Uchafuzi wa mazingira kwenye barabara kuu ziendazo mikoani must stop

Chesty

JF-Expert Member
Aug 30, 2009
5,777
2,720
Wakuu kuna mambo ambayo yanafanyika kwenye njia kuu ziendazo mikoani ambayo hayatakiwi kufumbiwa macho.

Abiria wa mabasi wanapoingia kwenye vituo vya kula chakula wengi wao wanachukua vyakula kama take away, kinachofuata ni kula ndani ya basi na kisha mabaki ya mifuko ya plastiki, chupa za plastiki za maji ya kunywa zinatupwa tu nje barabarani.

Ukifuatana na mabasi haya utaona jinsi abiria walivyokosa ustaarabu kwa kufanya vitendo hivyo vya aibu.

Kwa wale wanaosafiri barabara ya kwenda Mbeya kutokea Dar mtakubaliana na mie kuwa maeneo baada ya Mikumi kuelekea Aljazeera yamechafuliwa sana. Ni ushauri wangu kwa serikali kutighten sheria na ikiwezekana kutoa faini kali sana ili uchafuzi huu wa masingira ukome.

Nashauri yafuatayo:
1. Mabasi yaweke dust bins
2. Kuwe na matangazo kila basi linapotaka kusafiri na hata wakati wa safari kuwa si ruhusa kutupa uchafu nje.
3. Kuyafungia mabasi ambayo abiria wake wanatupa taka hovyo.

Tunaweza kufanya mengi ili kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa masafi.

Nawasilisha.
 
Kweli umenena! Hiyo tabia inaendelea hata kwa usafiri wa meli na maboti. Wasafiri wanaona raha kutuma vyupa vya plastiki wavione vinavyo elea na kusukumwa mbali na waves za meli/boti. Hata gari zenyekupitia mbugani (Ngara/kahama), unakuta watu wanachafua tu.
Niliona rwanda wamefika mbali kweli: wametenga sehem mbalimbali mbugani kwa watu kujisaidia. Sio kama TZ habiria akisema tu gari linasimama woooote wanashuka kujisaidia barabarani (hata haja kubwa). upuuzi huu unawafanya wanyama wakimbie eneo za kando ya barabara (as "human marked territorry" kwa lugha ya fauna).
Safari ndefu huana na hatua ya kwanza na nadhani Chesty katuelekeza direction ya msafara mkubwa unao tusubiri sisi pamoja na serikali.
 
Huwa napata shida sana kuelewa vyombo vyetu vya kusimamia masuala kama haya vipo wapi, ni kwa nini hii nchi inaendeshwa kienyeji kiasi hiki wakati wapo watu wanalipwa mishahaa kwa kazi hizi. Wapo watu pia wamesomea haya mambo. We are a very disorganized society, sijui tatizo ni nini jamani.
 
Licha ya kutupa takataka hovyo. Kuna suala pia la kujisaidia ovyo humo njiani. Kuna vituo maalum/ mapori ya kwenda kuchimba dawa. Humo hata nyasi zimeacha kuota kwani mbolea imezidi kiasi kwamba kuna vipara vya ardhi. Watu wamegeuza mapori hayo choo. Hii pia inahatarisha afya na kuharibu mazingira.
 
Back
Top Bottom