Ubunge East Afrika: James Milya anatufaa!!

Nali

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
1,155
811
Wana JF,

Kwa kutambua unyeti wa nafasi hii ya uwakilishi katika Bunge la Afrika mashariki; naomba tujielekeze katika uhalisia na sio hisia au siasa zenye chuki!! Miongoni mwa vijana wetu waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha Mh. James Kinyasi Millya.

Huyu Kijana ana sifa zifuatazo:

1. Ni msomi, mwenye degree ya sheria (LLB) Tumaini University-Iringa
2. Alikuwa Rais wa chuo hicho-aliaminika katika hoja na kutetea haki na maslahi ya wengi.
3. Ana masters ya sheria Pretoria University-South Africa
4. Ana uzoefu mkubwa katika kufanyakazi ndani na nje ya nchi
5. Akiwa intern ya sheria katika mahakama ya ICTR pale Arushakama mwanafunzi wa pretoria Univrsty;
alichaguliwa kuwa Rais wa wanafunzi (Interns) katika mahakama hiyo!
6. Ni Kijana mzalendo, mnyenyekevu, mwenye huba, Busara, Hekma na heshma kwa watu wote
7. Ni Mjumbe wa baraza la vijana la utekelezaji UVCCM Taifa
8. Ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha
9. Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mkoa wa Arusha
10.Ni Kijana mwenye maono na mzalendo mwenye kupenda nchi yake mfano wa Sokoine na Baba wa
Taifa Mwl.Nyerere!

Kwa haya machache na ninaamini wengi wa wana JF wamekuwa wakimuunga mkono Kijana huyu, Basi tuendeleze mshikamano wetu na uzalendo katika kuwapata vijana wazalendo wenye kiu ya maendeleo kwa nchi yetu!! Kila Mmoja atimize wajibu wake kumuunga MILLYA MKONO ili hatimaye atuwakilishe katika Bunge letu la EA!!

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania!!!

Nawasilisha!!!
 
Eeeeh..!!??
(Hiyo rangi ya maandishi yako inaniumiza macho)
 
Sijajua kwa nini amechagua hiyo rangi. Hivi nani wanaopiga kura kuwachagua hawa wabunge????
 
watu wenye kisomo na intergrity kuliko huyu ambae anatumiwa katika siasa za makundi huko ccm wako wengi!! Tunataka wawakilishi wasomi wa kweli ambao wenzetu wakiwaona watajua kuwa Tanzania sasa sio tena siasa na maneno mengi bali sasa ni vitendo tu bila siasa!! Wapo watajitokeza na kama kawaida kutakuwa na mafisadi watakaomwaga fedha nyingi ili cronies wao wachaguliwe lakini nadhani wabunge wamekomaa kuweza kukataa rushwa na kuweka utaifa mbele na kutuchagulia wawakilishi makini!!
 
Yupo kundi gani la lowassa or? Halafu cjakuelewa unaposema ana huba unamaanisha nn?
 
As long as yuko kwenye mfumo huu huu wa watafunaji then he is good for nothing!!!!
 
Hawa Je mbona umewatenga? Kumbuka mfumo wa vyama vingi mambo ya picha na kivuli hakuna tena, Kuna wagombea wengine kama;

1. William J Malecela
2. Happiness Elias
Lugiko
3. Geoffrey
Mwambe (mchumi Benki kuu)

4. Malenya Ngollo

5. Zainab Amir Gama
6. Mrisho Gambo (m/kiti wa asasi ya vijana Jumuiya ya Afrika)

wadau hamfungwi na siasa za ndioooo ama ushabiki chamsingi kujionea sifa zao na sio kuambiwa na ukahamasishwa na mtu ati mtu mgombea fulani anafaa kwa lipi? Ametufanyia nini akiwa katika nyadhifa alizowahi kuzishika?

DhiDAnGAnYikI Ng'o. Network failed try again!!

Watama turi kumwe!
Chaa! Ngachanyikiwo,

pambere wag'ojo!

Lamtondo!!

Wanyambara!

Nibitage!
Pamoja sana wazee!!
 
Safari hii lazima tupeleke watu wenye hadhi na sio vidudumtu kama tunataka nchi irudishe heshima!!
 
Huyo namba 6 mrisho gambo binafsi namwona ni mzuri zaidi kweli kwa upeo alio nao
 
Huyo namba 6 mrisho gambo binafsi namwona ni mzuri zaidi kweli kwa upeo alio nao

Wewe humjui Gambo ni Gamba la kuvuliwa huyo!! Sisi tunae kaa nae ndio tunamfahamu vzuri!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom