Uchaguzi Mkuu wa CCM 2012: Tumsapoti Lowassa

Hawa jamaa vipi? hizi taarifa zinafaa either zibandikwe kwenye ofisi za CCM au wapeane memo wao kwa wao kwani wenyesifa za kumchagua au kutomchagua ni wana CCM ambao idadi haizidi 5000, hata baadhi yetu humu hatuwezi kumchagua huyo EL, so hii taarifa haikupaswa kuwepo humu
 
Kwa mujibu wa gazeti la Dira, toleo la leo kama kweli tunaitakia mema nchi yetu basi tumuunge mkono Lowassa, achukue uenyekiti wa chama taifa na JK abaki na urais wake.

Kwani utaitishwa uchaguzi wa watanzania wote unaposema tumchague mamvi?
 
Kwa mujibu wa gazeti la Dira, toleo la leo kama kweli tunaitakia mema nchi yetu basi tumuunge mkono Lowassa, achukue uenyekiti wa chama taifa na JK abaki na urais wake.

President Elect, Kwa sasa Lowassa ndio anafaa kuiongoza CCM. Kwani anayo sifa kuu ya Ufisadi. CCM ilikuwa dodoki likibeba kila uchafu na sasa uchafu ulishageuka kuwa gamba. Kwa hiyo Lowassa kuwaongoza magamba wenzake ni sahihi.

Namuunga mkono kukiongoza Chama 2012.
 
Hivi hii inchi imekosa kweli watu makini wa kutuongoza.siyo hawa wahujumu wa uchumi hata akisimama mbele za watu hana cha kusena.unajua zinakuwa nyingi.
 
Akishindwa CCM atakuja Chadema ok..na hakuna wa kumzuia huko..

CDM wanawanachama na wafuasi wa kutosha ambao ni waadirifu, hawahitaji tena watu design ya Shibuda. Kama anahamu ya kuwa mwenyekiti wa chama aanzishe cha kwake, nafikiri huko anaweza kuamua hata kuwa mwenyekiti wa maisha kama Agustino Mrema.
 
For sure we need a person mwenda wazimu kama Lowassa lakini siyo Lowassa jamaa yake amemchafua sana

Natamani afyatuke aseme yaliyo moyoni mwake, lakini hivi kimya kimya itamgharimu sana, kwanini wasisahau tofauti zao na akina Sitaa wakamgeuka huyu mgonganishi anayewagonganisha? Anatumia trick ya devide and rule. Chanzo chote kinajulikana
 
Natoa mwito kwa wote wenye kumjua Mungu, tuiombee nchi yetu Tz. kwa bidii.

Paul anatuonya tusiombe kama mtu anayepiga ngumi upepo; tuiombee ifanyeje? Kuhusu mafisadi hatutakiwi kuomba tunatakiwa kuwazuia kwa maneno yetu na kukiri kwetu kila siku na kuchukua hatua ya imani kugombea nafasi stahiki ili kuitoa imani katika maneno kuiweka katika matendo; mimi 2015 nitampigia campaign Dr. W.P Slaa kuwa rais ili chama changu kipate madaraka na mimi nitumie utaalamu wangu kuwasaidia watanzania maana najua kila mguu wangu utakapo kanyaga Mungu amenipa hiyo sehemu; wewe je?....Kuhusu future tunatakiwa kuuliza manabii ikoje na kuhusu amani ndiyo tunatakiwa kumwomba Mungu maana yeye ndiye pekee aweza kuitoa si kama jinsi wanadamu watoavyo bali inayokidhi haja amabpo kupitia hiyo masikini atajikuta salama; tajiri na hata mnyonge...
 
Mtoa maada
CCM hawajapitisha ajenda ya kutenganisha hizo kofia
EL hajaomba / kutangaza kugombea nafasi hiyo hata ya urais hajasema kama atagombea tena
hapa tuna choka na habari za kusadikika .
 
Kwa mujibu wa gazeti la Dira, toleo la leo kama kweli tunaitakia mema nchi yetu basi tumuunge mkono Lowassa, achukue uenyekiti wa chama taifa na JK abaki na urais wake.

el ni mchapakazi na mtendaji mzuri na zaidi ni mfuatiliaji wa mambo kwa ukaribu,tatizo lake ni kama jk wote ni watu wa visasi sana,halafu sidhani kama anahtaji nafsi hyo kwani hawezi kumsaliti rafki yake kipenzi,nanukuu(ngd wananchi URAFKI WANGU NA MH RAIS KIKWETE HATUKUKUTANA BARABARANI na pia thread moja hmu jf inayosema!!!!!!please MEMBE BE CAREFULL!WANAJF HUO NDO UKWELI WA MAMBO
 
Nani atamzuia chadema Lowassa anachukua tu (anaweka dau kubwa kupita la sobodo)

Besides, keep on guessing

umefika wakati tuache mzaha wa kaitanzania na tuwe serious na issue na sio kujibu pumba kama hizi zako...Lowassa ana laana ya baba wa taifa na watanzania kwa ujumla...kwa yote haya anayotutendea iko siku monduli PATACHIMBIKA!!....
 
Back
Top Bottom