UBUNGE: Dili ya kibiashara, au mwito wa kuhudumia wananchi

wabunge wako wa aina nne, na wameingia huko kwa target tofauti, soma hapa chini uajue aina zao
1. kundi la kwanza - wenye nguvu kisiasa na mafisadi wakubwa
hili nikundi ambalo mamlaka ya bunge ni kama yako chini yao, wana pesa, wana influence kubwa sana, hata kichama wana nguvu na kana kwamba hamna wa kuwafunga kengelele ktk chochote wafanyacho.

2. kundi la pili - wabunge njaa
ili ni kundi la wabunge ambalo wako bungeni kwa ajili ya allowance na pesa za wabunge, hapa ndio kuna wabunge wa kuteuliwa, viti maalum, walipitishwa kugombea majimboni kwao wakati watu hawajajitokeza, ili ni kundi ambalo ni benderea hufata upepo, bungeni wao ni ndio tu ktk kila mjadala ilimradi allowance imeingia, ni kundi linalotumiwa na serikali kupitisha miswada, kundi linalotumiwa na kundi la kwanza kupitisha hoja zao, ni waoga kuikosoa serikali kwa kuogopa uchaguzi ukikaribia hawatapitishwa kugombea majimbo yao.

3. kundi la tatu - wafanyabiashara wakubwa na wenye asili ya asia
hili ni kundi ambalo halina njaa, liko bungeni kuweka mazingira mazuri biashara zao zisiingiliwe na serikali, hawajui hata matatizo ya wananchi au wanaishije wala tabu zao, hawana makundi ya kupigana vikumbo kugombea madaraka, wao ilimradi abaki kwenye system biashara zao ziende sawa, hawaudhurii bungeni mara kwa mara.

4. kundi la nne - wasomi uchwara
hili ni kundi la wasomi ambao wameacha taaluma zao kukimbilia maisha mazuri ya ubunge kwani fani zao hazilipi, ni wanatmiwa kuonyesha kua serikali inafanya vizuri kwa kuandika pepa za uchwara, wanagombewa na wale wa kundi la kwanza ili wale wa kundi la kwanza wajione wana base nzuri, taaluma zao ziko kapuni, hawakosekani bungeni kwa ajili ya allowance zao. solution zao ktk matatizo ya jamii ni zisizoendana na uhalisia wa mambo kwa mfano sasa wamekuja na kilimo kwanza wakati hatuna kiwanda cha kutengeneza matrekta.

5. kundi la tano - wasomi na wazalendo
ili ni kundi la wabunge wazalendo, wanajua matatizo ya jamii na watu, wanajitaidi kuibana serikali kuleta maendeleo, si matajiri, kila siku wako ktk misukosuko kwa misimamo yao, si wengi.

ktk makundi hayo, kundi la pili ndio lina member wengi, no wonder serikali inapitisha miswada kirahisi
 
Mkuu bona, you have an interesting explanation which seems to be somekind of naked truth. Kila siku nikiwa nasikia kipindi cha maswali na majibu bungeni huwa naona ni kama porojo tu, na nikiskia ile inayitwa bunge ilikaa kama kamati ndio utacheka...talk talk..and talk. What is being done not much. Na wabunge wanakuwa united sana when it comes to maslahi ya wabunge, lakini when it comes to maslahi ya taifa wanagawanyika kweli, wengine wanapendekeza wabunge wafungiwe na wengi wanapiga kura ya ndio kwa wabunge hao kufungiwa (Issue ya Zitto Kabwe ambayo baadaye ilikuja julikana kuwa Zotto alikuwa sahihi na waliopiga kura ya kumfungia hawakuwa sahihi).

Ajabu sana, na inasikitisha sana...naona classification yako ya wabunge ni inafanana sana na ukweli.
 
Wakuu naoamba wenye kumbukumbu nzuri mnisaidie kuweka orodha hii. Hili jambo tulizingumzia mwanzoni mwa mwaka huu tulisema watau watakuja kwa gear ya nimeombwa, nimeitwa, nimetumwa, wananihitaji.Na kweli imeanza kutokea. Hii ni kauli iliyotolewa na Bw Samson Mwigamba

“Ni kwa sababu hiyo, nimekubali wito wa wazee wa Magu walioniita na kuniomba nirejee nyumbani kuwasaidia. Ilikuwa niende masomoni mwezi wa tisa mwaka huu nchini Uholanzi kusoma Shahada ya pili ya uhasibu na usimamizi wa fedha, lakini wakaniomba niahirishe kwa kuwa wananihitaji sana hivi sasa, nami nimekubali wito wao. Elimu niliyonayo nimeipata kwa kodi zao na nilisoma kwa ajili ya kuwatumikia wao. Nakwenda kuiongoza Magu”.

There must be many more others who want to use us for their political ambitions.
 
ukiangalia aina ya wagombea ubunge wa siku hizi, ndio utajua bunge limekuwa kijiwe cha kukimbilia wastaafu serikalini, waharibifu wa mali za nchi na pia ni matapeli wa kisiasa. Ati wanadai wameombwa na wananchi, hii haijakaa sawa hata kidogo. Mbunge niliemchagua mwaka 2005, kila akiniona ananinunulia soda, kama vile mie nina shida au mshamba wa soda. Nilijaribu kumuomba mara kadhaa aje aonane na vijana waliomchagua japo tu kuwasikiliza, bt hakuwa na muda. Juzi juzi ninasikia anasema ati ataendelea kwa kuwa wananchi wamemuomba..!? Labda mkewe na watoto wake....
 
sawia sehemu kubwa ni matakwa na kwa manufaa binafsi,kinachonishangaza sana ni hiki.hivi tunaweza tukamchagua raisi halafu tukakubali atuongoze akiwa anaishi nje ya nchi ?
 
sawia sehemu kubwa ni matakwa na kwa manufaa binafsi,kinachonishangaza sana ni hiki.hivi tunaweza tukamchagua raisi halafu tukakubali atuongoze akiwa anaishi nje ya nchi ?

Kuishi nje ya jimbo ni kitu cha kawaida kwa wabunge wengi hapa Tanzania. Wapo wengi wanaoishi kwen ye majimbo yao lakini wapo wengi tu wanaishi nje ya majimbo yao. Jimbo kwako ni kama biashara, ni sawa na mtu una duka lako mbagala wewe unaishi Tandika, unachuma mbagala unalia tandika. Hatuna sheria ya kumfanya mbunge awe mwanajimbo halisi, hizo ndio sheria tunazopaswa kuziangalia, ni vizuri hata tukiwa na uwezo wa kuwaondoa katikati ya muhula wa ubunge, sio mpaka miaka mitano ipite.
 
Back
Top Bottom