Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,940
- 6,855
FM,
Lete solutions zako za mjini sasa, maana kulalamika tumesikia, na tatizo liko pale pale. Unayeona kuna solutions za vijijini na zile za mjini, basi tuletee za mjini.
Watu wanaendelea kufa kwa magonjwa yatokanayo na uchafu, kwanini tusitafute solution?
Wakipewa Wazungu hayo maeneo, watapata solution, huku Watanzania bado tunasubiri serikali ije utuokoe. Kama mnaweza itoeni hiyo serikali, lakini
kama hamna uwezo wa kuitoa serikali mtafanya nini? Mtaendelea kuzungukwa na uchafu?
Naona Mkuu haukusoma zaidi ya pale niliposema nimetofautiana na wewe! Ungeendelea ungekuta yafuatayo:
Tukitazama hili la uchafu, hata wananchi wa Manzese wafanye nini bila kuwa na chombo kitakachoweza kuukusanya huo uchafu na kwenda kuutupa mahali panapostahili, juhudi zao zitakuwa bure. Mfano angalia vile vitrela vya kuchukua uchafu vinavyo overflow. In desperation wananchi wamefikia hatua ya kuchoma bila kuangalia madhara ya moshi ulio na sumu! Wengine wanawalipa watoto wa mjini kuchukua na kwenda kutupa taka hizo sehemu wanazojua wao.
Hii ndiyo inayonipelekea kusema kuwa katika mazingira ya miji ni lazima utawala uwajibike kwa kuweka nyenzo na system za kushughulikia suala la uchafu. Wakishafanya hivyo, ndiyo waweke bye-laws zitakazomwadhibu yeyote ambaye atasababisha uchafu maana hatokuwa na sababu. Singapore unalipa faini kama unatupa Big G chini, kama hauflush public toilet kwa sababu mapipa na vyoo havikosi maji kwa hiyo hauna sababu ya kufanya vinginevyo. Sehemu nyingi Ulaya wenye mbwa wana wajibika kukusanya choo cha mbwa wao kwa sababu sehemu ya kukitupia kiko kila sehemu. Mtu anayeacha kinyesi cha mbwa wake bila kukikusanya anaadhibiwa!
Utamlaumu vipi mtu kujisaidia nyuma ya mti kama hamna huduma ya vyoo vya umma? Utamlaumu vipi mtu kutupa maganda ya ndizi chini kama hamna sehemu ya kutupia? Na zaidi ya haya, utawalaumu vipi wote hawa kama hauwaadhibu wakifanya hivyo wakati vyoo vipo na vipipa vipo?
Miji inahitaji utawala unaowajibika ili ifanye kazi. Hili sidhani kama tunaweza kukwepa.
Uwajibikaji wa mtu binafsi ni muhimu lakini ina mwisho wake ndiyo maana tunakua na serikali za mitaa. Sasa Mkuu, hilo lundo la uchafu watalipeleka wapi kama serikali ya mtaa haijatenga sehemu maalum ya kutupia taka? Inabidi wa wajibishwe na hao waliowaweka yaani wananchi wenyewe. Nchini mwetu tumefikia hatua ya ukipigwa na kibaka polisi wanakwambia kamkamate umlete! Siku nyingine si nitapiga kelele ili waje watu na mafuta ya taa na matairi? Ni lazima uwajibikaji wa viongozi uwepo.