Uchaguzi CUF: Prof. Lipumba ambwaga Prof. Safari

Watu wamechagua Kiongozi ambae anaheshimika ndani ya Nchi na nje ya Nchi yaani wamemchagua kiongozi ambae ujuzi alionao unawasaidia watu wa ulimwengu wa Kwanza huko maulaya ,hivi hili halitoshi ,kuwaonyesha WaTanzania walio wengi ,unajua kutokana na methali ya kiswahili ile isemayo Kila mdharau chake hakika amepotoka, hivyo tukubali kuwa wale wanaomuona Lipumba si lolote si chochote ,wajue wanaingia katika kundi hilo la waliopotoka ,sasa hapa kuna kisa ambacho walimwengu walitushangaa tumemtupa Salim Ahamed kwa sababu ni muarabu au sijui alikuwa hizbu,unajua hata walimwengu walimshangaa sa na Baba yenu wa Taifa ,alipomwacha Salimu na kumuweka Mkapa na juzi walimwengu walitushangaa walipomuwacha Salimu na kumuweka mpiga filimbi wa melini Kikwete ,mjue watu wanatucheka na haya yanayotrokea ni mambo ambayo tumejitakia ,hatukuweza kuchagua na kama tumechagua tulishindwa kulinda.

Msifanye mchezo katika kuchagua viongozi ,hili nawasihi sana wenzangu waTanzania jambo la kucheza na jazba na kiburi ndilo linalotufikisha pabaya sana na ndipo tunapopoteza dira ,kama tunahitaji shida na mchezo mchezo katika kuwapiga vita viongozi wanaoheshimika basi mjue tutabaki kupiga makelele na mayowe ya njaa.

Kuna wafinyu wa fikra ambao wanahoji eti amelifanyia au amefanya nini huko kijijini kwake ? Mnasahau kuwa wanaofanya mambo huko vijijini ni mafisadi tu ,hakuna jingine wizi mtupu ,ndio maana yake ,kiongozi aliesafi hatizami pale kijijini anapotoka bali huitazama Tanzania nzima kwa ujumla ,ukagombee sijui ubunge kijijini ili iwe nini ? Kama si kufanya ufisadi katika nyanja za serikalini ili uonekane unaimani na kijijini kwenu ,au sio ,wabunge wengi matajiri ni wala rushwa na watoa rushwa wakubwa katika mikoa yao ,hawa ndio wanaowalishia polisi na vyombo vingine ili wapate ulaji, hakuna chochote walichonacho cha kuwapatia fedha kihalali ni wizi tu,wizi mtupu.Tena nini kama si wizi ?

Viongozi hawa akina Lipumba au Salim watakapoweza kutwaa au kuchaguliwa kihalali kabisa na wananchi mi nawahakikishieni mageuzi ya kweli lazima yatatokea hapa Tanzania ,tusifanye masihala , ni watu ambao uongozi wao hauonekani kuwa na mbia na mtu yeyote wabia wao ni mtazamo wa wananchi wa Tanzania kwa ujumla bila ya kujali itikadi zao ,hebu fikiria tokea jamaa Kiwete afanye ziara Pemba hadi leo hakuna umeme wala hakutoki maji ,mtu ajiulize huyu alikwenda kufanya nini Pemba ,maana amerudi na chuki ,iweje hadi leo hakuna umeme ,Pemba hawana mawasiliano kabisa ,ndio hata simu huwezi kuwapigia ,yaani hata kuchaji simu zao hawajui wafanye nini ,halafu mnasema CCM ndio baba ,ni kosa la kutolinda ushindi baada ya kuhakikisha kuwa aliepewa ushindi sie alieshinda na matokeo yake ndio haya ya kuogopana na kucheleweshana ,vipngozi wanaoingia kwa wizi hawana nguvu za kuongoza nchi,hilo tukubali ,tunamuona Kikwete ,tunamuona Karume tunawaona na wengine hawawezi kusema kitu ni woga,wanaogopa kutobebwa tena katika chaguzi zijazo ,ila wananchi lazima waamshwe kama ni vita na wanaowabeba viongozi hawa mapepe basi ni bora viwepo vita kuliko kuendeshwa kibabe na kuonyeshana meno kama wanaotangaza tangazo la dawa za mswaki.
 
Kuna kitu kinaitwa political posturing jamani.....CUF inaelekea somo la MABADILIKO na USHINDANI halijawaingia sawasawa. Nobody refutes Lipumba competence as economist ingawa alikuwa ndio mshauri wa Mzee Mwinyi enzi zile but nyakati hizi zinahitaji zaidi ya hilo. Na hili suala la asilimia 99 kwa kweli haliwasaidii CUF kwani haliandani na dhima ya siasa za ushindani aka Demokrasia za enzi hizi.

Kwa kweli nina wasiwasi kama CUF inaweza kuondokana na hali ya "political stagnation" na zaidi kunatoa mwanya kwao kuendelea kupoteza mvuto badala ya kujijenga. Matokeo yake wataendelea na siasa za unazi dhidi ya wapinzani wenzao wanaonekana kuwapiku katika umuhimu kisiasa nchini. Mwisho wa siku neema kwa CCM ukitilia maanani uwezo mno (ingawa) unakua wa CHADEMA katika kutumia mianya iliyopo kujijenga zaidi.
 
Hivi hang'atuki huyu, hasemi basi sasa? Jipya lake ni lip? Au ameazima ukurasa wa viongozi wa CCM?

Hivi kwani CCM hawangatuki. Au unataka kuniambia kuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi. Ben Mkapa bado ni Wenyeviti Washirika wa CCM
 
Kwani Profesa Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa CUF toka Mwaka gani? Miaka kumi na tano kwenye uenyekiti wa chama sio mingi sana jamani. Mbona hata raisi wa nchi anakaa kwa vipindi viwili vya miaka 10 jumla? Cha ajabu nini kwa Lipumba kukaa madarakani CUF kwa vipindi vitatu?

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni

......ndiyohiyo
 
Pof. Lipumba apata ushindi wa tsunami (98.6%), Prof. Safari mmmhhh! apata chini ya kura 10.

Profesa Lipumba ameibuka mshindi wa kinyang'anyiro cha Uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu uliohitimisha mkutano mkuu wa 4 wa chama hicho katika ukumbi wa Diamond, jijini DSM hapo jana usiku. Profesa Lipumba alipata kura 600 kati ya kura 669 zilizopigwa na kuwashinda wagombea wengine wawili kwa asilimia 98.6. Wagombea wengine ni koplo Stephen Masanja alipata kura 10 (1.5%) na Profesa Abdalah Jumbe Safari aliyepata kura 6 (0.9%).

Maalim Seif Shariff Hamad naye aliweza kutetea vyema kiti chake cha Ukatibu Mkuu baada ya kuzoa kura 657 (99.5%) ambapo 4 zilisema hapana na 2 ziliharibika. Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo kama alivyokuwa Makamu wa Mwenyekiti, Mwanasheria Khamis Othman Machano aliyepata kura 653 (98.6%) ambapo 5 ziliharibika na 4 zilisema hapana.

Hongera zenu uongozi mpya (but karibu sura ni zile zile), leteni mabadiliko ya fikra mpya kuelekea ktk maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa madiwani mwaka huu na uchaguzi wa Rais na Wabunge hapo mwakani panapo uhai na uzima.
 
Last edited:
Demokrasia ya vyama vyetu bwana?

Si angeteuliwa tuu kama wa CCM?

Mbatia aliwekwa na mshindani hewa ambaye wala hakuwepo kwenye mkutano husika sasa Lipumba kashinda kama vile hakuwa na mpinzani ngoja tumsikie Safari atatoa kauli gani.

The problem is you don't know what is inside,kwa data nilizopata toka kwa jirani sina uhakika nazo sana nikuwa huyo jamaa Prof Safari alikuwa planted na chama kongwe Tz kisichotaka toka madarakani.Jamaa wakapata issues wakampiga chini kwa kura sita.Noma sana
 
Demokrasia ya vyama vyetu bwana?

Si angeteuliwa tuu kama wa CCM?

Mbatia aliwekwa na mshindani hewa ambaye wala hakuwepo kwenye mkutano husika sasa Lipumba kashinda kama vile hakuwa na mpinzani ngoja tumsikie Safari atatoa kauli gani
.

The problem is you don't know what is inside,kwa data nilizopata toka kwa jirani sina uhakika nazo sana nikuwa huyo jamaa Prof Safari alikuwa planted na chama kongwe Tz kisichotaka toka madarakani.Jamaa wakapata issues wakampiga chini kwa kura sita.Noma sana
Hata hivyo Prof Safari is not popular sana miongoni mwa wana CUF na wananchi kwa ujumla,watu wengi hata hapa JF walikuwa hawana CV ya jamaa.
Tunaomba upepo huu uvume kuelekea Chadema,Zitto chukua fomu ugombea na Mbowe tuone.
 
Aahh; Ya ngoswe hayo... Ukisema tu mawe!!

Lipumba na Mrema are the "best losers in Tz" - let Lipumba for a third/fourth straight defeat in his ever-diminishing presidential contest

Akishamaliza kazi yake... Atarudi CCM kwa shangwe na vigelegele

Katumwa huyo... we haya we!!!
 
Hongera zenu uongozi mpya (but karibu sura ni zile zile), leteni mabadiliko ya fikra mpya kuelekea ktk maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa madiwani mwaka huu na uchaguzi wa Rais na Wabunge hapo mwakani panapo uhai na uzima.

Junior
CUF waeona yaliyotokea CCM, sura mpya nyingi lakini zimefanya ufisadi kuwa ndio sera. Kwa hiyo issue naona sio sura bali ni uwezo wao kulinda itikadi ya chama na kuw viongozi wa kweli, na sio wasanii
 
Aahh; Ya ngoswe hayo... Ukisema tu mawe!!

Lipumba na Mrema are the "best losers in Tz" - let Lipumba for a third/fourth straight defeat in his ever-diminishing presidential contest

Akishamaliza kazi yake... Atarudi CCM kwa shangwe na vigelegele

Katumwa huyo... we haya we!!!

Are you sure with what you are talking? Mrema amefanyiwa fitna ya kutosha na usalama. Amefanyiwa njama nyingi, Lipumba sio loser amejenga CUF na kukifanya chama ambacho kimefka kwenye grassroot kwa muda mfupi sana. How can you call them losers? You should look at them with an open mind ndio uweze ku-judge kama wao ni losers au la.
 
Hivi kwani CCM hawangatuki. Au unataka kuniambia kuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi. Ben Mkapa bado ni Wenyeviti Washirika wa CCM.

Katika CCM wansng'atuka kinusunusu tu -- bado wana kauli kubwa katika maamuzi nyeti. Lakini maana yangu hasa haikuwa wenyeviti wa taifa, bali wale wengine -- akina Kingunge, J. Malechela, Msekwa n.k.
 
Kwenye CCM ndio hakuna kungatuka anaeondoka huwa mkubwa zaidi na ndio anaetoa kauli ya mwisho ,huko ndio kuna ile migogo ambayo imeota mijizizi ,mafioso ,wapo tayari kuua wakiona unakodolea macho tonge zao.
 
SIKU mbili baada ya kuangushwa vibaya katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Abdallah Safari amesema wajumbe wa mkutano mkuu walimdhalilisha na kwamba anaandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo.

Profesa Safari alitoa malalamiko hayo jana alipozungumza na Mwananchi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo uliomrudisha madarakani Profesa Ibrahim Lipumba, aliyepata kura 646, huku mpinzani huyo akiambulia kura sita tu.

Wakati Profesa Safari akijieleza, wajumbe walikuwa wakimzomea na baadaye kumrushia maswali yaliyomtingisha, ikiwa ni pamoja na kutaka ataje jina la katibu wa tawi lake, swali ambalo alibabaika kulijibu.

"Nimedhalilishwa; nimezomewa; nimeulizwa maswali ya kipuuzi. Ule ni uhuni hakuna kitu pale," alisema Profesa Safari.

"Wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wamepotosha na kuharibu maana ya demokrasia ndani ya CUF na kutumia vibaya nafasi hiyo ya kuchagua viongozi."

Alipobanwa kueleza iwapo anafikiria kuwania tena nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, Profesa Safari alisema hawezi na hana nia ya kuwania uongozi wa chama hicho.

"Sifikirii wala sina nia tena ya kuwania nafasi yoyote ndani ya CUF. Nitakapoita mkutano na waandishi wa habari, nitaeleza mengi. Mbali ya kuzindua kitabu changu, nitaamua shauri la kufanya pamoja na kesi ya uanachama wangu," alisema Profesa Safari.

Hata hivyo, wanasiasa wengine wanaona kuwa uchaguzi huo wa viongozi wa CUF umeonyesha kukomaa kisiasa.

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema CUF imeonyesha demokrasia na kumpongeza Prof. Lipumba kwa ushindi wake wa asilimia 97.

"Inaonyesha jinsi wana CUF walivyo na imani naye. Uchaguzi wa CUF umeonyesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama hicho, nawapongeza pia wana CUF kwa hatua hiyo," alisema Mrema.

Wakati huohuo, Said Salim anaripoti kuwa viongozi wapya wa CUF, wametoa salamu kali kwa CCM, wakisema kuanzia sasa suala la kuibiwa kura zao katika chaguzi mbalimbali nchini, limekwisha.

Wakizungumza mara baada ya kurejeshwa madarakani katika mkutano mkuu unaoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, viongozi hao walisema hawataruhusu tena wizi wa kura.

Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema atahakikisha anatumia ridhaa aliyopewa kukipanga chama na kuhakikisha kuwa wanashinda kila uchaguzi watakaoshiriki.

"Mfano mzuri wa kukataa kwetu kuibiwa kura tutaonyesha katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Magogoni Zanzibar... ni jimbo letu lakini tuliibiwa lakini lazima tuligomboe," alisema Hamad.

"Tunasikia kuwa tayari CCM wameshaandaa kura zao kwa ajili ya kujazia lakini nawapa salamu kuwa, watakavyoipiga ndivyo tutakavyoicheza. Hakuna tena msalia Mtume katika kulinda kura setu".

Aidha aliwataka wanachama wake kushikamana kwa pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya vikao vya chama ili wakitoka wafanye kazi kwa ushirikiano na mshikamano.

"Tumalize tofauti zetu ndani ya vikao vyetu, tukitoka nje tukisema tuvute kamba basi tuvute kwa pamoja, tukisema tuache tunaacha sote. Nitakuwa nanyi; sitawaangusha hadi tulifikishe jahazi bandarini salama salimini," aliahidi Hamad.

Naye makamu mwenyekiti mteule wa CUF, Machano Khamis mabaye alikuwa mshitakiwa nambari moja katika kesi ya uhaini iliyokabili viongozi 17 wa chama hicho mwaka 1997 hadi 2001 alisisitiza, kwa kuwa CCM ni wababe na wao lazima wafanye ubabe ili kukataa wizi wa kura.

"Wizi wa kura sasa basi; ikiwa wao ni wababe na sisi ni wababe vilevile; wakitunisha misuli na sisi tutatunisha. Hatutafanya vinginevo kwa kuwa tukifanya vingine, CCM wataendelea kujenga kiburi," alisistiza Khamis na kuongeza:

"Tukatae CCM kuchukua kura zetu kwa nguvu kwa kuwa wao hawana haki ya kutawala."

Alisema, ameshakaa jela mara nyingi, kwa hiyo hana tena woga na yuko tayari hata kupoteza maisha kwa kulinda maslahi ya umma.

"Haya ya kuwa siogopi, ndugu wajumbe, yanathibitishwa na kugombea tena nafasi hii. Kwa mateso niliyoyapata kwa kukaa jela, kama ningekuwa muoga ningekwishakaa nje ya chama hiki," alisema Machano.

"Katika uchaguzi huu, tumewafundisha CCM namna demokrasia inavyotakiwa. Katika chaguzi zao kuna rushwa, kupigana, kuchafuana na makundi lakini kwetu kuna amani, utulivu na upendo baina ya wanachama na wagombea."

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema amepewa jukumu zito na uzito wake unatokana na chama dola kung'ang'ania madaraka hata kama hakitakiwi nchini.

Alisema, licha ya ugumu huo, atahakikisha kuwa katika awamu hii wizi wa kura unakoma katika chaguzi nchini na wataanzia katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Magogoni na ule wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu.

"Ndugu wajumbe uchaguzi wa Magogoni ndio utakuwa kipimo cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010... kama tutakuwa na uchaguzi au mapambano; kama uchaguzi au uchafuzi," alisema Prof. Lipumba.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la uwakilishi la Magogoni la kisiwani Zanzibar umepangwa kufanyika Mei 23 baada ya kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo, Daud Hassan Daud.
Source: Gazeti la Mwananchi
 
LIPUMBA aja na kura za CHINA!
UKIMPIGIA safari zinahamia kwa lipumba, ni teknolojia inayotumika katika chaguzi tata! mshindi anaweza pata ushindi hata aslimia mia mbili (200% win) (JOKE...!)

Mkuu, kwani wana CUF wenyewe wanasemaje inawezekana wameridhika na Lipumba sijasikia manung'uniko kutoridhishwa na Lipumba. Hapa labda Lipumba mwenyewe angekuwa muungwana awape nafasi na wenzie.
 
Aliyekuwa mgombea uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na kubwagwa, Profesa Abdallah Safari, amesema hatathubutu kugombea nafasi yoyote katika chama hicho na kuahidi kutoa msimamo wake mwishoni mwa mwezi ujao, juu ya hatma yake ndani ya CUF.

Akizungumza na gazeti hili leo, Profesa huyo wa Sheria ingawa alikataa kusema kama atakihama chama hicho au atabaki, alisema: “Katika uchaguzi huu nimeonekana kama sitakiwi, nimedhalilishwa, na mtu kama hutakiwi huwezi kukaa, muungwana utaondoka tu.

“Ni kawaida kwa mtu kuhama chama kimoja kwenda kingine, sisemi nitahama na hakuna aliyenifuata nihamie chama chake, lakini naweza kusema sikioni chama makini hapa kwetu hata nilichomo cha CUF”.

Alisema katika uchaguzi huo amekashfiwa, amezomewa na kuonekana kama kulikuwa na mpango wa kumwaibisha na uthibitisho wa hali hiyo ni maswali yaliyoulizwa na wajumbe. “Unaweza kuona mtu kama Hamad Rashid Mohamed alivyoniuliza swali la kitoto vile, wakati anajua mchango wangu ni mkubwa katika chama hicho,” alisema.

Hamad alimuuliza kama ataweza kuwatetea Watanzania wakati alikataa kukitetea chama hicho kilipofungua kesi ya kupinga ubunge wa Afrika Mashariki na kumlipa Tundu Lissu Sh milioni nne kutetea kesi hiyo. Katika uchaguzi huo, Profesa Safari alikuwa mgombea ubunge wa Afrika Mashariki.

Alisema mwishoni mwa mwezi ujao, wakati atakapozindua rasmi kitabu chache cha ‘Haja ya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi’, ataelezea msimamo wake juu ya hatma ya kuendelea kuwa katika chama hicho. Alisema anaamini kilichochangia kushindwa kwake katika uchaguzi huo uliofanyika juzi, ni uelewa mdogo wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama hicho waliompigia kura.

“Mimi na viongozi wa juu wa CUF wakiwamo Profesa Lipumba (Ibrahim) na Maalim Seif, tunatofautiana, wao wanataka chama kishiriki katika uchaguzi, mimi sitaki mpaka kuwe na tume huru kwani bila kupigania kuwapo tume huru, hatutaweza kushinda uchaguzi, hivyo popote nitakapokuwa, nitasimamia kupatikana kwa tume huru,” alisema Profesa Safari. Malalamiko ya Profesa Safari yamekuja siku moja baada ya kutangazwa kushindwa katika uchaguzi huo ambapo alipata kura sita akiwa ameshika nafasi ya mwisho. Profesa Lipumba alipata kura 646 huku Stephen Masanja akipata kura 10.

Source: Gazeti la Habari Leo
 
Wakuu,

Katiba ya CUF inamruhusu mwanachama wake yeyote kupiga na kupigiwa kura kila kwenye uchaguzi bila ya kikomo. Nayo hiyo ni demokrasia inayokubalika duniani kote, ya kufuata katiba ya nchi na vyama.

Wakati katiba ya TANU/CCM ilipokuwa inaruhusu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alichaguliwa mfululizo kwa miaka 26 na ushee kuwa Mwenyekiti wa chama chake. Tena afadhali Profesa Lipumba alikuwa na mpinzani Profesa Safari. Nyerere kila uchaguzi, alikuwa ni yeye tu bila mpinzani. Mpaka alipoondoka, ndipo katiba ya TANU/CCM ilipobadilishwa kuwa kama ilivyo hivi sasa.

Profesa Lipumba na Maalim Seif wamechaguliwa kihalali katika uchaguzi rasmi ambao umekubalika na wanachama wa CUF. Sisi wengine tunapinga nini au tunaogopa nini?
Tuwaachie CUF wafanye wanavyotaka, kwa mujibu wa katiba yao. Uchaguzi wao inavyoonesha haukuwa na mizengwe kama ile ya TANU/CCM mjini Dodoma.
 
Profesa Abdallah Safari, baada ya kuanguka katika uchaguzi kugombea uenyekiti anawalaumu wajumbe wa CUF kwa kumdhalilisha.
Na Exuper Kachenje

SIKU mbili baada ya kuangushwa vibaya katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Abdallah Safari amesema wajumbe wa mkutano mkuu walimdhalilisha na kwamba anaandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo.

Profesa Safari alitoa malalamiko hayo jana alipozungumza na Mwananchi kuhusu matokeo ya uchaguzi huo uliomrudisha madarakani Profesa Ibrahim Lipumba, aliyepata kura 646, huku mpinzani huyo akiambulia kura sita tu.

Wakati Profesa Safari akijieleza, wajumbe walikuwa wakimzomea na baadaye kumrushia maswali yaliyomtingisha, ikiwa ni pamoja na kutaka ataje jina la katibu wa tawi lake, swali ambalo alibabaika kulijibu.

"Nimedhalilishwa; nimezomewa; nimeulizwa maswali ya kipuuzi. Ule ni uhuni hakuna kitu pale," alisema Profesa Safari.

"Wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wamepotosha na kuharibu maana ya demokrasia ndani ya CUF na kutumia vibaya nafasi hiyo ya kuchagua viongozi."

Alipobanwa kueleza iwapo anafikiria kuwania tena nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, Profesa Safari alisema hawezi na hana nia ya kuwania uongozi wa chama hicho.

"Sifikirii wala sina nia tena ya kuwania nafasi yoyote ndani ya CUF. Nitakapoita mkutano na waandishi wa habari, nitaeleza mengi. Mbali ya kuzindua kitabu changu, nitaamua shauri la kufanya pamoja na kesi ya uanachama wangu," alisema Profesa Safari.

Hata hivyo, wanasiasa wengine wanaona kuwa uchaguzi huo wa viongozi wa CUF umeonyesha kukomaa kisiasa.

Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema alisema CUF imeonyesha demokrasia na kumpongeza Prof. Lipumba kwa ushindi wake wa asilimia 97.

"Inaonyesha jinsi wana CUF walivyo na imani naye. Uchaguzi wa CUF umeonyesha ukomavu wa demokrasia ndani ya chama hicho, nawapongeza pia wana CUF kwa hatua hiyo," alisema Mrema.

Wakati huohuo, Said Salim anaripoti kuwa viongozi wapya wa CUF, wametoa salamu kali kwa CCM, wakisema kuanzia sasa suala la kuibiwa kura zao katika chaguzi mbalimbali nchini, limekwisha.

Wakizungumza mara baada ya kurejeshwa madarakani katika mkutano mkuu unaoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, viongozi hao walisema hawataruhusu tena wizi wa kura.

Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad alisema atahakikisha anatumia ridhaa aliyopewa kukipanga chama na kuhakikisha kuwa wanashinda kila uchaguzi watakaoshiriki.

“Mfano mzuri wa kukataa kwetu kuibiwa kura tutaonyesha katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi katika jimbo la Magogoni Zanzibar... ni jimbo letu lakini tuliibiwa lakini lazima tuligomboe,” alisema Hamad.

“Tunasikia kuwa tayari CCM wameshaandaa kura zao kwa ajili ya kujazia lakini nawapa salamu kuwa, watakavyoipiga ndivyo tutakavyoicheza. Hakuna tena msalia Mtume katika kulinda kura setu”.

Aidha aliwataka wanachama wake kushikamana kwa pamoja na kumaliza tofauti zao ndani ya vikao vya chama ili wakitoka wafanye kazi kwa ushirikiano na mshikamano.

“Tumalize tofauti zetu ndani ya vikao vyetu, tukitoka nje tukisema tuvute kamba basi tuvute kwa pamoja, tukisema tuache tunaacha sote. Nitakuwa nanyi; sitawaangusha hadi tulifikishe jahazi bandarini salama salimini,” aliahidi Hamad.

Naye makamu mwenyekiti mteule wa CUF, Machano Khamis mabaye alikuwa mshitakiwa nambari moja katika kesi ya uhaini iliyokabili viongozi 17 wa chama hicho mwaka 1997 hadi 2001 alisisitiza, kwa kuwa CCM ni wababe na wao lazima wafanye ubabe ili kukataa wizi wa kura.

“Wizi wa kura sasa basi; ikiwa wao ni wababe na sisi ni wababe vilevile; wakitunisha misuli na sisi tutatunisha. Hatutafanya vinginevo kwa kuwa tukifanya vingine, CCM wataendelea kujenga kiburi,” alisistiza Khamis na kuongeza:

“Tukatae CCM kuchukua kura zetu kwa nguvu kwa kuwa wao hawana haki ya kutawala.”

Alisema, ameshakaa jela mara nyingi, kwa hiyo hana tena woga na yuko tayari hata kupoteza maisha kwa kulinda maslahi ya umma.

“Haya ya kuwa siogopi, ndugu wajumbe, yanathibitishwa na kugombea tena nafasi hii. Kwa mateso niliyoyapata kwa kukaa jela, kama ningekuwa muoga ningekwishakaa nje ya chama hiki,” alisema Machano.

“Katika uchaguzi huu, tumewafundisha CCM namna demokrasia inavyotakiwa. Katika chaguzi zao kuna rushwa, kupigana, kuchafuana na makundi lakini kwetu kuna amani, utulivu na upendo baina ya wanachama na wagombea.”

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema amepewa jukumu zito na uzito wake unatokana na chama dola kung’ang’ania madaraka hata kama hakitakiwi nchini.

Alisema, licha ya ugumu huo, atahakikisha kuwa katika awamu hii wizi wa kura unakoma katika chaguzi nchini na wataanzia katika uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Magogoni na ule wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu.

“Ndugu wajumbe uchaguzi wa Magogoni ndio utakuwa kipimo cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010... kama tutakuwa na uchaguzi au mapambano; kama uchaguzi au uchafuzi,” alisema Prof. Lipumba.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la uwakilishi la Magogoni la kisiwani Zanzibar umepangwa kufanyika Mei 23 baada ya kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo hilo, Daud Hassan Daud.

Source:Mwananchi.
 
CUF ni ya MAALIM SEIF. Sasa huyu alitokea wapi tena? Amuulize Mzee Mapalala kilichomtokea baada kutofautiana na MAALIM.
 
Ndiyo yale yale nimedhalilishwa sana nimeonewa sana blah...blah.. kwa hiyo nimeamua kuachia ngazi. Kesho utasikia yuko CCM.
 
Back
Top Bottom