Elections 2010 Ubunge jimbo la Sikonge

Mkuu Mtanzania,

Mimi nina multiple-citizenship ya Rungwe, Kyela na Sikonge. Kwa hiyo zikija siasa za Rungwe Mashariki na Magharibi nitachangia, zikija za Kyela nitachangia na zikija za Sikonge pia nitachangia. Michango yangu ni ya ku-identify weaknesses ili mhusika aweze kuzifanyia kazi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake na wananchi waliomchagua.
Mkuu Keil,

Naona wewe umemzidi hata Sikonge maana nina uhakika ya Rungwe Magaharibi na Mashariki atakuwa hayajui. Yeye ni Kyela na Sikonge tu.

Sikonge mna watu wengi wazuri, watumieni kusukuma gurudumu mbele. Msije mkageuka Kyela ambako siasa za jino kwa jino zinatawala.

Kama una ushauri kuhusu Kyela basi nitumie PM.
 
Mganyizi,
Hawa watu huwa wako kimya kabisa na hata kuja nyumbani kujenga au kuwekeza hamna. Sintashangaa kuwa Dar au Moro ameweka Mzinga la hekalu na Sikonge ana kibanda cha kugombea ubunge.
Nkumba kashajionyesha kuwa hafai na hamna zaidi cha kuandika. Huyu Mzee sijawahi hata kumsikia ingawa jina la Kapya ni maarufu sana Sikonge ila kafanya nini, mhhhh!!!!!

Unaweza kutupa sababu za wewe kusema Nkumba Na Kapya hawafai?
 
Loohh, Vadugu vane (wandugu zangu),

Huu mjadala kwa kweli ulinipita kushoto na asante Keil kwa kunishtua. Nilishindwa kuupata hadi nikatumia jina la huyo mzee David Kapya.

Kumbe Sikonge ina watu wengi tu. Mie nilifikiri tumechoka sana na hatuna watu wanaoweza kuisaidia Sikonge yangu hii.

Huyu Mzee na Nkumba nadhani wote hawafai. Too sad Yongolo hawezi kugombea kwani eti na sisi Wanyamwezi tuna ka URAIA.

Walimkatalia baba yake na kisa tu kuwa Yongolo ni Wahamiaji. Upuuzi wa hali ya juu. Tunakubali kuwa na Nkumba kama Mbunge na kisa tu kwa sababu ni Mzawa na jamaa ni kweli kabisa ni MWALIMU WA SHULE YA MSINGI.

Ngoja nipate more datas na ntachangia zaidi hii kitu.

Muhanya..... (Mkuu)

Twende tukapige kazi tulichukue jimbo letu, mimi binafsi nina uhakika wa kuzoa kura vijiji vifuatavyo Sikonge, Ipole, Tutuo, Chabutwa, Mlogoro, Kabanga, Mibono mpya, Usunga I and II, Msuwa, Kininga, Kipanga, Kiloleri, Mkolye, Utimule.

Mzee naona ushavisahau vijini vyetu nini? ha ha ha - wakati tunakatiza kutafuta maembe, matonga ,tulantu na ntararii. :smiling:
 
Loohh, Vadugu vane (wandugu zangu),

Huu mjadala kwa kweli ulinipita kushoto na asante Keil kwa kunishtua. Nilishindwa kuupata hadi nikatumia jina la huyo mzee David Kapya.

Kumbe Sikonge ina watu wengi tu. Mie nilifikiri tumechoka sana na hatuna watu wanaoweza kuisaidia Sikonge yangu hii.

Huyu Mzee na Nkumba nadhani wote hawafai. Too sad Yongolo hawezi kugombea kwani eti na sisi Wanyamwezi tuna ka URAIA.

Walimkatalia baba yake na kisa tu kuwa Yongolo ni Wahamiaji. Upuuzi wa hali ya juu. Tunakubali kuwa na Nkumba kama Mbunge na kisa tu kwa sababu ni Mzawa na jamaa ni kweli kabisa ni MWALIMU WA SHULE YA MSINGI.

Ngoja nipate more datas na ntachangia zaidi hii kitu.

Muhanya - Nkuba kazawadiwa jimbo sababu ya baba yake mzee Nkumba - nakumbuka nikiwa shule ya msingi mzee Nkuba alikuwa kama Rais wa Tabora - wakati huo akiwa mwenyekiti wa CCM wa mkoa, na chama kimeshika hatamu acha bwana.
Ameshastaafu lakini CCM mkoa wakampa zawadi ya mwanae - kama mnavyojua Siasa la kurithishana. kifupi Saidi kapitia mngongo wa babake mzee Nkumba na yeye professional yake ni Mwalimu ana-hold Cheti cha ualimu wa shule za msingi...
 
Kipindi muafaka watanzania tuchambue pumba na mchele kama kweli tunataka kuondokana na lindi la umaskini na ufukara...tusiangalie nani au anafanya kazi na nani aua ana udugu na nani..........:dance:
 
Kipindi muafaka watanzania tuchambue pumba na mchele kama kweli tunataka kuondokana na lindi la umaskini na ufukara...tusiangalie nani au anafanya kazi na nani aua ana udugu na nani..........:dance:

Ndicho hicho tunaongelea hapa kwamba viongozi weak wanapatikanaje? mfumo wa kurisishana uongozi ndicho chanzo, kama baba yako alikuwa kiongozi mzuri basi si tiketi kwamba na wewe utakuwa vivyo hivyo - viongozi wengi wanaotokana na system hii wengi wao wanakuwa mzigo kwa wananchi.
 
Waliopo na watarajiwa waliojitokeza so far kwa mkoa mzima wa Tabora ni bogus!
 
Ahhh Mkuu Elnino,
Nisahau wapi hayo mambo? Ninamiss sana "mahama" maana zamani pale Usupilo, Sikonge kama unakwenda Kisanga, kulia kulikuwa na mji wa Shangazi na mumewe Elia Masanja. Ukienda kumtembelea wakati wa likizo basi unakuta yameanguka, ni raha tupu. Nyumbani mzee alikuwa na miti mingi sana ya matunda kama mapapai, michungwa, mastafeli, matopetope, mapera, limau, maembe, miforosadi, minazi ............
Msituni ndiyo unakuta Nsungu, nkuni, matonga (tulipokuwa JKT Msange, watoto wa Dar walikuwa wanayala kama hawana akili nzuri), Nfulu, ....
Kuwinda ndenge vipi? Upile, Kigwaulima, Jorwe, titi ( wa mpotya mpotya, kwikala mkalambo Lu**ndo fyetete, mtwee pono. Mtaka kwa mponda kusema, lakini limvwa, ihhhh kusata....) Ahhhh, those was real sweet old days. Elnino memory yangu huwa inafanya kazi safi sana. Hivi yule Ndege anaitwa MTINDI, kwa kiswahili anaitwaje?

Turudi kwenye habari kuu. Kwa mwaka huu mie lazima nikiri kuwa sijajiandaa na sidhani kama hata ntakuja kugombea. Ntaanza kuangalia mipango kwa mwaka 2015 kama Mungu akipenda mwaka 2012 dunia isiishe maana wanasemasema sana. Kuna viongozi wazuri sana Sikonge ila tu wengi wakiondoka Sikonge basi wanasahau kabisa na kuja kukumbuka kurudi Sikonge kuomba ulaji tu. Hii haitawapeleka mbali kwani unakuta wanapitwa hata na Mwalimu wa shule ya Msingi, kijana Said (Hitler) Nkumba. Huyu Nkumba mwenyewe ni mshamba wa kutupwa jamani. Yaani pamoja na yote, kaja kujenga mzinga wa jumba kule Mole. Utafikiri anajiandaa akizeeka basi arudi kulima tumbaku. Sasa unategemea mtu kama huyu alete mawazo mapya kwa wananchi? Kama yeye mbunge anaenda kujenga Mole, basi walimu wa shule za msingi wakajenge Ntankwa kama siyo Utawambogo.

Umasikini na ujinga wa Sikonge, umeifanya Sikonge kuwa moja ya mihuli ya kuipigia kura CCM. Yaani Sikonge hata uweke NYANI kwa kiti cha CCM, basi ni kuwa watamchagua CCM. Nina uhakika kabisa, utasikia Wanyamwezi wanamsifia kuwa huyo nyani kapendeza sana ndani ya suti ile ya kijani na kwa hiyo atampigia kura. Siku Sikonge itaamka basi ujuwe CCM imekufa. Nina uhakika CCM kura yao ya mwisho kabisa itakuja kutoka Sikonge. Ubaya tu ni kuwa hela za kifisadi hazifiki kabisa Sikonge. OVYO KABISAAA...... Ila huwezi kushangaa hilo kwani unakuta mtu anajiona MATAWI sana na kisa tu ni kuwa anafanya kazi kwa Hemed Nassor au ndugu zake. "ahhh, sasa hivi mie ni Bishaushi na ninafanya kazi kwa Rashid Koronzo..........." Jamaa kakupigia kisuti cha kaki na ndani ana wake wawili........... Ka uswahili ndiyo kamejaa na kujifanya mtu wa dini saaana wakati dini yenyewe haifahamu.
Nilicheka siku moja mzee fulani kakutana na Sheik wa Sikonge. Aliposalimiwa "salaam Aleikum mwana Mbati......" Mzee akajibu kwa adabu sana (ingawa alikuwa mkristo) kuwa ".... waleka Muislaam." Hapa alimaanisha Aleikum Salaam ila hilo neno kwa Kinyamwezi linakuwa "kaacha Muislaam".

Bado nakusanya datas na ntakuja na habari kamili soon juu ya uchaguzi wa Sikonge. Mapalamu ya kuchoka.

Muhanya..... (Mkuu)

Twende tukapige kazi tulichukue jimbo letu, mimi binafsi nina uhakika wa kuzoa kura vijiji vifuatavyo Sikonge, Ipole, Tutuo, Chabutwa, Mlogoro, Kabanga, Mibono mpya, Usunga I and II, Msuwa, Kininga, Kipanga, Kiloleri, Mkolye, Utimule.

Mzee naona ushavisahau vijini vyetu nini? ha ha ha - wakati tunakatiza kutafuta maembe, matonga ,tulantu na ntararii. :smiling:
 
maana yeyote atakayepita kura za maoni CCM basi tayari ni mbunge wa Sikonge, kama mkuu Sikonge alivyosema!
 
Mkoani Tabora, Jimbo la Urambo Mashariki, Samuel Sitta alikuwa akiongoza kwa kura 6,130 dhidi ya Masoud Maswanya

mwenye kura 2,432 na Ali Karavina kura 464. Jimbo la Urambo Magharibi (sasa Kaliua), Profesa Juma Kapuya anaongoza

kwa kura 5.656 dhidi ya Ramadhan Kalla mwenye kura 751.

Jimbo la Nzega, Hussein Bashe alikuwa akiongoza kwa kura 6,815 na Lucas Selelii ambaye niMbunge aliyemaliza muda
wake, ana kura 1,420.

Jimbo la Bukene, Mbunge aliyemaliza muda wake, Teddy Kasella-Bantu ana kura 1,968 na Suleiman Zeddy ana kura 1,727.

Sikonge ni George Kakunda anaongoza kwa kura 1,570 dhidi ya Mbunge anayemaliza muda wake, Said Nkumba mwenye kura 1,365.

Tabora Mjini, Ismail Aden Rage anaongoza kwa kura 4,145 dhidi ya Mwanne Mchemba ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu

mwenye kura 2,985 na mbunge wa jimbo hilo, Siraju Kaboyonga ana kura 835.
 
Wakati tukisubiri majibu huko Sikonge, naomba mwenye kuweza kunipa maana ya hama maneno maana naona hiki ni Kimyamwezi cha Igalula na nimetoka kapa. Nitakuwekeeni link za miziki hii kwa atakayetaka kuvuta au kununua. Imenifurahisha sana Kinyamwezi kisicho na maneno ya Kiswahili mengi. Yaani ni pure. Hivi neno MAZUBA ni nini?

YouTube - Nyamwezi-Uwi, mamsanga makumbulage wagela mnyabo

Lazima nikiri kuwa imenikumbusha ngoma ya Marehemu Mwanywele wa Urambo au Mwinamila pale ofisi ya PM Dodoma.
 
Mkuu,
Nilikuwa sijaona ujumbe wako. Jamaa nasikia ni mzuri. Nafikiri iwe isiwe, atakuwa bora zaidi ya Nkumba. Kama akifanya mzaha basi lazima afahamu kuwa mwaka 2015 nitakuwa Sikonge nikichukua form kwa kutumia CHADEMA.

Bahati mbaya Mkuu wa Wilaya anaweza kuondoka maana kashinda kwenye uchaguzi wa ubunge. Jamaa alikuwa msaada sana zaidi ya huyo Nkumba. Alikuwa na wananchi katika kuwasaidia kimawazo na nini wafanye ili wainue kipato chao. Moja ya miradi ni ufugaji wa Samaki. DC wetu, kila la kheri huko uendako na tutakumiss sana.
Mbona Kakunda kashinda, hamna habari, Kakunda maana yake Njiwa! Karibu Mbunge mteule Kakunda!
 
Eeeh, mwe vwagosha, mbe kakunda kakindaga, Mulungu wa kisa, Nkumba wale wanfulaa na oyagayegu mwi bunge!
Leke kowone nakakakunda nako kaketa vihe, hamo mhanya wiswe wa nse okowonela kisa kovwa kawaziri ko magombo ga "ujenzi!
Mbe kwena kinto kemo kokovwa kekovwa kotandola nzela yafii( tarmac ) kofuma ha Nzega, yevwetele ha Ntoola kayewaye yedolekezwe ko Mbeya na ko Mpanda!
Nizokela, balozi wiswe mbe wale asogolwe sanga yale yekavwa kwapandeka waziri, balozi vwimanyile sana na Kikwete, wose wale wayanda vwa kanola mino (Nyerere), watomamage hakemo, wale akapiwa owaziri!
 
Haijavamiwa Mkuu. Tumekimbia kule kwa Wanyakyusa wale wajinga kama nini. Wanatukanana huku wanatoka kijiji kimoja.

Sasa tuko hapa twala Kinyamwezi. Samahani Mkuu kama utakuwa hukuelewa. Tupo tunasogoa Kikwetu kidogo maana wengine wa mijini wanasahau na si vibaya wakikumbushwa.
MODS mko wapi thread imevamiwa ?
 
naomba breakdown ya kura walipota wagombea wote huko sikonge, na kule njombe kwa Danford mpumilwa
 
Back
Top Bottom