Hili si ndilo gazeti la mwandishi wake Kubenea kununuliwa na RA ? hili limeisha kosa imani kwa watz
Nimelisoma gazeti la leo la mwanahalisi.Nimekuwa nikifurahishwa na uandishi wa gazeti hili kutokana na umahiri wa waandishi wake.Pamoja na mambo yote mazuri yaliyoandikwa leo,nimefurahishwa na habari inayohusu uchaguzi mkuu wa Bavicha uliomalizika.Hakika kila kitu kimewekwa hadharani.Kuna mgombea mmoja ambaye alituhumiwa kutoa rushwa kwa wajumbe kupitia M-pesa na Tigo Pesa.Wengine tulidhani labda ni majungu tu yaliyosababishwa na wapinzani wake.Kumbe hisia zetu hazikuwa sahihi.Mwandishi wa gazeti la mwanahalisi Alfred Lucas ametoboa kila kitu,ameenda mbali kwa kutaja na kuziandika namba zote zilizopokea pesa hizo mpaka muda zilipotumwa.Hakika hii nimeipenda.Huu ndio uandishi na uchunguzi wa habari tunaoutaka.Hakuna atakayesimama na kusema niliondolewa kwenye mchakato kwa uonevu.Mambo yote yako hadharani.Hata wale Matomaso waliopenyeza uongo wa porini wataamini sasa...........
Hongera Mwanahalisi,waandishi wengine igeni mfano huu.