Ubovu wa barabara

mboyi

New Member
May 20, 2012
4
0
Kumekuwa na tatizo kubwa barabara ya kutoka bariadi hadi lamadi kawaida unatumia saa moja na nusu kutoka bariadi hadi lamadi kwa wanaoifahamu lakini jamani kwa sasa inasikitisha kwamba unaweza kutumia masaa manne mpaka matano kwa sabau ya ubovu wa barabara hiyo nashindwa kuelewa kama serikali ilitenga mwaka wa fedha 2011/2012 tena ijengwe kwa kiwango cha rami na kampuni ya kichina iko pale eneo moja linaitwa nyakabindi wamekaa tu, walijaribu tu kidogo na sasa hawaendelei tena hiki nacho ni kitanzi kwa serikali inayotawala kwa sababu kama fedha ilitengwa na ujenzi ukaanza na ghafla ukasimama bila taarifa yeyote hili ni tatizo je mnataka tena tusubiri bajeti ya mwaka gani sasa? Na kibaya zaidi tunaelekea kwenye msimu wa zao la pamba ambapo serikali imekuwa ikipata mapato mengi na inachukua na kuondoka tu. Bariadi inalima asilimia 60 ya pamba yote inayolimwa tanzania lakini mpaka leo miaka hamsini ya uhuru hawana barabara ya rami ni aibu sana tunahitaji mabadiliko sasa na serikali iseme kwa nini ujenzi wa barabara ya bariadi kwenda lamadi na bariadi kwenda maswa kuunganisha shinyanga hauendelei! Jamani hata kilomita mia mbili hazifiki ni kama 180 tunamtaka magufuri atueleze kwa nini?
 
Rais yuko marekani kuomba omba huku kaacha nchi yake ina maziwa makubwa matatu , bahari mito gesi makaa ya mawe mbuga misitu na nguvu kazi ya populations ya watu mil 40
 
Subirini mpaka 2015 zote zitatengenezwa kwa rasilimali za hapo madini ni mengi sana huko CDM italifanyia kazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom