Elections 2010 Uchaguzi mkuu 2010 kuvurugika?

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52
Yaani huwezi amini. Zikiwa zimebaki siku 5 tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA bado hawajafahamika mpaka sasa.

Mimi nipo katika mkoa wa Dar es salaam. Na nimefuatilia kwa karibu sana zoezi hili la kuchagua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Lakini nimeona kuna ujanja mkubwa unafanywa ili kuingiza wasimamizi ambao kwa namna moja au nyingine watapendelea chama tawala.

Ukienda kwa mkurugenzi wa manispaa iwe ya Temeke, Kinondoni hata Ilala. Ukaulizia majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura atakwambia , majina hayo yameshapelekwa katika Kata husika. Ukienda kwenye kata yako nao wanakwambia hatujaletewa bado hayo majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutoka kwa mkurugenzi .

Lakini katika pita pita zangu mitaani nimepata taarifa kwamba tayari hayo majina yameshatoka na watu sasa hivi wapo kwenye semina za namna ya kusimamia vituo vya kupigia kura na namna ya kuiba kura.

Kama unabisha nenda sasa kwa ama mkurugenzi wa manispaaa husika au kwenye kata yako waulizie hayo majina wameyabandika wapi uone kama watakupa.

Huku viongozi wetu wa siasa wakiwa wamejikita katika kufanya kampeni tu, wakifikiri ndo watashinda , lakini hiyo ni kama kujaza maji kwenye tenga. Maana wenzenu chama tawala mwaka huu wa 2010 watatumia Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika KUCHAKACHUA matokeo ya uchaguzi. Hivyo vyama vya upinzani "kalaga baho" na kubobea katika kupiga kampeni tu, wakati mchakato mzima wa kuwapata Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura unafanywa katika misingi ya KUCHAKACHUA matokeo !!!!

Mwisho ningependa kusema kwamba Zoezi zima la kuwapata WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA mwaka huu katika jiji la Dar es salaam limejaa UFISADI MTUPU !!!

MUNGU IBARIKI DAR ES SALAAM !!!
 
Kwa nini unataka kumfahamu msimamizi wa mtihani? Wewe ngoja siku ya mtihani nenda ingia kwenye chumba cha mtihani na ujibu maswali yatakayokuwa yameulizwa kwenye paper
 
Mhh kaka hii mbona haijatulia?? wala haina mantiki yoyote. Uwajue, usiwajue, uchaguzi utafanyika na this year around haibiwi mtu!!!!
 
Uchaguzi mkuu 2010 kuvurugika??
Hapana mkuu!
Wasimamizi unaweza usiwajue kirahisi, lakini kikubwa hapo ni WAKALA wa chama husika kuwepo!
 
Wewe naona ni walewale wa kuleta uchochezi usiokuwa na maana. Majina ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wewe unayataka yanini? Au ulienda kuomba usimamie ukanyimwa? Ninachojua ni kwamba wasimamizi wataanza semina Alhamis kuhusu namna ya usimamiaji wa kupiga kura, kuwaelekeza matumizi ya kile kitabu chenye majina ya wapiga kura na kitu kama hicho. Sasa hiyo habari ya kwamba wanakwenda kujifunza kuiba kura zimetoka wapi? Mimi ni mmoja wa watu walioteuliwa kwa ajili ya kusimamia na sijaambiwa kwamba tutafundishwa namna ya kuiba kura. Jaribuni kuwa wakweli basi!!
 
Kwa nini unataka kumfahamu msimamizi wa mtihani? Wewe ngoja siku ya mtihani nenda ingia kwenye chumba cha mtihani na ujibu maswali yatakayokuwa yameulizwa kwenye paper

Miaka yote wasimamizi wa wa vituo vya kupigia kura majina yao yalikuwa yakibandikwa wiki mbili kabla ya siku ya uchaguzi.Halafu hat semina za wasimamizi wa uchaguzi zilikuwa zikifanyika mapema sana. Tena zilikuwa si semina za vificho. Iweje mwaka huu , Majina ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura iwe siri ???

Kwanza embu jiulize hata hayo majina yakibandikwa kesho hizo taarifa zitawafikia vipi walengwa ??? Halafu mbona huku mtaani kwetu tayari hizo semina za wasimamizi wa vituo vya kupigia kura watu wameshaanza kupewa ??? Kwa nini zoezi hili la uchaguzi mwaka huu linaendeshwa kwa usiri mkubwa, tofauti na chaguzi nyingine zilizopita ???? Kuna nini cha magendo kinaendelea katika Uchaguzi mwaka huu . Au ndio mipango yenyewe hii ya KUCHAKACHUA matokeo ???
 
halingumu ngumu taadhari yangu ni ya muhimu kuzingwatiwa. lolote linawezekana kutoka CCM. Cha msingi tuwaangalie kwa umakini sana
 
Wewe naona ni walewale wa kuleta uchochezi usiokuwa na maana. Majina ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wewe unayataka yanini? Au ulienda kuomba usimamie ukanyimwa? Ninachojua ni kwamba wasimamizi wataanza semina Alhamis kuhusu namna ya usimamiaji wa kupiga kura, kuwaelekeza matumizi ya kile kitabu chenye majina ya wapiga kura na kitu kama hicho. Sasa hiyo habari ya kwamba wanakwenda kujifunza kuiba kura zimetoka wapi? Mimi ni mmoja wa watu walioteuliwa kwa ajili ya kusimamia na sijaambiwa kwamba tutafundishwa namna ya kuiba kura. Jaribuni kuwa wakweli basi!!

Yaani wewe unaonekana ni mgeni kabisa katika zoezi la uchaguzi mkuu na kuwa msimamizi wa kituo cha kupigia kura. Kwanza ningekuuliza swali moja Dar es salaam peke yake ina vituo vingapi vya kupigia kura ??? Kila kituo kina Wasimamizi wangapi ??? Je taarifa kwa waliopata nafasi ya kuwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura huwafikiaje ??? Wanapigiwa simu ??? Lool... mwenzangu upo nchi hii kweli ???
 
Yaani huwezi amini. Zikiwa zimebaki siku 5 tu kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA bado hawajafahamika mpaka sasa.

Mimi nipo katika mkoa wa Dar es salaam. Na nimefuatilia kwa karibu sana zoezi hili la kuchagua wasimamizi wa vituo vya kupigia kura. Lakini nimeona kuna ujanja mkubwa unafanywa ili kuingiza wasimamizi ambao kwa namna moja au nyingine watapendelea chama tawala.

Ukienda kwa mkurugenzi wa manispaa iwe ya Temeke, Kinondoni hata Ilala. Ukaulizia majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura atakwambia , majina hayo yameshapelekwa katika Kata husika. Ukienda kwenye kata yako nao wanakwambia hatujaletewa bado hayo majina ya Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kutoka kwa mkurugenzi .

Lakini katika pita pita zangu mitaani nimepata taarifa kwamba tayari hayo majina yameshatoka na watu sasa hivi wapo kwenye semina za namna ya kusimamia vituo vya kupigia kura na namna ya kuiba kura.

Kama unabisha nenda sasa kwa ama mkurugenzi wa manispaaa husika au kwenye kata yako waulizie hayo majina wameyabandika wapi uone kama watakupa.

Huku viongozi wetu wa siasa wakiwa wamejikita katika kufanya kampeni tu, wakifikiri ndo watashinda , lakini hiyo ni kama kujaza maji kwenye tenga. Maana wenzenu chama tawala mwaka huu wa 2010 watatumia Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika KUCHAKACHUA matokeo ya uchaguzi. Hivyo vyama vya upinzani "kalaga baho" na kubobea katika kupiga kampeni tu, wakati mchakato mzima wa kuwapata Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura unafanywa katika misingi ya KUCHAKACHUA matokeo !!!!

Mwisho ningependa kusema kwamba Zoezi zima la kuwapata WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA mwaka huu katika jiji la Dar es salaam limejaa UFISADI MTUPU !!!

MUNGU IBARIKI DAR ES SALAAM !!!
 
Binti yangu pia kateuliwa kusimamia kituo na semina anasema Alhamisi.

Unaniambia atafundishwa kuiba kura? Usipende kutoa allegations usizokuwa na uhakika nazo!

Kama una kithibitisho kiweke hapa nimshauri binti yangu kuachana na shughuli hiyo.
 
Wacha wawaweke wanaowataka na kuiba hawawezi. Tutawabana mbavu maana na sisi ni wajanja kuliko......................
 
Back
Top Bottom