Elections 2010 Uchaguzi 2010: CAMPAIGN AU COME PAIN?

Mpelijr

Member
May 17, 2010
89
11
Nimekuwa nikifikiria jinsi mambo yanavyobadilika tukifika kwenye mwaka wa uchaguzi na hasa nikafikiria je ni kweli kwamba asilimia kubwa ya watanzania wanafaidika na kampeni au ndo wanaandaliwa kwa ajili ya maumivu ya baadae?
Viongozi wamekuwa wakiwanyenyekea mno wananchi hichi kipindi kwa ajili ya kujitengenezea ulaji miaka mitano hii inakuwaje kwa wananchi?wanaandaliwa nini kama baada ya uchaguzi hawasikilizwi kwa maoni wala shida wakati ni jukumu la huyo mtu waliyemchagua?
Tanzania tuna kazi ku overcome selfishness katika serikali....
 
tubadilike tuchukueni hatua ambazo zitatuletea mafanikio hapo baadaye.
TUACHENI WOGA KUONDOA FIKRA MGANDO KWENYE UHALISIA WA WAKATI NA MAHITAJI YETU.
 
Watanzania tukibadilika na kuwa tayari kuweka maslahi ya taifa letu kwanza na kuweza kuchagua viongozi wetu kwa kuzingatia sera zao na siyo ahadi wala utashi wao walionao na watu....viongozi waadilifu wataofanya kazi kwa kuzingatia kuwa wananchi ni mabosi wao na siyo watumwa wa ahadi zao za uchaguzi.....
 
Back
Top Bottom