Uchaguzi 2010 Ahadi za wagombea urais

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Ahadi mbalimbali za wagombea urais 2010

Saturday, 09 October 2010 21:34
Jakaya Kikwete

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera 9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo – Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
33.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
34. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
35. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
36. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
37. Kulinda haki za walemavu- Makete
38.Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
39.Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
40.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

41.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
42. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
43.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
44.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
46.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
47.Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
48.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
49.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
50.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
51.Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
52.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini
53.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
54.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa

55. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
56. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
57.kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
58.kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
59.ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
60.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
61. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti


Maalimu Seif Sharif Hamad

1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
2.Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar- Pemba

4.Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
5. Kuwaunganisha wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba
6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja
9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
10.Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba
11.Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na pemba
12.Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda maiti
13.Kukomesha rushwa-Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
14.Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la ole Pemba 15.Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni Pemba
16.Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh180,000-Chakechake Pemba 17.Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
18.Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
19.Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
20.Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
21.Kila mzanzibar kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
22.Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda maiti
23.Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka kwa Zanzibar -Unguja
24.Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu - Viwanja vya Kibanda miti
26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
27.Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda maiti
28.Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba
29.Kujenga bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani pemba.

Profesa Ibrahim Lipumba

1.Kubadili katiba na kumteua Dk, Mohamed Shein kuwa makamu wa Rais –Unguja
2.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu -Tanga
3.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri-Tanga
4.Kuunda serikali shirikishi-Mtwara 5.Kusimamia rasilimali –Tanga
6.Kuimarisha miundombinu-Kidongo chekundu
7. Kusimamia na kuboresha afya-Kidongo Chekundu,Dar
8. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji-Mtwara
9.Kudhibiti uuzaji wa zao la korosho-Mtwara
10 Mfuko maalumu wa kusomesha walemavu-Tanga

Dk Willibrod Slaa

1.Kurudisha pesa za mradi wa Rada-Moshi
2. Kushughulikia suala la taasisi ya kuweka na kuvuna pesa(DECI)-Uwanja wa mashujaa Moshi
3. Kujenga nchi isiyo na ufisadi-Mwanza
4.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar-Ifakara
5.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo –Arusha
6.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais-Mwanza
7.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15-Arusha
8. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho-Kilimanjaro
9. Kutoa huduma bora za afya bure-Mwanza
10. Kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi-Tarime
11.Kufuta walimu wote wa cheti na stashahada shule za sekondari na kuleta walimu walio na shahada –Arusha
12. Kutoa elimu bure kuanzia shule ya awali hadi kidato cha sita -Morogoro
13.Kutoa huduma za afya bure kuanzia kituo cha afya hadi hospitali ya rufaa-Mwanza
14.Kutoa ruzuku taasisi za kidini-Ifakara
16.Kusambaza magari aina ya shangingi kwa jeshi la polisi ili wakamatie wahalifu,badala ya mawaziri kuyatumia-Ifakara

Dk Mohammed Shein

1) Kuboresha maisha ya wavuvi-Chakechake Pemba
2) Kusomesha wafanyakazi-Mnazi mmoja
3) Kipaumbele katika elimu -Unguja na Pemba
4) Kipaumbele katika afya-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.

5) Kuulinda Muungano- Wawi kisiwani Pemba
6)Kuleta mabadiliko Zanzibar-Pemba na Unguja
7)Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya-Kibandamaiti

8)Kuboresha Maendeleo Zanzibar- Jimbo la Wete, Pemba
9.Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba- Mtambwe
10.Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar- Kijiji cha Kambini Mchangamdogo
11.Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba- Kijiji cha Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba
12.Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Pemba katika miradi mbalimbali-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
13.Ahadi eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi- Micheweni Kaskakzini Pemba

14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani -Mkoani
15.Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja- Mkoani
16.Kuiamrisha makazi bora kwa wazanzibar- Mkoani

Imeandaliwa na Hussein Issa
 
Ilikuwa ndoto tu, kulikucha tukaendelea na shida zetu.
Ndoto nzuri ya namna hii itajirudia tena, tukilala mwakani.
 
JK alikuwa anadhani anapiga bedtime stories kwa watoto unaweza waambie chochote ili mradi kiwe na mwendelezo hata km hakina ukweli.
 
mkuu hii thread umeua. maana 95% ya ahadi za kikwete ulizooredhesha hapa ametekeleza.
bila shaka saccos iitwayo kadima wataumia sana.
 
mmh!
ndipo kauli ya ubongo wa mtu mweusi ni dhaifu huthibitika.
"Zanzibar Kuwa Hong Kong ya Africa"
na wazenj wakamwelewa
 
Mwakani lazima wagombea Urais wapimwe akili, vinginevyo utasikia wanaahidi kuleta meli ziwa Singidani!
 
Back
Top Bottom