Uchaguzi 2010: Masilahi Ya Taifa Kwanza!

- Mkulu Pasco, vipi ukiiweka wazi hapa hiyo record ya huyu waziri na vita dhidi ya ufisadi? Wengine hatuifahamu!

Respect.


Field Marshall Es!

Kamanda Mkulu FMES,

Nafikiri unafahamu fika ni kwa nini huyu bwana alitolewa pale Ujenzi, Haya mambo ya chama kuingilia utendaji wa baadhi ya viongozi kwa maoni yangu ni kitu kibaya sana........simply because others they were able to make a KING...............

kwa kifupi JPM njia yake ilikuwa nyeupe kwa sababu baraka zote zilikuwepo.........nafikiri unaelewa vizuri ni kwa jinsi gani MTANDAO walivyomfanyizia huyu jamaa.........anyway ndio mambo ya siasa ndani ya Chama.........

ana bahati mbaya moja vita vyake na mafisadi havikuwa smart kwa sababu alikosa guidance na hasa kwenye sheria..........

Mkuu FMES........unakumbuka
vita vya Bohari kuu.......na
ununuzi wa magari ya serikali......(NOTE: si matumizi)
huko kwenye miradi ya barabara ndio usiseme.....mafisadi walikoma ubishi.....


in short....jamaa anafaa sana kuwa kiongozi wa hii nchi....anahitaji timu nzuri ya wanasheria....jambo ambalo si gumu kulipata.......
 
Pasco,
Nafikiri bado "Prof. Lipumba is the best candidate kwa wakati huu, mtazamo wangu ni kwamba tuna tatizo la umaskini, umakini katika kuendesha mambo (commitments and seriouness) na mtu ambaye si "mchumia tumbo" yaani mlafi au fisadi...

Prof. katika kuongoza CUF nikiwa nimfuatiliajia wa siasa za upinzani ameepukana na kuhusishwa na rushwa na ufisadi katika ruzuku unlike mbowe, mrema and other folks

Kila mara ameweza kutoa hoja mbadala kwa maslahi ya Taifa na mara zote nimeona jamaa hana nonsense yuko committed na ana feel amejaribu kuwa mkweli wakati wote

Ni msomi anayeshimika katika anga za kimataifa..kwahiyo tutaondoka na aibu ya taifa kuwakilishwa kwa kiwango cha chini katika world political forums..ukimuangalia JK wakati ule wa mkutano IMF dar utaomba asiwe rais wako..he literally incompetent...that is fact..
Kwa bongo Prof. Lipumba is Obama like..
Mimi nafikiri Upinzani is high time wamuunge mkono Lipumba for presidency, wakati huo huo kulinda kura maana 2010 uwizi utakaofanyika mtashangaa kwasababu mzee wa kaya umaarufu umepungua..atakuwa rais wa NEC!
Yes Lipumba is fine, ila baada ya kujaribu mara 3 kapa, hana tena mashiko. Hana dynamisim na charisma ya kuchagulika, its a gone case unless tunamtafutia JK msindikizaji sio mpinzani.
 
Yes Lipumba is fine, ila baada ya kujaribu mara 3 kapa, hana tena mashiko. Hana dynamisim na charisma ya kuchagulika, its a gone case unless tunamtafutia JK msindikizaji sio mpinzani.
Nasubiri list ya wengine wenye charisma na kuchagulika...lakini nafikiri uchaguzi ni pamoja na campaign strategy ..still "I think Lipumba" is product which can be sold and bought...by wananchi...kwa standard zote anatufaa ni swala la kutafuta "Wauzaji wenye uwezo wa kuuza bidhaa" hapo ndipo mimi nafikiri wapinzani wanatakiwa walenge..
 
Wakuu Ogah na Pasco,

Sina matatizo na utendaji kazi wa John Pombe Magufuli kwa kipindi chote alichokuwa Waziri zama za BWM. Ni kweli kuna madudu alifanya kama ulivyotaja, swala la uuzaji nyumba za serikali.

Nina tatizo kubwa moja, unajua madudu mengi ya ufisadi yanayoibuka sasa yalifanyika zama Mkapa. Magufuli alikuwa ni pendekezo la Mkapa kwenye nafasi ya Waziri Mkuu mara baada ya uchaguzi wa 2005. JK aliweka mguu chini akalikataa hilo pendekezo la Mkapa na kuamua kumpa swahiba wake (EL).

Mtu yeyote ambaye ni chaguo la Mkapa ama ambaye anasema Mkapa ni mtu safi, mimi nimwogopa sana. Kama utakumbuka vyema, siku Pinda anachukua kiti cha u-PM, alimfagilia sana Mkapa kwamba alifanya kazi chini ya BWM pale Ikulu na akaendelea na kumfagilia EL. Few months down the road, Pinda huyo huyo akaja kumtetea Mkapa kwa makosa ambayo yako wazi, swala la Kiwira.

Ukisema tumchague mtu kama Magufuli, huu uchafu tulio nao (ufisadi) wote utafukiwa kwa kuwa ukizama ndani zaidi kwenye hizo kashfa utakuta kuna mikono wa Mkapa. CC na NEC tayari wameishasema kwamba Mkapa asiguswe, pamoja na huu uchafu wote uliopo ambao unamgusa yeye moja kwa moja.

Kiwira tayari imeishafunikwa, Radar imefukiwa, Ndege ya Rais ndo hiyo imetulia Terminal II, na hata hizi kesi za EPA ambazo hazijaenda mahakamani lazima kuna mikono ya CCM, Mkapa ama RA, ndiyo maana tunawaona watuhumiwa wanatesa mtaani. Ukiuliza utaambiwa kwamba hakuna ushahidi wa kutosha ama wamerudisha pesa zote. Je, waliopelekwa hawajarudisha? Ama waliopelekwa ushahidi wao ulipatikana wapi? Makosa ni yale yale, lakini hatuwa wanazochukuliwa watuhumiwa ziko tofauti.

Kwa maoni yangu, mtu yeyote ambaye alishawahi kuwa close na Mkapa ama ambaye anaona CCM ya sasa ni safi, huyo hatufai hata kidogo. Ninasema hatufai kwa kuwa ni CC na NEC ya CCM ndo wamekuwa kiwingu kikubwa sana kwenye agenda ya ufisadi. CC na NEC ndo wanaendesha kampeni za kuwasafisha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi. SO, ukimchagua yeyote ambaye anaona CCM na Mkapa ni safi, hatuwezi kufika mahali, tutakuwa tunapiga mark-time, na kujikuta hatufiki popote. Sana sana atasaidia kufukia ushahidi wote uliopo ili Mkapa na baadhi ya viongozi wa CCM waonekane wako safi, na kumbe si kweli bali ndiyo wanaoongoza kwa ufisadi na kulindana wao wenyewe.

Kwa kuwa Magufuli ni mtu wa Mkapa, akiwekwa kwenye nafasi ya kumshughulikia Mkapa na madudu yake, hatuwezi kufika popote. Magufuli hana tofauti na akina JK, EL, Pinda na wengineo. Kinachomtofautisha ni kwamba yeye mwenyewe (Magufuli) ana madudu machache sana, sawa na jinsi alivyokuwa Pinda pia ni mchapa kazi mzuri sana, huwa hana siasa kwenye kazi. Lakini hayo madudu machache siyo warrant/guarantee kwamba akiwekwa kwenye nafasi hiyo atafuatilia mpaka mwisho ufisadi wote uliofanyika huko nyuma. Tunataka kiongozi atakayefuatilia hayo madudu ya nyuma ili kuweka msingi kwamba mtu akichaguliwa kuwa kiongozi ama akipewa uongozi basi asijihusishe na ufisadi. Akija kiongozi wa kufunika uchafu, tutakuwa hatufanyi kitu.

Kupata kiongozi safi ndani ya CCM ni kazi ngumu sana kwa kuwa mfumo wa kupata viongozi umetawaliwa na rushwa, ni mafisadi ndio wanaamua nani awe kiongozi kwa maslahi yao. Baadhi ya prominent figures ndani ya CCM ambazo tunaona kwamba zinafaa kupewa uongozi, hawakubaliki na "wenye chama" (mafisadi). Siku ikitokea hao tunaosema ni wasafi ndani ya CCM wakishika uongozi, basi ndiyo tutakuwa tumeizika CCM rasmi.

Magufuli atafaa iff atapewa condition kwamba agenda ya ufisadi inaanzia siku atakaposhika madaraka, lakini hawezi kurudi nyuma 15 yrs, maana atakuta mikono ya Mkapa na hawezi kumgusa.
 
Wakuu Ogah na Pasco,

Sina matatizo na utendaji kazi wa John Pombe Magufuli kwa kipindi chote alichokuwa Waziri zama za BWM. Ni kweli kuna madudu alifanya kama ulivyotaja, swala la uuzaji nyumba za serikali.

Magufuli atafaa if atapewa condition kwamba agenda ya ufisadi inaanzia siku atakaposhika madaraka, lakini hawezi kurudi nyuma 15 yrs, maana atakuta mikono ya Mkapa na hawezi kumgusa.


Keil, maadam tuko safarini kuelekea 2010, nashauri tusonge mbele, lets concetrate na tuendako kwa kupanga malengo tunataka kufika wapi. Tukizidi kuangalia nyuma sana, nani alifanya nini wapi, tutaishia kupiga mark time.

Hata JK angeanaliwa kwa track record yake Nishati na Madini, yeye akiwa Waziri katibu Mkuu wake Mwandosya, jamaa walifanya mambo ya ajabu sana Mwandosya as a man of integrity, akarejea UDSM. Hayo yote yalipita na wote walikuwa wagombea.

Sasa tunamtafuta wa 2010, waacheni wafu wawazike wafu wao, sisi tusonge mbele kuutafuta mwanga wa huko tuendako, au kwa vile tumeshalizoea giza, basi bora tuendelee kuenenda kwenye giza?.

I can see light in Dr. Slaa.
 
Shalom, facts are sturbon things, its a fact ndiye rais wako kwa sasa, uwe ulimchagua au hukumchagua, akishaapishwa ni rais wa wote, hii ni fact, haina mjadala,

Kwa upinzani legelege tulionao kwa sasa, tutake tusitake, 2010 ni JK tena, its sad but its a fact, ndio maana napendekeza tumtafutie mshindani wa kikweli kweli ili kumsafishia njia ya 2015 na sio msindikizaji. Wote alioshindana nao 2005 walikuwa wasindikizaji ndio maana jamaa akaibuka na ushindi wa kishindo.

Akisimama na jabali kweli kweli, ndio bado atashinda lakini sio kwa tsunami, hicho kitakuwa kiashiria 2015 mabadiliko yanawezekana, vinginevyo i watu wale wale kwa mbinu zile zile na tutaendelea kuwapa ridhaa yetu watutawale milele.

Khakha, topic ina sema tujadili masilahi ya taifa, wewe unasema kuwa tusimjadili Jk kwani tayari ni Rais 2010. sasa mimi nimekuuliza je hili nalo ni masilahi ya taifa unaanza kutoa maelezo mengi?

Nakuuliza tena hilo la kutomjadili JK ni masilahi kwa taifa? kama ikionekana kuwa kipaumbele cha taifa ni Ufisadi na record ya JK ni zero, bado wewe utadai ni masilahi ya taifa kutomjadili.

Mimi nachojua ni kwamba unapoajadili kitu kwa masilahi ya taifa kwanza unaangalia masilahi ya taifa (issues) halafu baadaye unayapa rasilimali watu wa kuyaendesha( watendaji).

Wewe umeanza kuangalia kwanza watu na desturi zao halafu ndiyo unarudi kwenye issue halfu unadai hii ndiyo masilahi ya taifa.

Halafu jamani tuache haka ka laana ka kusema fulani ni raisi tu 2010 wakati kuna utaratibu, na elewa pia unavyosema hivyo madodoki ni mengi yanabeba hicho hicho kinachosemwa Kwa lugha fupi ni kwamba kauli huwa zinaumba.
 
Kumtaka Dr. Slaa arudi Karatu sii dawa inayoponya maradhi tulokuwa nayo na nadiriki kusema kwamba pamoja na jitihada zake bungeni Mheshimiwa Dr Slaa amebakia kama uwanja huu wa JF ambapo tunaandika mengi sana lakini tunazaa matunda hafifu yasiyo na tija kwa taifa kwani maamuzi mengi yameshikiliwa na Mafisadi wenyewe.

Mkandara,

Hili na mimi limenistua sana ila sikutaka kusema jana kwani si unajua tena ukimwona nyoka anatoka shimoni lazima uone kichwa ndiyo ukate nami nakaona ni kheri nikisubiri lakini umeniwahi.

Dr Slaa agombee karatu eti ni masilahi ya taifa du!
 
Kwanza kwa heshima na tahadhima muombeni Mweshimiwa Rais JK asigombee halafu mimi nimeangalia msimamo alionao Mweshimiwa Six, kwa kweli anafaa sana katika vita hii.
 
- Wakuu uchaguzi mkuu wa taifa uko kwenye kona, Mzee Mandela aliwahi kusema kwamba kwenye ishu muhimu za taifa kama hizi kuwa kimyaa au kuwa neutral ni dalili za kuwa coward.

- Kwa wale tulio na influence ya namna moja au nyingine kwa taifa, ni vyema tukaweka wazi msimamo wetu kwa public kuhusu wagombea ambao tunaamini kwamba wanafaa katika kutusaidia taifa, nimekuwepo JF kwa muda mrefu sana sasa nikiwa na lengo moja tu, nalo ni siku moja kuliona taifa langu likiongozwa kwa kuheshimu sheria.

- Kwa hiyo leo nitaanza rasmi kuwataja wagombea ninaona wanafa kwa masilahi ya taifa letu, na sababu.

Respect.

FMEs!

Dk Slaa kwa Urais 2010. CHADEMA msipuuze
 
2010 Rais yupo. Ni JK tena. Labda atumie busara ya kawaida tu kupima aone kama afya yake itamruhusu kuendelea. Vinginevyo mjadala huu hauna tija kwa sasa na mazingira tuliomo. KATIBA yetu, TUME yetu ya Uchaguzi, vyombo vyetu vya dola na WANANCHI wetu VIJIJINI na MIJINI.
Hamwoni ziara za VIONGOZI wetu WAKUU wa NCHI mikoani zimeongezeka sana? Hamsikii wala kuona wanayoyasema; hamwoni wanavyopokelewa? JK ameshaanza kampeni za kurudi kwa kishindo madarakani 2010. Sioni atazuilika vipi.
 
Wapinzani wakiungana na kuchagua Mgombea Mmoja itasaidia sana kuleta Mabadiliko ya kweli na atakayeshinda kweli atakuwa na ridhaa ya Kuliongoza Taifa letu na hawezi kuleta MIZENGWE wala USANII bila kujali jina lake wala Chama.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Prof. Ibrahimu Lipumba for 2010 presidency...wapinazni wote wamuunge mkono tafadhali..right person in a right time.

Tumaini, yuo have to remember that you can not teach an old dog new tricks. unategemeya Prof. ana nini kipya cha ku2pa cc. for the last 15 yrs cjaona ki2 kipya kwake zaidi ya ngonjera za kila cku. Je 2nahitaji kiongozi bila uongozi au ungongozi bila kiongozi bora
 
Dk Slaa kwa Urais 2010. CHADEMA msipuuze


- Wakuu heshima mbele, kabla hatujaendelea na majimbo mengine kuna hoja moja inaonekana kukubalika na wengi nayo ni DR. Slaa for President, I like it lakini nina wasi wasi kwamba wengi hatumjui vizuri sana na hasa record yake ingawa ya vita na ufisadi iko wazi, mnaoijua vizuri record yake iwekeni hapa maana Urais wa Dr. Slaa unajadilika,

- Halafu vipi wakuu kweli Dr. Slaaa anaweza kuwa Rais bila muungano wa wapinzani halafu wakamsimika kuwa mgombea wao?

Respect and Later!


FMEs!
 
Kama ni kwa ajili ya kutunisha RUZUKU ya CHADEMA kwa kura za URAIS, Dr Slaa anafaa sana. Yatakuwa pia ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya 2015 ambapo CCM watakuwa wamenyukana kiasi cha kutosha
 
Back
Top Bottom