Ubunge au Uwakilishi?

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika hivi karibuni yamenifanya niwe na maswali hasa baada ya Dr. Shein kuanza kuteua wateule wake.

Juzi aliteua wajumbe 8 wa Baraza la Wawakilishi kama Katiba ya Zanzibar inavyomtaka. Mmoja wa wateule hao ni Balozi Seif Ali Idd. Huyu mteule kwa bahati nzuri alikuwa tayari ni Mbunge Mteule/mchaguliwa wa Jimbo la Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Jana Dr. Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ. Mpaka hapo tayari huyu Mzee ana post 3. Mara nyingi vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano na Vikao vya Baraza la Wawakilishi huwa vinafanyika kwa karibu wakati mmoja, je huyu Mzee atawawakilisha wananchi wake wa Kitope au ataenda kuhudhuria vikao vya Baraza ili kumwakilisha Rais?

Kimuundo [correct me if I am wrong], Kiongozi wa serikali kwenye Baraza la Wawakilishi ni Waziri Kiongozi, je, protokali hapa inakaaje maana Makamu wa Pili wa Rais nae ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wawakilishi. Who is senior wanapokuwa huko ndani ya vikao vya Baraza la Wawakilishi?
 
Kwa Katiba ya sasa hakuna Waziri Kiongozi. Makamu wa pili ndie jkachukuwa nafasi yake. Hivyo wananchi wake wataridhika zaidi kuliko angekuwa mbunge wa kawaida na Naibu Waziri wa Mambo ya nje, post isiyo na faida ya moja kwa moja kwa waliomchaguwa.
 
Mmmm itambidi amuone shekh yahya hussein ,ampe japo jini mmoja kwa ajili ya kugawana kufanya hiza kazi,pekeyake itakua ni 1.0
 
Tutegemea kufanyika kwa uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo la KITOPE muda sio mrefu,

NAHISI ni lazima Mhe. itampasa ajiuzulu ili kumpa mtu mwengine nafasi ya kuwa MBUNGE. si tegemei kama anaweza kula kiapo huko bungeni. Logically yeye hawezi kuwa MBUNGE tena kwa nafasi aliyonayo na kazi alizonazo. vyenginevyo CCM wapindishe kanunu za BUNGE ama za Baraza la Wawakilishi. Tusubiri tuone
 
Kufuatia marekebisho ya katiba ya Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais ndo kiongozi wa shughuli za Serikali kwenye Baraza la Wawakilishi. Nafasi ya Waziri Kiongozi haipo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom