Ubungo/Tazara Junctions ?

De Javu

JF-Expert Member
May 5, 2010
264
33
Ubungotazara.jpg

Wakati wasanifu wapo mbioni ku design flyovers za Bongo, mnaonaje mkateremsha kitu namna hii pale Ubungo na kule Tazara?
**Mafisadi hebu jinyimeni mwaka mmoja tu kipatikane kitu namna hii!
 
Hivi ndivyo inavyotakiwa kuwa ili kuondoa msongamano, lakini shida itakuwa space. Hiki kitu kinataka space ambayo haipo, ngoja tuone hao wataalamu watakuja na nini kama ni kweli wana desing fly overs. Maana kwa space iliyopo utaziweka wapi!
 
sijui tutaweza kuendesha hapo. Palivyo Mhuuuuuuuuuu...........

Hapana ugumu wowote wa kuendesha, chukulia hii inayotoka chini kwenda juu ndio ubungo/bandarini. Inayotoka kushoto/kulia ndio Nyerere road (ya juu kabisa) na yenye round about ndio itakayohudumia eneo la buguruni, tazara na kuendelea.
 
Mazee, hiyo picha yako sijui kama hata umeiangalia. Hiyo mbona nayo ni FLY-OVER? Tena sasa yako ina hadi Fly-Under (sijui wanaita hivyo?). Kwa hali iliyofikia Dar, tunahitaji fly-over ziitwazo Diamond Interchange kwani hizi hutumika sana Mijini kwani zinatumia space ndogo. Diamond Interchange ni kama hiyo picha umeweka. Hizi zenye round kubwa, hutumika nje ya mji kwani ukisema ujenge pale TAZARA, basi itabidi hata TAZARA uivunje.

Mwisho ni kuwa hiyo picha, kila kitu pale kimewekwa kwa kupigiwa mahesabu. Huwezi kwenda kujenga kitu kama kile pale Tazara bila ya kufanyia mahesabu idadi ya magari na kukisia kwa miaka 10 au 20 ijayo, kutakuwa na idadi ya magari mangapi na hiyo ndiyo itumike kupigia mahesabu aina ya Interchange na idadi ya LANES za barabara zinazotakuwa kuwepo na mwisho kama kuna haja ya kuweka Traffic light au laa na kama kuna space kubwa basi kuweka round-about ili "kutuliza cars movements".

Mwisho kwa MVUA za Tanzania, huwezi kuchimba chini. Inamaana kuwa itabidi ujenge barabara katika floor mbili. Hapo ndipo unagundua kuwa mkuu, hiyo picha yako italeta UFISADI wa kufa mtu. Ndiyo maana ninasema kuwa mambo ya Traffic Engineering waacheni wataalamu wenyewe. Na hata wakijenga, wasikilizeni Wataalamu wengine wanavyotoa comments. Kuna mambo mengine kwa mtu wa kawaida unaweza kuyaona hayana maana ila kwa waliotengeneza, wanafahamu kwa nini. Kwa mfano unapo-design kitu kama hiki, unaweka kwenye akili tabia za watu wa sehemu hiyo. Ndiyo maana kivuko kilekile na idadi ileile ya magari kwa Tanzania, itaonekana vingine, German na UK itaonekana vingine kwa sababu tu wenzetu wana adabu sana wakiwa barabarani na hata kama hutaki, basi CAMERA zipo kukuumbua.
SR500_DesignViz_0809_500.jpg
 
https://www.jamiiforums.com/jamii-photos/attachment.php?attachmentid=11894&d=1279739872

Mkuu shida iliyopo si kuwa na barabara pana ndani ya mji na zile zinazotoka nje ya mji zikawa nyembamba. Kwa mfano wakati barabara ya Sam ujoma inepanuliwa, hiyo ya Mandela/ Morogoro (Hapo Ubungo) na ya Ali Hassan Mwinyi (Pale Mwenge) ni finyu. Kitaalamu hii inakuwa ni sawa na "bahari kuwa inaingiza maji Mtoni badala ya Mto kuingiza maji baharini".

Ukifutalia rekodi za mipango miji za mkoloni miaka ile ya 1950, ilengo lilikuwa kuwa barabara ya Morogoro iwe na lane zipatazo sita. Lakini ule mradi wa kujenga barabara hiyo wa Ubungo Chalinze, ukaishia kuongeza mitaro mikubwa tu na kuibana barabara kiasi kwamba tukiitaji tena kuipanua itatugharimu zaidi ya kujenga barabara ya kilometa 100 kurekebisha hayo makorongo. Angalia barabara nyingi za nchi yetu upana wake haupo kwenye standards zinazolingana. Kuna zile zinazotoka mijini ni pana kuliko kuliko zinazoingia. Ukienda katika kuu inayoingia Manispaa ya Morogoro unaweza kushuhudis u mbumbumbu wa wataalamu wetu wa Ujenzi, Mkandarasi kajenga barabara ambayo "service road (ile ya wapitao kwa miguu) ina lanes mbili pande zote wakati ya magari kupishana inakuwa tabu tupu (10% lazima ilichotwa).

Unaweza kuona sehemu ya usanifu wa barabara za wenzetu hapa hapa Afrika. Hili ni eneo ambalo ardhi ni haba kuliko Tanzania.



Jo_burg_road_ws.JPG






















<!-- PHOTO 480 x 320 -->

1.1264249698.flyovers-they-call-them-here.jpg



Flyovers

<!-- PHOTO 480 x 244 -->
1.1264249698.highway-flyway.jpg


Highway flyway
 
Mnataka flyovers mnafikiri Chama Cha Majambazi kitapata wapi vijisenti? Mnataka Chalinze lile hekalu lisijengwe, au RA asipeleke fweza Iran, Je Pesambili Mramba aache kujenga kwao? Au mmesahau Che nkapa na Kiwira. Vipi BOT twin towers Nimrod Mkono atapata wapi fweza ya kununu jet etc. Watanzania wataendelea kufa kama inzi na vifo vya mende hadi pale watakapopata akili ya kuwaondoa wafanyakazi kama Dau wa NSSF ambao wanaangalia matumbo yao wakati watoto wanateketea kule Tabora kwenye investment za kitapeli. Au JK na kumbatio lake la Mafisadi kutoka nje.
 
uliza pesa yake ni bei gani hapo....na je, hii ni ya muhimu kuliko kulipia wanafunzi vyuoni, kujenga shule za maana, kulipa mishahara na maisha mauziri kwa walimu wetu ili wafundishe vizuri, kujenga hospitali, kujenga barabara zinazounganisha miji na miji kuliko zilizoko mjini ndani etc. hapo ndo utapata jibu kamili kama inawezekana kuwa hivi tz au la! na tunahitaji karne ngapi kufikia hapo....

watakubali kupunguza garama za administration ya selikali yao...mashangingi yatafutwa, ufisadi utapigwa vita bila unafiki?...etc. kama majibu yote hapo ni No...pesa kama hiyo tutapata wapi?..tutakinga bakuli?...
 
Kama sijakosea kuna habari kua serikali ya Tz na serikali ya Japan zinashirikiana katika hatua za awali za utayarishaji/ubunifu wa michoro itakayofaa katika hiyo mada, baadae kwa kushirikiana na serikali hiyo hiyo ya Japan kuangalia uwezekano wa kugharimia ujenzi huo, kwa maana hiyo mkae mkao wa kula. Swali kuhusu hizo picha zilitolewa na wachangiaji mbali hizo ni kama dreams, nini kitakua tusubiri wahusika.
 
Back
Top Bottom