Ubinafsi katika matatizo unatuumiza Watanzania.

Mjomba wa taifa

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
231
161
Kila kona ya nchi sasa hivi kuna vilio. Sio watoto sio wazee, si kina mama si kina baba wote wanalia. Wanalia juu ya hatma ya maisha yao yatakuwaje. Wengi hawajui kesho wataamka vipi.

Lakini cha kushangaza kila mmoja amekuwa akilia kivyake. Madaktari walipolia kada zingine walidhani ni msiba wa madaktari tu, wafanyakazi wamelia juu ya sheria ya pensheni sauti zimewakauka wamebaki kimya, wazee vijijini wamelia kupanda kwa bei ya sukari mpaka mishipa ya usoni imewasimama hakuna mtetezi. Leo walimu wanalia tunadhani ni msiba wa walimu tu. Hivi inakuwaje watanzania tusiguswe na matatizo ya jamii nzima. Hivi hatujui kwa njia moja ama nyingine msiba wa jirani ni msiba wako pia?

Wananchi tuamke, tumetoa sauti makoo yametukauka, tuungane pamoja kudai haki zetu hata kwa kuingia barabarani. Mvuvi wa samaki ukerewe akipata matatizo hata wewe ulie songea unaathirika pia.
 
Back
Top Bottom