Uchaguzi Igunga: DC apata kisago kutoka kwa wana- CHADEMA

Nafurahi sana kusikia DC kachezea kichapo
wamezidi hivyo ndivyo wanavyoweza kurekebishika labda wataacha agenda zao za kuchakachua

Hata mimi napenda amani na whatever, lakini kwa hili, ningetumia misuli yangu yote ya triceps and biceps kutembeza kichapo kwa huyo jamaa...!! Hawa ndiyo wanaotuletea matatizo, ndo hawa akina Kabwe, na wengine ambao wanafikiri watapewa vyeo vya upuuzi huu..!!

Mie nipo Igunga,na ninachokisema ndio haswa kimetokea,kimsingi hatakiwi kabisa kuwa kwenye eneo tunalofanyia mkutano,kwani ratiba ipo wazi,lakini pia kutaka kuwalagai wananchi ni uwendawazimu
Unauhakika na unachokiongea mkuu? unataka kututhibitishia kuwa ni kweli huyo DC hajapigwa? na kama hajapigwa, vipi hajafanyiwa vurugu
zozote toka kwa wanachama wa CDM? tujuze mkuu

Siafiki namna hii ya kukabiliana na watu tusiokubaliana nao.

Mkuu, kama wasomi sisi tuwe wa kwanza kuhubiri amani na ufuatwaji wa sheria tulizojiwekea. Naamini mzee wangu Slaa na Lissu wangeweza kuchukua maamuzi sahihi kuwawakilisha wadau/wanachama wao katika kudai haki zao.

Hivi tunaelekea wapi? Imekuwaje hadi akapewa kisago? Hakukuwa na ulinzi? Naye kwanini afanye hujuma?

mkuu heshima,
siungi mkono moja kwa moja vurugu, lakini naamini kuna wakati vita (kama vya kagera) au kumpiga mtu huwa ni the best wisdom to opt. ipo gharama kubwa kulipia option hii, lakini ndilo chaguo lenye hekima bora iongozwayo na busara ya mwangwi wa tukio.
hatuwacheki leo waliomshangilia kibanga kumpiga mkoloni, kwa sababu matendo ya wakoloni yahakukubalika na jamii, na jamii haikukosea kwa hilo. pengine itakuwa ni funzo wanapopewa semina elekezi wapinge baadhi ya maagizo kandamizi ambayo yanaweza kuamsha ujasiri wa wananchi ambao ni nadra kutokea. Toka enzi za kibanga mpaka leo tegemea wakandamizwaji kushangilia. pole dc

Kwanza walianza kutumwagia tindikali sasa wameanza kuwapiga viongozi wetu wa nchi na mwisho wataanza kurusha mawe ikulu. Hili halikubaliki na lazima wafungiwe kufanya kampeni kabla ya uchaguzi ili washike adabu. Narudia tena, hili halitavumiliwa.

wewe unachezea meno ya Simba unatarajia nini yaani nyie mtupigie rafi tuwaangalie tuu?

haya tuliyategemea, tindikali kisha mapanga, ikafuata kumbaka binti, tena DC, Hii ndio chadema iliyopeleka MUNGIKI na INTARAHAMWE, na hawa intarahamwe wanapenda kubaka hawa!

Mie nipo Igunga,na ninachokisema ndio haswa kimetokea,kimsingi hatakiwi kabisa kuwa kwenye eneo tunalofanyia mkutano,kwani ratiba ipo wazi,lakini pia kutaka kuwalagai wananchi ni uwendawazimu

Wewe haupo Igunga ila upo Chuo cha ualimu Mpwapwa. Hizo propaganda za kitoto hazikufai. Mimi nimepigiwa simu na kiongozi wa CCM na amesema ni kweli tukio limetokea na Mkuu wa wilaya amejeruhiwa jicho la kushoto na sehemu ya mbavuni. Suti yake imechanwachanwa na ilibidi watu wamuazime suruali.

Hawa ma-DC huwa hawana kazi kwani hawapo kabisa kikatiba! Ni wanasiasa tu waliowekwa na kazi yao kubwa ni wakati wa chaguzi -- kuhakikisha CCM inashinda. Na kwa vile wengi wao siyo wasomi, na huteuliwa kwa kujuana tu, basi huwa wana ka-ujeuri fulani ka-kufanya mambo watakavyo, kwani nani atamuuliza?

Kwa mantiki hii mara nyingine ni sahihi kushikishwa adabu hasa wanapojiingiza katika masuala kinyume na sheria au utaratibu. Hao wana-CDM hata wangeenda polisi kuripoti, polisi wasingefanya chochote -- sasa wangeenda wapi au wafanye nini katika kupunguza hasira zao?

Kwa ujumla serikali ya CCM inatupeleka kwenye maafa. Juzi utawala wao mbovu umesababisha vifo vya mamia ya watu huko Visiwani na angalia jinsi wanavyosuasua kuwakamata wahusika na kuwawajibisha. Kwanza hata kumtaja mmiliki wa meli wanapata kigugumizi -- kwani ni mwenzi wao.

Hizi zote ni njaa,na mabilioni au milioni yanayotumika Igunga yananitisha. Ningeshauri turudi wakati ambao mbunge alikuwa na kiatun pea moja yenye soli iliyotoboka. Au enzi ambayo waziri mkuu alikuwa annavaa buti za jeshi na kaunda suti(Sokoine). Haya maposho yanaua vijana,wazee na watoto wetu directly au indirectly..... It's a shame tulivyo tayari kupoteza maisha yetu kwa ajili ya hawa punda wenye tamaa  za hela.
Kila nikimuona mwanasiasa yoyote wa Tanzania, nakumbuka enzi zangu za SUA na vili vienyekiti vinavyoitisha kunji ilhali wao wanakula vimichango vyetu....wezi tu hawa hawana mpango!
Kwa nch kama Tanzania inabidi uombwe na ubembelezwe na wananchi kuongoza, na hao watu waliompiga DC, ikiwezekana washtakiwe na wahukumiwe adhabu ya kifo kwa njia ya kunyongwa, ingekuwa barabara zaidi kama wangepigwa kitanzi hadharani. Demokrasia siyo mfumo mzuri kwa watanzania.

Unawazimu sana Kobello! Hao ccm na serikali yake wameua raia wangapi wasio na hatia na hawajajichukulia action yoyote, Ila kwa vile DC kapigwa
wakati akitekeleza maagizo kutoka juu ndiyo unaona bora hao watu wanyongwe? unawazimu sana mruguru wewe

Punde nimepokea habari kutoka Ingunga kuwa DC wa wilaya hiyo kapata kipigo kutoka kwa wana chadema waliomtuhumu kuhusika katika njama za kuwahujumu katika moja ya mkutano.

soon nitaweka udhibitisho wa habari hizi au nitarudi kusema kama imedhibitika kuwa ni uongo.

kumbuka hii bado ni tetesi .

Byabato

May be

haya tuliyategemea, tindikali kisha mapanga, ikafuata kumbaka binti, tena DC, Hii ndio chadema iliyopeleka MUNGIKI na INTARAHAMWE, na hawa intarahamwe wanapenda kubaka hawa!

Kwa nini pia hutaji wale Gestapo wa CCM? Mwaka jana pekee wameuuwa wananchi 52 wasiyokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi. Na hakuna aliyeshitakiwa. Hii ni sheria ya wapi? Mbinguni? Nao si pia wanachangia kutupeleka vitani?

Mie nipo Igunga,na ninachokisema ndio haswa kimetokea,kimsingi hatakiwi kabisa kuwa kwenye eneo tunalofanyia mkutano,kwani ratiba ipo wazi,lakini pia kutaka kuwalagai wananchi ni uwendawazimu
Usituletee mambo yako ya kipuuzi, hebu nipe sheria inayomkataza DC kutokuhudhuria mkutano wa hadhara. Huo nio mhadhara na mtu yoyote anaweza kuhudhuria...vikao vyenu vya kamati au halmashauri zenu zinahudhuriwa na wajumbe....ila hadharani mtu yoyote anaweza kuhudhuria.....Acha pumba/mataputapu!!

Ikiwa tumekubaliana kupongeza KINJEKITILE,MKWAWA,na wengioneo kwa maovu yaliyofanywa na Wakoloni,basi kwa sasa ni yepi yanayofanywa na CCM huwezi ukatofautiasha na wakoloni. bila shaka amevuna alichostahili hili ni vunzo kuwa WANANCHI WEMECHOSHWA NA UPUUZI WA CCM UKIZIDI ya libya Tunisia na Misri si ajabu kutokea

Kwa nini pia hutaji wale Gestapo wa CCM? Mwaka jana pekee wameuuwa wananchi 52 wasiyokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi. Na hakuna aliyeshitakiwa. Hii ni sheria ya wapi? Mbinguni? Nao si pia wanachangia kutupeleka vitani?

Nitajitundika iwapo huyo Mzee wa mawe anajua maana ya hilo neno ulilolitumia - Gestapo! hakika nitajitundika!

dc_igunga.jpg
DC baada ya kuzuiwa kuvuruga kampeni za chadema akiwa chini ya ulinzi, akihojiwa na waandishi wa habari wakati mkutano unaendelea.

Kwanza walianza kutumwagia tindikali sasa wameanza kuwapiga viongozi wetu wa nchi na mwisho wataanza kurusha mawe ikulu. Hili halikubaliki na lazima wafungiwe kufanya kampeni kabla ya uchaguzi ili washike adabu. Narudia tena, hili halitavumiliwa.

sikupendi! Kwanini hufi?

Back
Top Bottom