Uchaguzi mdogo Magogoni: Matokeo

Hasira za nini au za kushindwa?
za kuchezewa demokarasia na akili za wananchi, unafkiri hili igizo walilofanya Magogoni litaishia hapo? mpaka 2010 watakuja na ubaradhuli kama huu wa kuchezea demokarasia na kulazimisha kushinda.aaagh
 
Asalamu alaykum.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni umefanyika kwa usalama na amani na hakuna udanganyifu uliofanyika katika upigaji kura kwa ile jana tatizo kubwa lilikuwa wakati wa uandikishaji kuna watu wengi sana walikataliwa kuandikishwa kutokana na kutokuwa na vipande vya ukaazi ambavyo waratibu wa vipande hivyo ni viongozi wa serikali za mitaa (masheha) wanatuhumiwa kutoa vipande hivyo kwa ubaguzi mara nyingi hukataa kuwapa watu wenye asili ya pemba.

Tatizo jengine sio kama watu wamechoka na upinzani lakini kutokana na hali za maisha zilivyo ngumu wananchi wanachoka kukipa chama ambacho kila kinapotokea uchaguzi kinakoseshwa ushindi hivyo wananchi wengi wamekata tamaa lakini kubwa zaidi kuliko yote wananchi wengi hawana elimu ya uraia na hivyo wamekuwa wakitilia chama ambacho wanaamini hata kama hukukipa kitashinda tu kwani mara kadhaa viongozi wake wamesikika waksiema hawatoi nchi kwa kura kwa kuwa wamepindua.

lakini pia wananchi wengi hawajajitokeza kupiga kura kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuvunjika moyo, kuogopa kwa kuwa kila uchaguzi unaofanyika zanziabr huwa hauna salama lakini zaidi kazi ya kuihamasisha jamii haikuwa kubwa hivyo wananchi wengi wameona huu ni uchaguzi ambao hausaidii kitu katika kubadilisha utawala.

kila la kheri huo ni mtazamo wangu
Usitoe sababu za hewani, CUF hata siku moja hawatakuwa na ubavu wa kushinda Magogoni, na lile jimbo la Jina lako mkae mkao wa kulipoteza 2010.
 
Kura za Chadema zipo wapi?

Nadhani hawakushiriki uchaguzi ngazi ya tawi! Kwani hilo tawi lilikuwa na mashina mangapi? Kwani naona walojitokeza ni sawa na wapiga kura wetu hapa Mkanyageni, Tanga!
 
Nadhani hawakushiriki uchaguzi ngazi ya tawi! Kwani hilo tawi lilikuwa na mashina mangapi? Kwani naona walojitokeza ni sawa na wapiga kura wetu hapa Mkanyageni, Tanga!
Si useme tu kuwa hawana ubavu wa kuvuka bahari!
 
Kule Bara na Sangara wao, CCM kaingia na Tilapia..! Chadema leo wapo kidogo sana hapa Ukumbini! Poleni sana!
 

- Hoya! na huku nako hata viongozi wakuu hawakuenda lakini ushindi tu, saafi sana wananchi wanaelewa CCM ina viongozi wachache wabovu sio wote!

Respect.

FMES!


Mkuu naswali kama board directors pamoja na managing director wa kampuni wachafu...dereva, secretaries, marketing managers, pr managers na staff wengine watafanya kazi kwa usanifu kweli? wanaweza kukiuka policy ya kampuni??
 
Mkuu naswali kama board directors pamoja na managing director wa kampuni wachafu...dereva, secretaries, marketing managers, pr managers na staff wengine watafanya kazi kwa usanifu kweli? wanaweza kukiuka policy ya kampuni??

- Mkuu ongelea uchaguzi, nani ameshinda na kwa nini nani kashindwa na kushinda, uchaguzi tayari CCM wameshinda sasa ya directors siyajui yana uhusiano gani na ushindi wa CCM Busanda na Magogoni?

Respect.

FMEs!
 
Back
Top Bottom