia katika historia mpya ya kuirejeshea zanzibar mamlaka yake . Tuombe dua lakini………
3. KUHUSU MAMLAKA YA ZANZIBAR NA KATIBA MPYA KITENDAWILI ?
Uchaguzi huu unaweza ukaleta suali jee ikiwa nguvu hile ya vikosi ndio kusema ni kazi ya wale wahafidhina wasiotaka mabadiliko na ambao kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakishika kasi katika harakati zao za kujikwamua ? linaweza likazuka suala hili. Hizi tetesi kwamba kuna kigogo mmoja wa CCM na mwandamizi katika GNU anahusika zote si ishara nzuri ikiwa kutakuwa na ukweli.Lakini hata mwenendo wa kampeni za CCM kumejidhihirisha hilo wasemaji wakuu walikuwa ni wahafidhina na kila waliposimama ni kuzungumza Muungano uliopo na waliacha kueleza sera za mwakilishi na chama chao jee wale wanamambo leo ndio wamedhibitiwa na tayari hili suala la mwamko wa mamlaka ya Zanzibar nalo ndio limefika mwisho ? jitihada za hawa jamaa kutaka kuzima huo moto ni kubwa uchaguzi wa bububu unaweza ukawa ni kigezo ? wazalendo leteni maono yenu. Lakini wanamabo leo mbona hatuwasikii je ni mkakati au kudhibitiwa ? Basi makamo mwenyekiti wa chama zanzibar ndio asifunguwe kampeni basi hata kufunga kuna nini hapa ? siri ndani ya siri.
MWISHO.
- wazalendo watu wazidishe harakati zao kuangalia maslahi ya Zanzibar iwe ni kwa njia ya vyama au taasisi nyengine za kijamii. tusipoutumia mwanya huu wa katiba mpya Zanzibar imekwisha kuna kila dalili wasioitakia mema wametibuliwa mpango wao na utaajuwa tu kwa kauli zao ile agenda ya kuelekea kuwa nchi moja ina siri nyingi na tayari hao hao( CCM wazalendo ) wamegunduwa na ndio wakabadilisha mwelekeo ingawa inawezekana walijifigha toka mwanzo lakini hawakupenda.
- Tuwe tayari kumuunga mkono kila mwenye uchungu wa kuitetea zanzibar na tuwe tayari kumlaani kila anayeiidhoofisha Zanzibar bila kujali itikadi za kisiasa, kidini na nyenginezo
- Tushikamane na kamwe tusirudi nyuma kuitetea zanzibar na kuipatia mamlaka yake kamili.
_ GNU iwe macho na wahafidhina hili la BUBUBU limwirikwe vizuri ninavyoona litaleta sokomoko ingawa ni kigezo kizuri kujuwa mwelekeowetu
Mungu ibariki Jamhuri ya Zanzibar na watu wake. Amiin
 
Back
Top Bottom