Uchaguzi Mkuu wa CCM 2012: Tumsapoti Lowassa

Mzee Lo itabidi atazame political career nyingine lakini kwa Uraisi wa nchii jina lake limepata madoa mengi. Huyu mhe. Peter Serukamba mbona mara nyingi kwenye social life huwa anaonekana na Mtoto wa mzee Lowasa, Serukamba yuko kambi ya Richmonduli?
 
Kama ana kiu kali ya urais si lazima apitie CCM kama wao hawamtaki vipo vyama vingi tu......CDM, CUF,UDP..........au aanzishe chake(nasikia ana pesa nyingi).......Kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila raia.........muacheni atumie haki yake labda atabadilika na kuwa kama Sokoine



Unasema labda atabadilika na kuwa kama sokoine!? Mkuu, ufisadi ni kama wendawazimu. Mwandawazimu haponi, anapata nafuu tu! Huyu jamaa anaonekana ananafuu sababu yupo nje ya serikali. Ugonjwa upo palepale. Akipewa nafasi ndio utajua! Na bahati mbaya sana ni kwamba, kumpa nafasi huyu ni kama kuijaribu sumu kwa kuionja! Mungu aepushie mbali!
 
Historia ndio jibu..Marando, Slaa, Safari, Lwakatare..list goes on..

Lazima kuwepo na dampo la kutupa ili ionekanae kuna domo-ghasia



Dampo ni lipi hasa. Maana huko kwenu kuna Wassira, Kaburu, Lamwai, Ngawaiya, Tambwe Hiza and the list goes on! Achilia mbali akina Nape, Sita na wengine wa ccj. Bado mafisadi wote wa nchi!!?
Fungua Macho Mwita25. Hivyo vihela vya Nape vinavyokupofusha kwa kukuweka jf kutwa nzima havina future! Cdm ikishachukua nchi utatupwa kama akina Tambwe hiza na kuishia kuongea upuuzi kama Lusinde wa Mtera!?
 
Sasa si usubiri atakwenda chadema akipigwa chini ccm..

Wakati huo cahdema watabadilisha wimbo kabisa ..utaumia lakini ndio siasa hiyo..


Huijui cdm wewe! Magamba yamekupa uzito wa akili sasa unafikiri kwa kutumia masaburi!
 
Ni kweli kabisa kwa mtazamo wako lakini utashi unasema mbona huyo lowasa ana ksshifa nyingi anasafishika? au ninyi ndo mlimtuma? huwagawia hato mapesa? maana sioni sababu ya maana sana kwa yeye kupigiwa upatu kwa kila kitu mradi tu aukwae urais 2015. Kuna nini hapo? Mbona hamsemi Salim Ahmed salim, au Mkapa au Sumaye au Warioba, au hata mzee Malecela/ Kwanini kila kitu Lowasa tu. Mh! There must something wrong somewhere.

Lowasa kugombea ni haki yake kama wana-CCM watampatia kura ni sawa tu, kwani huko CCM hakuna aliye afadhali zaidi ya Lowasa CCM ni genge la majambazi hakuna msafi kule yeyote atakayechukua form CCM ni mchafu, fisadi na mwizi.Kumsema Lowasa hamtamtendea haki kule samaki wote wameoza na kuvunda.Hakuna msafi wooooooote mafisadi.KANYAGA TWENDE LOWASA WEWE NDIYO CHAGUO LA MAFISADI, WEWE NI FISADI ULIYEKUBUHU NDIYE UNAFAA KUWAONGOZA MAFISADI WENZIO CCM.
 
Dampo ni lipi hasa. Maana huko kwenu kuna Wassira, Kaburu, Lamwai, Ngawaiya, Tambwe Hiza and the list goes on! Achilia mbali akina Nape, Sita na wengine wa ccj. Bado mafisadi wote wa nchi!!?
Fungua Macho Mwita25. Hivyo vihela vya Nape vinavyokupofusha kwa kukuweka jf kutwa nzima havina future! Cdm ikishachukua nchi utatupwa kama akina Tambwe hiza na kuishia kuongea upuuzi kama Lusinde wa Mtera!?

Kama ambavyo wewe umepewa na chadema au siyo..unajua nyie watu chadema huwaga hamnazo mnafikiri kila mtu amehongwa mnajisahu kuwa nanyi mmehongwa..kama wewe hoja hongwa huwezi kufikiri mwenzako amehongwa period..

Lowassa is out of ccm, sasa dampo lake la kwanza ni Chadema

Sijui nani atamzuia hamtaki hela nyie nyingi kuliko za sabodo?
 
Kukataa Lowassa asigombee ndani ya ccm kutaimaliza.Ndo ukweli huo.No one can stop him ndani ya ccm.Binafsi sina chama ila naamini EL anaifaa ccm kabisa.
 
Jamaniiii huyu Lowassa ni nani hata awe mjadala kila siku. Nini uhakika hatakuwa Raisi wa nchi yoyote hata kufa kwake. Kwani sisi wengine tusiokuwa na kashfa kama zake hatuwezi kumwongoza. Naye akakaa chini akawa raia mwema.
 
Lowasaa ni mwizi lakini anawekeza nchini kwake, jamaa pesa yote kawekeza nchini kwa hiyo hapo hakuna wizi kachukua pesa ilikuwa idle serikalini yeye akaiwekeza.Mbona hamjamsema fisadi JK aliyewekeza SA na arabuni.Lowasa chukua formu wana CCM watakupa kula za ndiyo na wala usihame CCM tulia huko huko, nafasi ya mwenyekiti ni yako mwakani.Go go go go go go Ngoyai Lowasa Eduardo
 
Ukweli ni kwamba EL will keep on fighting for presidency to last breadth. Ni mpaka watakapotoa jina lake ndio atastop, believe me. Na ndani ya CCM hakuna wa kumzuia, JK mwenyewe anamkubali, Mukama na uongozi wa UV-magamba wako kambi yake. Kama wanaweza kumzuia EL ni kitu kimoja tu, wamtimue ndani chama wala wasisubiri ajivue gamba, walivue tu kwa nguvu hata kama linauma, walivue. La sivyo, 2012 tutashuudia EL akichukua uenyekiti na 2015 akigombea, na kama katiba itakua ni hii hii, utashangaa awamu ya 5 ni EL. Hapo ndipo kila mtu ataonja joto ya jiwe.

Lakini pia kama EL atakuwa mwenyekiti wa magamba then tutegemee magamba kugawanyika into pieces, aidha chama kipya au kukimbilia upinzani. sababu naamini kuna watu hawezi kabisa kuwa member with EL chairman. I believe wale walio wasafi CDM/CUF/NCCR zitawapokea. Lakini kwa maoni yangu itaongeza changamoto bungeni sababu magamba watapoteza more and more seats!
 
Nyani hawezi kuwa sokwe... Jk, el, malechela hawa hawakuwa chaguo la mwl.. Ni uroho tu wa madaraka ndio uliotufikisha hapa EL ni mroho 2 kwani lazima awe rahisi mmh! Utakuwa ni uwendawazimu hv kwa nini asiendelee 2 kuchunga ng'ombe mmh! Híi Tanzania siyo ya ccm peke yao pia ni ya wazenj na wadanganyika tusio na vyama... Kweli hasidi hachi kutenda husuda ona alicho mtenda dr. Mwakyembe. Sasa hv anaendesha sihasa za kinafiki, kizandiki juu ya mwenyekiti wake... Ambaye kamtoa hata kumpa upm ambao hakustahili na ndiyo maana Mungu ameingilia kati... Atubu kwanza mauji aliyotenda tena asiende mbali kma kwa TB Joshua atubu hata kwa sendolo
Mtanzania a2660783 said:
Kama ana kiu kali ya urais si lazima apitie CCM kama wao hawamtaki vipo vyama vingi tu......CDM, CUF,UDP..........au aanzishe chake(nasikia ana pesa nyingi).......Kugombea nafasi ya uongozi ni haki ya kila raia.........muacheni atumie haki yake labda atabadilika na kuwa kama Sokoine
 
Back
Top Bottom