Uchafu katika miji yetu nayo ni siasa?

Nyami2010

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
227
50
Ndg wana JF

Kwa nini miaka yote, miji yetu ni michafu kiasi hiki? Kipindupindu....imagine!

Leo asubuhi, Radio One wametangaza hali ya uchafu katika Jiji la Arusha nimeogopa. Dar, Moro, Tanga, n.k usiseme!

Hivi, uchafu ni tabia au ni kushindwa kwa wahusika kuchukua hatua?

Nini kifanyike?
 
Kwanza ni uzembe wa serikali kupitia wizara yake ya afya kutokufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa usafi wa mazingira. Pili wananchi kutokuwa na mwamko na moyo wa kujituma kutunza mazingira yao, hapa serikali inalo jukumu la kutoa elimu ya usafi na pia kuweka sheria kali wa wachafuzi wa mazingira.
 
Kwani Manispaa za Moshi na Iringa mbona wanajitahidi? Kulikoni, Arusha, Dar ni kwingineko? Au siasa zinatupeleka huko?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom