William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,374
- Thread starter
- #81
William kabla hatujaanza kujadili tathmini za uchaguzi zilizotolewa na NEC wewe binafsi bila kujali itikadi yako kichama unatoa tathmini gani? Suala la uchaguzi huu ni dosari za makusudi ili kukipa nguvu chama tawala; kimsingi NEC si chombo huru hii ikumbukwe kilikuwa ni kilio tangu wakati wa mfumo vyama vingi ulipoanza; wapinzani wa kweli wakati ule waliliona lakini wengi waliingia kwenye mtego wa ruzuku ambao unaendelea hadi leo hii; kama wapinzani kweli wanataka kuleta mabadiliko wajitoe kwenye hii mifumo ya ruzuku serikali haipashwi kulea vyama kwa ruzuku jukumu la kulea vyama ni la wanachama wenyewe, dosari ni dosari tu iwe ndogo ama kubwa uchaguzi unatakiwa uwe huru na waki.
- Tathmini yangu ni kwamba wananchi wana imani na Rais waliyemchagua, lakini wana tatizo sana na viongozi wake wa chini hasa mawaziri, ma-RCs, na ma-DCs, HOWEVER mimi kama mwanachama huru wa CCM nimetatizwa na mapungufu mengi sana yaliyojitokeza kiuongozi ndani ya chama changu, na pia nimesikitishwa sana na ushauri mbovu ambao Rais, Dr. Kikwete alikuwa akipewa na wasaidizi wake kuhusu muenendo wa kampeni hizi, ninasema hivi viongozi wote wa CCM taifa wajiuzulu sasa maana wameharibu sana na hawafai kabisaa! Hwafai kwa chama chetu CCM na hawafai katika kuweka muenendo wa CCM katika kutawala taifa, they are simply incompetent! Hawawezi na huu sio wakati wa kuoneana haya katika kuambiana ukweli!
- Ni mshauri gani aliyemshauri Rais kwenda kwenye majimbo ya viongozi wa CCM ambao politically wana tuhuma nzito sana za corruption against society, I mean huyo kiongozi afukuzwe kazi mara moja hafai huku USA tumeona Obama, akikwepa kwenda jimbo la Harlem ambako kuna kiongozi wa chama chake mwenye tuhuma nzito za corruption, tumeona viongozi wengi tu wa chama cha Obama wakigoma kuonekana naye kwenye majimbo yao wakiogopa hasira za wananchi kwa sababu policies za Obama, hazikubaliki katika majimbo yao hivi kulikuwa na tatizo gani kwa Rais kutokwenda hayo majimbo au kwa Rais kwenda kwenye hayo majimbo, lakini hao viongozi wenye tuhuma wasiwepo kwenye mikutano yake Rais?
- Tunasikia vitendo vya kuhuni katika hizi kampeni ambapo mbunge mmoja wa CCM alikuwa akigombea jimbo lake na pia kumsaidia mpinzani wa jimbo la mgombea mwenzake wa CCM, na yule mwenziwe naye anagombea kwake na huku anamsaidia mpinzani wa mwenziwe matokeo wote wawili wakashindwa na kuyaacha majimbo ya CCM yakichukuliwa na Wapinzani, I mean nani alikuwa msimamizi wa huu mkoa wa Mwanza ambako ndio tumesikia haya yametendeka, msimamizi wa taifa wa CCM huko anatakiwa kufukuzwa kazi mara moja, nasema sasa na hao wagombea wafukuzwe chama chetu mara moja maana hawatufai CCM wala taifa, I mean I can go on and on, lakini nitahakikisha kwamba ujumbe wangu unawafikia CCM taifa na hasa Mwenyekiti kwamba wakati ni huu wa kujiangalia usoni bila kuoneana aibu!, au tusubiri aibu zaidi ya mwaka 2015!
William.