Elections 2010 Ubunge jimbo la Hai

Kwayu

JF-Expert Member
Nov 8, 2007
499
92
Kwa yeyote menye wasifu wa bwana Christopher Winea Mushi anayetaka ubunge jimbo la hai na ambae amechaguliwa kuwa kamanda wa vijana wilaya ya Hai please, ili tuweze kumfahamu kama anastahili ubunge au ni fisadi
 
Hivi mtu hawezi kuwa au kugombea ubunge bila huo ukamanda wa vijana?kazi kweli.Huko atakutana na Sauti ya Zege Freeman Mbowe

Mwaka 2000,nilikuwa nasoma kidato cha pili shule moja huko Hai,kwa kweli kishindo kile cha Mbowe,CCM Hai hawatakisahau.Sasa huyu kijana anaenda kuaibika
 
Nadhani hakuna haja ya kutafuta wasifu wa Bwana Christopher Winea Mushi,huyu wala hawezi kuteuliwa na CCM kugombea ubunge jimbo la Hai labda kama atagombea udiwani lakini ubunge hapi kitu.CCM wanamwandaa Bwana Meena kupambana na Freeman Mbowe tusubiri kidogo mambo yatawekwa hadharani.
 
Kuna Chrispher Mushi fulani mtu wa Machame alisoma Ilboru, kama ni huyu, basi Mbowe ana kibarua kigumu mbele yake, Jamaas hawa ndio wenye Meru Farmacy za AR na MS. Ni debeter mzuri sana na alifanya kazi UNDP.
 
Huyo Meena ni nani?

Na sas Mkuu,Pasco...

Mbowe anamiliki Hotel,Club,amewekeza kwenye Media na ana uwezo wa kujenga hoja pia.Pia ni Katibu wa vyama vya kidemokrasia Africa
 
Huyo Meena ni nani? Kuwa na PHAMACY arusha na moshi ni kigezo cha kushinda kweli?
 
Ni mtoto wa marehemu Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Kilimo na Mifugo, Awinia Abel Mush,Mushi ameanza tangu kama miaka 2 iliyopita kuweka mizizi kwa kujishughulisha na wananchi na shughuli zao za kimaendeleo.
Na hivi karibuni alitowa msaada wa fedha kwajili ya kujenga daraja la mto Mongwa, kutokana na usimamizi mbovu jamaa wa serikali ya kijiji wamekula pesa zote na daraja limeshindwa kukamilika.
 
Kuna Chrispher Mushi fulani mtu wa Machame alisoma Ilboru, kama ni huyu, basi Mbowe ana kibarua kigumu mbele yake, Jamaas hawa ndio wenye Meru Farmacy za AR na MS. Ni debeter mzuri sana na alifanya kazi UNDP.

Ndio huyo huyo Mkuu Pasco walisoma pale enzi hizo na akina Simbo Mushi.Mbowe kweli hana kazi ngumu sana kama ulivyo sema maana Christopher hana ushawishi sana kwa watu wengi kama ilivyo kwa Mbowe,Mbowe ana kubalika zaidi na yuko kwenye ulingo wa siasa mda mrefu.
 
Sasa kama hawezi kusimamia hata hela ambazo zinatoka mfukoni mwake,je atakuwa na uchungu na hela za serikali kweli?
 
Ataweza kupambana na akina Fuya Kimbita na Meena tuliyemsikia ndani ya CCM kweli?
 
Huyu jamaa atateuliwa na CCM maana Mama vicki Nsilo Swai ambaye mwenyeti CCM mkoa wa Kilimanjaro,ana muunga mkono jirani yake Christopher na yeye ndiye aliyempa wazo la kugombea ubunge kwani jamaa alikuwa anataka kugombea udiwani tu.
 
Sasa kama hawezi kusimamia hata hela ambazo zinatoka mfukoni mwake,je atakuwa na uchungu na hela za serikali kweli?

Hilo nalo ni tatizo ila jamaa nguvu yake kubwa inatoka kwa Mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro Vicki Nsilo Swai

View attachment 9848
Mama Vicki Nsilo Swai (ktk)

Huyu Mama ana nguvu sana kwa mkoa wa Kilimanjaro na yeye ndiye anasuka mpago wa kumngoa Mzee Ndesamburo jimbo la Moshi mjini.N hivi karibuni wataitisha harambee maalumu ya kuchangia CCM ili kumngoa Mzee Ndesa.
 
Christopher alikuwa Programme Officer (Poverty reduction) UNDP, Tanzania. Sijui kama bado yupo au la
 
Hilo nalo ni tatizo ila jamaa nguvu yake kubwa inatoka kwa Mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro Vicki Nsilo Swai

View attachment 9848
Mama Vicki Nsilo Swai (ktk)

Huyu Mama ana nguvu sana kwa mkoa wa Kilimanjaro na yeye ndiye anasuka mpago wa kumngoa Mzee Ndesamburo jimbo la Moshi mjini.N hivi karibuni wataitisha harambee maalumu ya kuchangia CCM ili kumngoa Mzee Ndesa.

Wanapoteza muda tu! Mzee Ndesa yuko vizuri
 
Kabisa. Pamoja na pesa zao,sisiemu wamemshindwa huyu mzee!
Mnadhani Mzee Ndesa ataweza kurudi Bungeni tena? hiyo ni ndoto,Mhe rais aliuwaliza i"Iakuwaje huyu mtu ashikilie Sehemu ambayo ni kitovu cha mapato cha Mkoa kwa kipindi chote hicho? Nataka mwaka huu hilo jimbo lirudi CCM mwaka huu". hapo kila mbinu mwaka huu lazima ifanyike ili kulikomboa hilo jimbo.
 
kwani kampeni iliopigwa moshi mjini mwa 2005 ilikua cha mtoto...CCM makao makuu ilimwomba Zakhia Meghi , asigombee nafasi yoyote, akaongoze kamati ushindi ya wa CHAMA CHA MAPINDUZI pale Mjini Moshi...
Kikwete akitaka naye anaweza kwenda kujiunga na kampeni za kumg'oa Ndesa akapate aibu aliyoipata Mkapa pale Temeke nbaada ya kujiunga katika kampeni ya Sisco dhidi ya Mrema Lyatonga, matokea ikawa Mrema 80% . CCM wanatamani majimbo yote washinde wao, hawajawahi kutamani kuona mpinzani pale Bungeni. kwa maneno ya Kikwete ni sawa na maneno ya Mpinga Democrasia yoyot toka chama hiko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom