Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,012
- 95,358
Ndugu zangu watanzania wenzangu (kama kweli mi ni mtanzania kwa mujibu wa CCM)
Uchaguzi wa mwaka huu umegubikwa na wimbi la watu waliokuwa wanajijua kuwa ni watanzania kumbe kwa mshangao wao wanajikuta kuwa si watanzania.
Kuna mmoja aliyekuwa anataka kugombea ubunge kupitia CHADEMA huko Mwanza aliwekewa pingamizi na Waziri Lawrence Masha na pingamizi hilo kukubaliwa. Amenifanya nipate uchungu na kuanzisha sredi hii ili wajuvi mnisaidie
Binadamu huyu amezaliwa Tanzania Miaka 33 iliyopita. Hajawahi kuishi nje ya Tanzania. Baba yake ni mtanzania aliyezaliwa Tanzania. Baba wa baba yake (babu) ni mtanzania aliyezaliwa Tanzania. Ila mama yake ni mzaliwa wa Kenya aliyekulia Tanzania.
Kinachonigongeshaa kichwa:
Baba anapokuwa raia wa Tanzania na mama si raia, na mtoto kazaliwa na kukulia Tanzania mtoto anakuwa raia wa wapi?
Kama mtoto anakuwa si raia wa Tanzania, anapaswa afanye nini ili awe Raia wa Tanzania?
Mwenye mamlaka ya kumtangaza mtu kuwa ni raia wa Tanzania ni nani?
Je uraia wa mtu unagundulika tu pale anapogombea nafasi za uongozi wa kiasiasa?
Naomba msaada wenu, nina mpango wa kuikomboa nchi hii mwaka 2015 sasa nahofia nisije kukomboa nchi isiyo kuwa ya kwangu.