Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2007

Hapo Hapo!! Huko Kisulu nako kuna habari isemayo!!

CUF Kasulu yabwagwa, yakimbiwa na wanachama​

Kutoka Gazeti 'letu' la Uhuru
Na Prosper Kwigize, Kasulu


CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeshindwa katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika wiki iliyopita katika kata ya Nyamidaho, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Katika uchaguzi huo ulioshirikisha wagombea kutoka vyama vya CCM na CUF, mgombea wa Chama Cha Mapinduzi, Mustapha Mgereranya aliibuka mshindi dhidi ya Abel Nuhu wa CUF.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi Msaidizi, Nicholaus Kimondo alisema wapiga kura 7,274 walijiandikisha na waliopiga kura walikuwa 2,746.
Kimondo alisema kati ya kura 2,746 zilizopigwa, halali zilikuwa 2,696, wakati nyingine zikiripotiwa kuharibika.

Nuhu alipata kura 1,047, wakati Magereranya alishinda kwa kupata kura 1,649.
Wakati huo huo, vinara wa CUF katika tarafa ya Makere, wilayani Kasulu wamekihama chama hicho na kujiunga na CCM kwa kile walichodai kuwa ndani ya chama chao hakuna demokrasia.

Waliojiunga na CCM ni Tumaini Sambilo na Henrico Kimorimori, ambaye alikuwa mgombea wa kiti cha udiwani wa kata ya Nyamidaho kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu mwaka 2005.

Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Said Hamad alisema kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wanachama hao kunaonyesha kukomaa kwao kisiasa na kukubalika kwa Ilani na sera za Chama.
 
CCM yatoa changamoto kwa wananchi kuacha malumbano

Kutoka Gazeti 'letu' la Uhuru,
Na Tiganya Vincent, MAELEZO-Tanga


CHAMA Cha Mapinduzi mkoani Tanga kimetoa changamoto kwa wakazi wa mkoa huo kufanya kazi kwa bidii badala ya kuendesha malumbano mitaani, ambayo hayawasaidia katika kujiletea maendeleo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Idd Ally Ame alisema hayo jana wakati wa kilelele cha sherehe za Umoja wa Vijana wa CCM, zilizofanyika wilayani hapa kwa mara ya kwanza.

Ame alisema maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana kwa watu kuchapa kazi kwa bidii, kutumia fursa zinazotolewa na Serikali katika kujiletea maendeleo na si vinginevyo, kama watu wachache wanavyodiriki kuwadanganya wengine kwamba serikali itawapatia fedha.

“Hatukusema kila mtu tutampelekea fedha mfukoni… hatukusema tutamjengea kila mtu nyumba kama sehemu ya kuhakikisha kuwa anakuwa na maisha bora, unachomaanisha ni kumtengenezea fursa zitakazomwekea mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo,” alisema.

Alisema wananchi hao wanatakiwa kubuni miradi, kuandaa michanganuo na kuianzisha ili kujiletea maisha bora kwa kujiongezea kipato.

Ame alisema ardhi iliyopo mkoani Tanga inaweza kusaidia kutengeza ajira nyingi kama wananchi wataitumia vizuri katika kuzalishia mazao ya kilimo na chakula.

Alisema kwa baadhi ya viongozi kudiriki kupita mitaani na kupiga kelele huku wakiikashifu Serikali kwa mazuri inayofanya si suluhisho la kuwaletea maendeleo, bali ni katika kujituma na kutumia fursa zilizotolewa na serikali.

Aliwakumbusha wananchi wa Tanga kuwahakuna haja ya kulumbana na vyama vya upinzani kwani jukumu lililoko mbele yao ni kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005.
 
Kumbe Kasulu watu walijiandikisha , je kwa nini Tunduru wamekataa kuandisha wapiga kura ila wanataka kutumia wale wale wa zamani ?
 
Habari za masiku Wana-JF,

Samahani sikuwepo ila uchaguzi huku CCM umepamba moto sana na kazi ni mingi sana! Nimerudi sasa kwa habari motomoto huko CCM kwenye Uchaguzi Mkuu! Soma Habari Hapo Chini Kwa Zaidi!!!

Mchuano CCM leo

Kutoka gazeti la 'Wapinzani Wetu' Tanzania,
Na Nasra Abdallah


ccm_header1.jpg

MBIO za kuwania uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ngazi ya taifa, mikoa na wilaya zinaanza rasmi leo.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa chama hicho,Yussuf Makamba, kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, ilisema fomu za kuwania nafasi hizo zinaanza kutolewa leo hadi Juni 5, ambayo pia itakuwa ndiyo siku ya mwisho kuzirejesha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi za uongozi zitakazogombewa kwa ngazi ya wilaya ni pamoja na mwenyekiti, katibu wa siasa na uenezi na katibu wa uchumi na fedha.

Nafasi nyingine katika ngazi hiyo ya wilaya ni wajumbe watano wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, wajumbe 10 wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya na wajumbe wawili wa mkutano mkuu wa CCM Mkoa.

“Katika ngazi ya mkoa, nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, mjumbe au wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, yaani mmoja kwa mikoa ya Tanzania Bara na wanne kwa mikoa ya Zanzibar.

“Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa, wajumbe wawili kutoka kila wilaya ya Tanzania Bara na watano kutoka kila wilaya ya Tanzania Zanzibar,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Nafasi nyingine katika ngazi ya mkoa ni katibu wa siasa na uenezi wa CCM mkoa na katibu wa uchumi na fedha wa CCM wa mkoa.

Katika ngazi ya taifa, nafasi zinazogombewa ni ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, nafasi 85.

Orodha hiyo ya taifa ya viti 85, imegawanyika katika makundi matano, ambayo ni kundi la Bara nafasi 20, kundi la Zanzibar nafasi 20 na kundi la wanawake nafasi 20.

Makundi mengine ambayo kihistoria yamekuwa na mchuano mkali ni kundi la vijana nafasi 15 na kundi la wazazi nafasi 10.

Katika taarifa yake hiyo, Makamba alitoa wito kwa wote wenye sifa za kugombea nafasi hizo kujitokeza kugombea.
 
KWELI mtandas wamekamata chama ..hatimaye mwenyekiti wa jumuia ya wazazi ambaye wakati wa muchakatoo wa urais alitangaza hadharani kumuunga mkono FREDERICK SUMYE...amevuliwa madaraka yote chamani..pia mwingine aliyevuliwa ni aliyewahi kuwa mbunge wa bukoba na sasa katibu wa chama bukoba mh kataraia....wote wanadaiwa kuwa wabadhirifu..na zaidi kataraia anadaiwa kusaidia upinzani..

vipi wadau naona ccm imeanza kuadhibu wabadhirifu kwa kuanza na hao ..tusubiri wengine nao..au isijekuwa ndio mtandao wameanza kufanya usafi...
 
Kondoo wa kafara hawa...wabadhirifu wenyewe wanaoathiri uchumi wapo mtaani na wala hawaguswi.
 
hivi kataryai ni katibu wa ccm bukoba amba katibu wa ccm mkoa wa singida ? maana ninavyokumbuka alikuwa katibu wa ccm mkoa wa mwanza na kudaiwa kutafuna fedha kabla ya kuhamishiwa singida kwa wadhifa huo huo
 
jee kama hawana nidhamu kweli na wanaenda kinyume na katiba ya chama waachwe?

CCM kwa wengine kila ifanyalo kosa, ikiwachukulia hatua wabadhirifu kosa, ikinyamaza kosa lipi hasa kwenu liko sawa ?

hawa wahuni wache wende to the hell la kama chadema mnawataka kawanunuweni ili mlipe kama mnavyodai ati wenu wananunuliwa
 
mtu mwitu umeona mambo ya KOMANDOO hayo,kwani yeye sui mjumbe wa KAMATI KUU? au ndio amenuna???

Komandoo apata mapokezi makubwa
Na Sama Said, Zanzibar


RAIS Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, amepata mapokezi makubwa na wakazi wa Kijiji cha Kidombo, Mkoa wa Kaskazini Unguja ambako alizaliwa.


Dk Amour alifika jana kwa mara ya kwanza kijijini hapo tangu aliporejea kutoka kwenye matibabuni nchini China.


Kiongozi huyo maarufu kama 'Komandoo' alilakiwa kijijini hapo kwa shamrashamra za wakazi wa eneo hilo, huku wakeretwa wa CCM waliovalia sare rasmi za chama hicho na wananchi mbali mbali wakiwa wamejipanga barabarani wakimshangilia.


Mara baada ya kuwasili alishuka kutoka kwenye gari lake na kusalimiana na wananchi

na wazee walikokuwa na shauku ya kumwona.


Kufuatia hafla hiyo, baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkwajuni wameilalamikai Sauti ya

Tanzania Zanzibar (STZ) wakidai haikuwatendea haki kwa kukataa kutanagza tangazo lao la kuwataarifu wananchi juu ya ujio wa Dk Amour katika Jimbo lao.


Afisa mmoja wa (STZ) alikiri kuliona tangazo hilo na kudai kuwa baada ya hapo hakuelewa kilichoendelea hadi kufikia kutotangazwa, licha ya wananchi hao kulilipia kama utaratibu unavyotaka.


Akihutubia umati wa watu walifika kumlaki, Dk Salmin alisema: ?Leo sio siku ya mazungumzo marefu ?, ni siku ya kusalimiana na nashukuru Mungu, mie sijambo na nyie vipi je, hamjambo, wazimaaaa?


Aliwashukuru wananchi wa Jamhuri ya China kwa ushirikiono wao kwake ambapo alisema Taifa hilo ni rafiki wa kweli kwa Tanzania.


Hata hivyo aliwafahamisha kwamba Wachina wamejikita zaidi katika kufanya kazi kwa bidii ili

kujipatie maendeleo, hivyo aliwataka Watanzania kuiga mfano wao.


Awali, katika risala yao iliyosomwa na Kada wa CCM, Maulid Nafasi Juma, wazee wa kijiji hicho walimtaka Komadoo ajisikie yuko nyumbani na kwamba wamefarijika sana na kurejea kwake akiwa mzima.


Dk Amour alilakiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Riziki Omar, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Kakazini Unguja, Fum Mati na baadhi ya viongozi wa Jimbo la Mkwajuni na Maskani ya Kisonge.

http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=743
 
Ndio maana tuliwaambia kuwa Dr. Salim out, sasa wameingia kina Makamba, next election iutakuwa ni Fulll Hand ya Mtandao, na huo ndio kwanza umeanza, abiria fungeni mikanda!
 
Ndio maana tuliwaambia kuwa Dr. Salim out, sasa wameingia kina Makamba, next election iutakuwa ni Fulll Hand ya Mtandao, na huo ndio kwanza umeanza, abiria fungeni mikanda!

Mzee ES umetumia lugha ngumu kidogo, naomba ufafanuzi najua unaweza kuwa na mengi kwenye hii hoja ya wana CCM kutimuana.
 
Bila CCM kufarakana na kutimuana do you expect upinzani utaimarika lini?

CHADEMA, CUF kula vichwa hivyo,,, ndio nyomi yenyewe hiyo
 
Kutimuana kwa CCM haina maana kwamba ndio Upinzani utaimarika kwa hao waliotimuliwa kujiunga na Upinzani, kwani kama Kigezo cha kutimuliwa ni Ubadhirifu na utovu wa Nidhamu, sidhani kuwa watakua waadilifu wakiingia upinzani, bado wanadamu ya KiCCM hayo watakuja kutuvuruga tu hao, hawafai.
 
Mimi napendekeza Kamati Kuu ya CCM ipitie mikataba yote ya uwekezaji na kuwachukulia hatua waliohusika. CCM's CC mara nyingi imekuwa na ujasiri wa kufanya kile ambacho Wabunge na viongozi wengine mmoja mmoja hawawezi kufanya.
 
Kutimuliwa kwa hao jamaa kama ni kwa ubadhirifu mi nawapa tano kamati kuu. Wakianza kamati Kuu kusafisha maovu tuna hakika kuwa polepole tutakuwa na viongozi wenye ahueni katika utendaji na uwajibikaji wao.Ni wazi kuwa viongozi tunowapigia kelele hivi sasa ni wana ccm walopitishwa na kamati yao kwa nyadhifa mbalimbali miaka ilopita, na sasa kama upembuzi wa maadili ya viongozi unaanzia huko kwenye kamati kuu basi hii ni dalili njema mana haohao ndo watakuja kuwa viongozi wa juu baadae.
La kama ni kutimuliwa kwasababu za kimrengo (Sumaye vs Lowassa & Co) hilo lafaa kupigwa vita
 
Nakubaliana kweli kwamba hawa ni wabadhirifu,,, lakini kumbukeni asilimia kubwa ya wapinzani ni watu wenye makovu fulani fulani hata kama sio ya ubadhirifu wa fedha/mali moja kwa moja... Kwani kwa mfano Mrema ana uadilifu gani?

CC inatakiwa kupongezwa kumuondoa mwenyekiti wa jumuiya kubwa kama ile ya wazazi na kwa maana nyingine alikuwa mjumbe mwenzao wa CC sio jambo rahisi lazima washukuriwe kwa hili.

Lingine si kweli kwamba CC inamtandao,,, CC ya sasa bado inaundwa na jamaa wote wa Zamani, kwa maana CC ya sasa inao akina JSM, FTS etc.

Mwanakijiji pia amesema jambo la maana; kwamba kumbe wabadhirifu wanaweza adhibiwa kwa kunyang'anywa vyeo vya ccm na ccm yenyewe: (duh! isije kuwa CC ndio Senate yetu.....); anyway they have tried, loud aplause
 
Mimi napendekeza Kamati Kuu ya CCM ipitie mikataba yote ya uwekezaji na kuwachukulia hatua waliohusika. CCM's CC mara nyingi imekuwa na ujasiri wa kufanya kile ambacho Wabunge na viongozi wengine mmoja mmoja hawawezi kufanya.

UJASIRI !Wameanza lini huo ujasiri? hapa unanichanganya kidogo. CC ya CCM ndio walewale,tena hao ni hatari zaidi kwani vikao vyao vimetawaliwa na USIRI mkubwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom