Uchaguzi 2010: Zitto, Mbatia wajitosa Ubunge!

Hongera zake.Mimi nashauri agombee Kinondoni.Sababu nitazisema baadaye.
Kinondoni kuna msururu mrefu...Muro, Mbano, etc etc .....na sasa hivi aingie na mkuu huyu, basi kazi ipo. Azan naye pengine atakuwa amesoma na kumaliza usomi wake kisha kukidhi mahitaji ya kugombea ubunge mwaka huu pia. Who knows
 
Nadhani hiyo team ya survey itakuja na ushauri mzuri juu ya jimbo gani ugombee!
 
Du!huyu jamaa si ndiye aliyewahi kusema siasa halikuwa chaguo lake?!!!!!!!!!!!
 
Naunga mkono maamuzi yako kufanya utafiti kwanza. Lakini tatizo lako kubwa (Mh. Nyepesi) ni kuwa unapenda kusikilizwa zaidi kuliko kusikiliza. Na hii inakufanya ushindwe ku-coexist na peers wako. Kumbuka siasa sio hesabu kwamba moja na moja ni mbili, kwenye siasa inaweza kuwa kumi na moja. Learn political torelance and be visionary by aiming higher /future. Be strategic and avoid to be opportunist.

Haya ni mawazo yangu kwenye SWOT yako.
 
Zitto Kabwe, Mb.
Kigoma Kaskazini.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika Gazeti la Mwananchi na The Citizen ya leo Jumatatu, Tarehe 1/3/2010 kuna habari ya kwamba ninatafakari kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Nimeona ni vema nitoe taarifa rasmi juu ya jambo hili.

Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010. Majimbo ambayo nimeomba wayaangalie ni pamoja na Kigoma Kaskazini (ukiondoa kata ya Mwandiga ambayo imependekezwa kukatwa na kupelekwa Jimbo la Kigoma Mjini na hivyo kuondoa zaidi ya wapiga kura 15, 000 kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini la sasa), Kigoma Mjini, Kahama, Kinondoni na Geita.

Nimeelekeza kufanyike utafiti (survey) wa kina ili nitakapofikia kufanya maamuzi nifanye maamuzi kutokana na taarifa za kutosha. Tutatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya utafiti huo katika majimbo hayo na pia kwa ajili wa uchambuzi wa hali ya kisiasa na kutoa mapendekezo.

Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe 28/3/2010.
Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.

Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.


(imetiwa sahihi)
ZZK.
1/3/2010

Kulikoni Kigoma? Mh. natumaini ulifikisha malengo ya wapiga kula wako huko. Hii biashara ya 'window shopping' ya jimbo gani ugombee 'inafurahisha'
 
Nilikuwa sijui kama anapatikana hapa, namshauri atumie nafasi hii kufafanua ile katuni iliyoonesha akielekea CCM , jambo hili lilitafsiriwa na wengi kuwa anaamia huko.
 
Du!huyu jamaa si ndiye aliyewahi kusema siasa halikuwa chaguo lake?!!!!!!!!!!!

Nakumbuka alisema kwamba anafanya PhD ili awe mhadhiri wa Chuo Kikuu na kuachana na siasa kwa sasa! Sasa haya ya kutapa tapa ni jimbo lipi agombee ni kutokana na kwamba jimboni kwake inasekana hajafanya lolote la maana kwa miaka yote mitano aliyokuwa mbunge wao.

Wananchi wa jimbo lake wanalalamika kwamba amewasahau na kujikita kwenye siasa zaidi hasa viata dhidi ya ufisadi! Tusubiri tuone! Ila Dar pagumu, maana ndipo panaongoza kwa wapiga kura vigeugeu!
 
Nilikuwa sijui kama anapatikana hapa, namshauri atumie nafasi hii kufafanua ile katuni iliyoonesha akielekea CCM , jambo hili lilitafsiriwa na wengi kuwa anaamia huko.

Kwa hiyo gazeti la Uwazi likitoa katuni unaiamini. Watanzania bwana
 
...pamoja na kuwa dhamira ya kugombea ubunge ni ya kibinafsi zaidi lakini kwa mapana ni msukumo aliokuwa nao mgombea juu ya changamoto za kuleta maendeleo mahali fulani. Na msukumo huu hauji ghafla kama mwivi avamiapo mahali fulani (ingawa yeye mwizi hupanga).

Sasa hili suala la kufanya feasibility study kujua ni jimbo gani atagombea, na pia kuweka wazi kwa wananchi kabla ya kuchagua jimbo la kugombea, nadhani si njia nyofu kwa mbunge huyu mtarajiwa na nitatoa sababu:
i) Mwananchi wa jimbo lolote kati ya hayo ambapo Zitto ataamua kugombea (ukitoa Kigoma Kaskazini) wataona Zitto anawatumia kama mgongo wa kisiasa, na si mtetezi wa dhati wa changamoto zao
ii) Sijawahi kusikia mahali popote kwa mbunge kufanya feasibility study publicly. Huwa wanafanya kimyakimya na wanapojitokeza huonekana kweli wamedhamiria kupigania maendeleo ya jimbo husika. Na hata kama imewahi kufanyika mahali fulani, mgombea lazima atakuwa kwenye lose-lose situation.
iii) Pia inaweza kuleta mgongano wa kimaslahi katika chama chake, kwa kuwa nina imani, kuna watu tayari wamesha earmark hayo maeneo mengine (ukiachia Kigoma Kaskazini).

Ukiachilia sababu hizo, ninakubaliana naye kimsingi kabisa kuwa kama mtanzania, ana haki ya kujitosa kugombea nafasi ya ubunge mahali popote. na kwakuwa dhamira yake pana ni ya kitaifa zaidi, yaani ukiwa mbunge huongelei, hupitishi miswada ya jimbo lako pekee. Unakuwa pale kwa manufaa ya taifa zima.

Labda nimtakie kila la heri kwa zoezi hilo, lakini pia asisahau angalizo lile pale juu.
 
Hapa Zitto anapima jinsi gani anavyokubalika katika jamii ya Watanzania. Ningependa kusikia kama kuna mbunge mwingine anaweza kuwa na option nyingi kama alivyo Zitto. Nafikiri mwingine anayeweza kufanya hivi kwa sasa ni Dr. W. Slaa.

Naona anapima joto kuelekea kugombea kuwa kiongozi wa majimbo yote ifikapo mwaka 2015/2020.
 
Suala lisiwe tu kugombea. Fikiria kwanza ni nini unatarajia kwenda kuwafanyia wanajimbo wako? halafu angalia ni jimbo gani wanahitaji huo msaada wako ndio wataweza kukusikiliza na kuona umuhimu wa sera utakazoombea kura. Kuna haja ya kuonyesha tofauti yenu na mfumo uliopo wa ccm.
 
Yaaaaa gombea kinondoni kuleta mapinduzi maana watu wa Dar bado hawajapata mbunge wa kweli
 
Kwa hiyo gazeti la Uwazi likitoa katuni unaiamini. Watanzania bwana
Kwa sababu ilianzisha mjadala mkubwa sana hapa JF kuwa anarudi ccm na amefirisika kisiasa, mpaka mimi nikawaeleza kuwa ni vyema tumsikilize yeye anasemaje,
 
Gombea Dar Mkuu, kule chalenji zako zitapimika vizuri...Kigoma is peanut for a person of your calibre!
UWEZO wa kupata UNAO!
 
huyu kijana kwisha habari yake................. ni miujiza tu ndiyo inayoweza kumrudisha bungeni...................

mipango yake imevuja ndo maana magazeti yaliandika mpango huu kabla hajausema............. mara anamsapoti kafulila kgm kaskzn na kumpa magari (aliyoyapata kifisadi) kumsaidia kampeni............. halafu leo anasema kati ya majombo anayoyafikiria ni pamoja na kigm kaskzn!!!!!!!!!!!!!!!!!......... anataka akagombane na kafulia (nccr) na yryr (chdm)................. mmh, hapa kuna habari ya kitoto sana............... huyo kishakataliwa huko kgm kaskzn na nec imemaliza kwa kuitoa mwandiga na kuipeleka kgm mjin................. kwisha kabisa huyu dogo...........

ccm walimlia taiming zammani, wakamwonjesha ladha ya pesa za bila jasho....... akawehuka........... akanyea kambi yake iliyomtoa mavumbini (chdm)................. sasa mara anaunda timu (posho anazowapa si za kifisadi??????????, zinakidhi matakwa ya muswada mpya wa fedha za uchaguzi???????????)........... huyu ndiye mBunge wa kwanza kutangaza kwenye vyombo vya habari kutoa takrima uchaguzi huu................ HII NAYO NI REKODI YA AINA YAKE.............

upuuuzi upuuzi upuuuzi............. akishindwa uchaguzi wansheria watamlia dili watamkonvince akate rufaa wale hela zilizosalia halafu akimwagwa kotini.............. ATAENDA KUOMBA KAZI KWA MAKAMBA..................... HUYU SI MWANASIASA................ ANA MAMBO YA KITOTO SANA.................NASHANGAA ETI ANASHABIKIWA NA WATANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!..................... AAH, INAUDHI SANA.............

asubiri miujiza....................... kwani bongo nako miujiza haiishi...........
 
Darisalama hakuna wapiga kura wa kuchagua upinzani. Wapiga kura wote mabishoo na masister duu wa kupnga foleni. kaiz yetu ni kuchambua matokeo ya wizi wa CCM na kukaa kuangalia matokea kwenye Luninga.


Namshauri zito akagombee Geita au Kahama sisi wa mujini wote ni ma analyst wa mambo
 
Back
Top Bottom