Nimeiona na kuisoma hiyo risala. Kimsingi ina mambo mengi ya maana kama unazungumzia ukweli wa jumla na ujumla wa mzungumzaji (yaani isingekuwa imetoka specifically kwa wanafunzi wenye mahitaji yao maalum kama wanafunzi). Lakini kama ni matumizi bora ya fursa (namaanisha rational utilization of opportunities, neno "rational" badala ya "bora" sina kiswahili chake), wanafunzi hapa walihitaji ushauri zaidi. Nasema hivyo kwa maana kuwa fursa ya kukutana na rais ingefaa wao kuyatatua yale immediate issues zinazowakwaza kimasomo, kama hayo ya upungufu wa hela, matatizo ya matibabu, mahitaji ya kompyuta nk, sasa hayo mengine ya EPA na Richmond wangeweza kumwandikia na kumtumia kwa njia ya posta. Unapomdai mkubwa haki fulani, unaweza kuchomeka siasa kidogo kumuonesha una taarifa na uko pamoja nae katika jitihada za kujenga nchi, lakini usizidishe sana hadi ukaonekana kuwa hoja yako ni kumpinga huyo unayemtaka akupatie unachodai. Naona hawa wadogo zangu (na wengine wanangu) wamezidisha pilipili sasa chakula kikawa hakiliki! Ukichukua hii risala, ukafuta kichwa cha habari na kuwakabidhi watu 10, ukawaambia kila mmoja atoe maudhui au hoja kuu ya risala hiyo unadhani wangesema ni nini? Mahitaji yao halisi hawa vijana wameyafanya yakafunikwa na hoja za ufisadi ambazo kuna watu wengine wenye nafasi zaidi ya kupambana nazo kuliko hao wanafunzi, tupo sisi, wabunge wazuri tu kina Mwakyembe, Slaa, Zitto, Kilango na wengine, nk nk, ndio mgawanyo wa kazi, sasa wadogo zetu hawa wanataka wamalize kila kitu kwenye risala moja?
Ninapingana na uamuzi wa ubalozi kuwazuia kusoma risala hiyo. Badala yake wangewashauri tu jinsi ya kuiweka vizuri (unless wamepewa ushauri huo wakakataa), au wangewaonesha maneno wanayoona hayapendezi. Sasa ikitokea kuwa hayo maeneo ubalozi unayokataa ndio maslahi halisi ya wanafunzi, basi hapo ndio wasaa wa kupiga kelele, na kumuwahishia Field Marshal ES amfikishie muungwana. Risala hii kama ilivyo kwa sasa inafanana na hotuba anayosoma mtu dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa, mfano unapomhoji rais kuhusu ajira milioni 1 alizoahidi, sasa sijui ndio unamsuta au ni nini? Na hapo hapo unamwomba akuongezee fedha za kujikimu nk, sasa wewe kipaumbele chako kipi, uongezewe hela za kujikimu au rais atimize ahadi yake ya ajira milioni 1? Vipaumbele, na matumizi rational ya fursa mbalimbali (kama hii waliyopata ya kukutana na mkulu) ndio vinavyowaangusha hawa vijana.
Mkuu mimi sijaiona lakini kama ilikuwa inauliza mambo ya EPA na RICHMOND sion tatizo, tabaka la wasomi ndo wanaitaji kuoji zaidi mnakata haoji nani kama sio wasomi, wale sio watoto wa shule ya msingi na sekondari, ni watu wazima wana haki ya kujua kinachoendelea kwenye nchi yao.
Hili tatizo mkuu la wasomi wetu kukaa kimya ndo linamaliza vyuo vyetu vikuu, haviwezi kuoji kitu siku tofauti na zamani wasomi wa mlimani wakioji watu wakawaida wanafurahi kuwa wamewakilishwa na chuo chao.