Ng'wamagigisi
Member
- Jan 3, 2011
- 35
- 1
Toka Bodi ya Mikopo ianze shughuli ya kukusanya mikopo yake iliyotoa imekua ikichukua fixed amount kati ya Sh.10,000 na 30,000 ya basic salary ya waajiriwa wote. Saizi imetoa maelekezo kwa waajiri wote kuwa kuanzia mwezi Oktoba,2012 waajiri wote wawakilishe 8% ya basic salary za waajiriwa wote wenye mikopo HESLB. Kwanza sielewi huu uamuzi umejadiliwa wapi mpaka ukapitishwa, pili ni kwanini wanafanya mabadiliko kama haya kimya kimya tatu hivi kweli na mishahara yetu ya kibongo bongo ambayo inakatwa PAYE, NSSF/PPF, Skill Development Levy etc uongeze na 8% ya hawa jamaa kwei tutabaki na nini. Huku kama sio kulazimisha watumishi hasa wa serikali na mashirika ya umma kuongeza viwango vya rushwa wanazotaka ni nini...km serikali imeishiwa pesa na mawazo ya kubuni njia sahihi zisizo za kibeberu za kupata pesa kwanini wasiombe mawazo ya wananchi??!!