Uchaguzi 2015, Mgombea Chadema Anateuliwajei?

WaMzizima

Senior Member
Jun 25, 2009
152
41
Awali tuwaombee faraja kwa wahangwa wote wa ajali ya meli, Mwenyezi Mungu awape nguvu kwa kipindi hichi kigumu ndugu na jamaa wote waliofiwa na tunawaombea majeruhi wote wapone mapema.

Kwa sie ambao uelewa wetu wa siasa za CDM ni mdogo, ningependa kupewa darasa kuhusu mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kupitia CDM. Wengi wetu tunajua jinsi CCM inavyopata mgombea kwa kupitia mkutano wao mkuu.

Je CDM hutumia mfumo huo au kuna kura fulani za maoni maana sijui jinsi walimvyompata Dr Slaa kugombea safari iliyopita au Mbowe kabla yake.

Ningependekeza CDM wawe na kura za maoni ama kwa wanachama wao nchi nzima au kwa wananchi wote husika, tunaweza kupiga kura kwa simu na kupunguza gharama. Ni kweli Dr Slaa alitoa upinzani mkali sana kwenye uchaguzi uliopita, lakini bado alikuwa nyuma kwa kiasi kikubwa na hata wabunge wa CDM hawakushinda majimbo yanayozidi asilimia 10 (wabunge 23 kati ya 239 wa kuchaguliwa) majimbo yote Tanzania bara na 0 Znz.

Hivyo ni wazi kazi bado ni kubwa na najua kuna operesheni kubwa za kuhamasisha wananchi nchi nzima na hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wananchi. Lakini kama ukiangaliwa wabunge wengi wa CDM ni wa miji mikubwa (Dsm, mbeya, Arusha, Moshi, Iringa) kazi kuu iko vitongojini, vijijini na mikoa ya kusini pamoja na visiwani.

Zitto alitangaza nia yake ya kugombea watu wengi wakamlaumu nami nikaona kama ni kumuonea maana kila mtu ana haki ya kugombea nafasi ya uongozi kwenye nchi yetu, na nina uhakika CDM sio kama CUF kwa maana kuwa kila mara wagombea wao ni haohao tu kama vile chama hakina viongozi wengine makini. Je swala hapa ni nani atagombea toka CDM Slaa, Zitto, Lissu au Mbowe? naamini kutakuwa na mchuano mkali kama ilivyo kwa CCM...
 
Back
Top Bottom