Uchaguzi ukiisha tuambieni ukweli

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
WAKIMALIZA WATUELEZE

Wakati kampeni za uchaguzi mdogo wa Tarime ulipoanza kushika kasi chama tawala kilitoa makadirio yake na fedha ambazo watatumia katika uchaguzi huo ilikadiriwa kama chini ya mil 200 , chadema nayo iliyoa makadirio yake ilikuwa chini ya mil 100 mmoja wa wasemaji wa chadem alisema kwamba san asana ni mil 80 watakazo tumia kwa sababu lile ni jimbo lao kwahiyo hawana shida sana katika mpambano huo .

Siku zimehesabika sasa tunazidi kuona maajabu katika uchaguzi huu mdogo baada ya chadema kuleta helicopter 1 ya kampeni , ccm imeleta helicopter 2 kila chama kikijinadi kwa wananchi wa jimbo hilo la uchaguzi .

Katika kampeni zote hizi kila chama kinajaribu kuonyesha wananchi kwamba wao ni wazuri wanatumia pesa vizuri na watahakikisha maendeleo ya tarime ndio nguzo yao kuu wakishinda uchaguzi huo , kwa bahati mbaya sana katika kampeni zote hizi wagombea hawako tayari kuwekwa kitimoto na wananchi wao kujibu maswali au kujibu chochote ni kampeni na kuishia mitini
Yote haya ni tisa tutawasamehe kwa kukimbia , kwa kupigana na kufanya karaha zingine zote wanazozifanya jimboni tarime , lakini mwisho wa uchaguzi huo tunaomba vyama vyote vilivyoshiriki vitupe matumizi yao katika kampeni hizo kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa uchaguzi huo .

Wakifanya hivyo watakuwa wamefanya mambo ya busara sana , wananchi wataweza sasa kujipanga na kujua gharama za majimbo yao kifedha , manake hizi helicopter , polisi wanavyopelekwa kule na mambo mengine yanatisha sana watu wanaacha kazi za kujenga taifa wanakimbilia tarime wote hawa wanalipiwa na vyama Fulani .

Mwisho kabisa watuambie ukweli vyanzo vyao vya mapato ukiacha ruzuku wanazopewa na serikali , hizi pesa za kuchezea kurusha helicopter juu zinatoka wapi au ndio wanakopa wakishinda uchaguzi waje kulipa kwa pesa za wananchi ? mwisho wa siku wananchi wanaendelea kuwa masikini ?

Sijasikia mgombea akiahidi kujenga chuo au kitu chochote muhimu wengi wanakimbilia katika huduma za maji tu , sijasikia mgombea akiongelea ajira kwa wana tarime na mambo mengine muhimu muhimu hivi wanatarime wasipoelimika hata hizo huduma za maji zitatumikaje wagombea ??
USIKU MWEMA
 
CCM wamekodi helicopter kwa kuaiga Chadema katika kufanikisha kampeni zao ingekua bora si kuishia katika hilo bali kukopi na kuhakikisha kua wanatetea yale yote mazuri Chadema wamekua wakiyapigia kelele Ufisadi ,rushwa n.k.Chadema wanatumia helicopter hii nikutokana na hali ya barabara zetu ambazo CCM kwa wakati wao wate ambapo wamekua madarakani hawakuliona kwao kutumia helicopter ni matusi kwa wana Tarime hii inakua kama si uchaguzi bali Air show kwa upeo wa CCM kama walivyozoea kwadanganya wananchi.Wananchi wanapaswa kuwauliza kwanini watumie helicopter.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mkuu kumbuka kwamba Chadema tuliweka hadharani matumizi yetu ya fedha za kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, waambie CCM waweke za kwao walizotumia katika uchaguzi mkuu uliopita, na kwa CHADEMA tayari tumeshaamua kwamba tunaweka hadharani mahesabu yetu ya chma yaliyokaguliwa ni moja kati ya maazimio ya kikao cha juzi tu cha Kamati kuu kwa hilo sisi CHADEMA hatuna la kuficha kwa kuwa fedha tunazotumia katika shughuli za chama ni fedha za walipa kodi maskini wa Tanzania.
 
unafikiri wataacha kutoa taharifa wakitaka, watasema RA alichangia bilioni 40 utasema nini zaidi ya kukubaliana nao.
 
Back
Top Bottom