Ubahili kwenye ndoa

Duh sasa mm nilikuwa natoa 70,000/= kwa wiki huduma ya nywele bado naambiwa bahili unaichukuliaje hili? Maana nilikuwa najinyima kunywa Safari nikawa nakunywa Bingwa ili kumfurahisha yeye lakini nimeambulia patupu.

siku nyingine upige mahesabu Fidel...fikiria kila mama angehitaji hizo kila wiki wale wenye mishahara ya laki nne kwa mwezi wange ishije?
70 000 kwa wiki anafanya plastic surgery au ni hizi hizi saluni za kawaida?
 
Mke kujibweteka na kumtegemea muwewe kwa kila kitu kipesa ni vibaya, na mume kumuachia mkewe mzigo wote wa kufinance maisha ya familia ni vibaya vile vile.

kama hawataki kuchanganya pesa zao na kuweka bajeti ya familia, basi wapeane majukumu nani alipie wapi..na huyo mdada asiguse kabisa majukumu ya mumewe, pengine atajirekebisha
 
Kinachomuumiza ni kwamba si kwamba hubby wake huyo hana pesa, ana kazi nzuri tu na analipwa vizuri sana, na akaunti zake (anadai anazionaga ki bahati mbaya) zina salio la kutosha tu. Ila ni bahili!
!:rolleyes:[/QUOTE]

Tunaweza kuanza kulaumu kumbe kuna tatizo zaidi
nilidhan bwn huyu hana pesa ua kuna sehemu anakozielekeza kumbe anazo, yawezekana mama
ni mmbadhilifu hajui thamani na maana ya pesa! Mi nashauri huyu mama kama anavitabia kwamba akiona pesa ndani amani inatoweka ajirekebishe kama pesa zipo inamaana mumewe yuko makini zaid katika maisha
akumbuke "anayependa vya mafuta hawezi kua tajiri"
 
naomba nikae upande wa kiume leo though I am a woman. Mwanaume anapenda sana mkewe apendeze katika kila hali. kwa mfano: huyu mdada anayelalama hapa ana kazi nzuri kama ya mumewe kwa nini msikae chini kufanya mahesabu mjue mtachangia nini kwenye matumizi yenu ya kila siku?

Wanaume wanafikia kufanya hivyo kwa sababu wakishajua vipato vyao utashangaa anaenda kwa jirani kuchuku kadi za michang kila siku ili achangie harusi,kitchen party huku mwenzie amebudget. Maisha ya ndoa ni kuzungumza, kusaidiana katika shida na raha siyo kusaidiwa. kama kuna biashara na kazi za pembeni basi kinachopatikana kigawanywe siyo kutaka tu mwanaume akufanyie kila kitu ndiyo ujue anakupenda. Wanawake ACHENI KULALAMIKA HATA VISIVYO VYA MSINGI.

FANYA NA WEWE AFUATE MFANO WAKO. Wanawak hao hao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuwa nyanyasa kama waume zao hawana vipato.
 
Ndoa ni kusaidiana, kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana kwa dhati. Mimi sijui mwanzo wao ulikuwaje na upendo kati yao ukoje lakini kwa uhakika hapo sio ubahili ila hakuna UPENDO kati yao.
Kutatua hilo tatizo ni kwa kurudisha upendo kwanza kati yao.
Kuna mambo mengi sana kwenye ndoa siku hizi na kuna waharibu ndoa wengi sana siku hizi kuliko zamani. Wazazi wetu zamani walikuwa wavumilivu lakini wanandoa wa kizazi hiki uvumilivu ni 35%.
 
bible inasema msinyimane......quran inasema oa wake kwa kadri uwezavyo ila usiolewe na wanaume kwa kadri upendavyo.........very segregetive.............
 
naomba nikae upande wa kiume leo though I am a woman. Mwanaume anapenda sana mkewe apendeze katika kila hali. kwa mfano: huyu mdada anayelalama hapa ana kazi nzuri kama ya mumewe kwa nini msikae chini kufanya mahesabu mjue mtachangia nini kwenye matumizi yenu ya kila siku?

Wanaume wanafikia kufanya hivyo kwa sababu wakishajua vipato vyao utashangaa anaenda kwa jirani kuchuku kadi za michang kila siku ili achangie harusi,kitchen party huku mwenzie amebudget. Maisha ya ndoa ni kuzungumza, kusaidiana katika shida na raha siyo kusaidiwa. kama kuna biashara na kazi za pembeni basi kinachopatikana kigawanywe siyo kutaka tu mwanaume akufanyie kila kitu ndiyo ujue anakupenda. Wanawake ACHENI KULALAMIKA HATA VISIVYO VYA MSINGI.

FANYA NA WEWE AFUATE MFANO WAKO. Wanawak hao hao ndiyo wanakuwa wa kwanza kuwa nyanyasa kama waume zao hawana vipato.

Du , nimecheka sana. Hyuyu dada ana kazi lakini anadai kipato chake si kikubwa kama cha mmewe so anaexpect mumewe awe anamkumbuka yeye pia kama mkewe. ah it all depends wanaishije, ndo maana nasema inawekana there is more to that than what meets the eye!
 
Endeleeni kutegemea waume zenu bila kujishughulisha akifilisika familia inateteleka na wengi wenu ndo hapa napo wachukia wanawake ukisha fulia tu basi mwanaume unakimbiwa na mke na ndo kama ni mzuri basi inakuwa balaa anahamia kwa wenye fweza wewe unabaki kukomaa sura tu.

Fidel, 2010 or is it 2012 ikifika ndipo utamwelewa Carmel anasema nini.Una point nzuri sana lakini kuna kitu hujakiona.
Katika ndoa kuna ile hali ya kuacha kuwa na changu... mnaanza kusema vyetu.Utashangaa katika ndoa nyingi, wanaume hudhania kuwa mke ni kama kitegauchumi au chanzo cha kujitatulia matatizo - yaani humwachia mke kila kitu kinachohusu kutunza familia- chakula, mavazi, shule za watoto huku akujisingizia yeye anashughulika na mambo makubwa zaidi!Huu ulikuwa mwelekeo wa kizamani enzi za ujima ambapo mwanaume alikua na ardhi kubwa kisha kuoa wanawake lukuki na kuzaa watoto wa kutosha kupata nguvu kazi ya kuzalisha.Wanawake waliachiwa jukumu la kulima chakula kwa matumizi ya familia.Maisha ya sasa siyo yale ya ujima au ya subsistance farming ndugu yangu.Unapooa ujue kama baba kisheria unawajibika kuitunza familia yako - mke na watoto na wategemezi wenu.Na ndio maana kisheria unaweza kushtakiwa usipotimiza wajibu huu.

Hata hivyo, mama/mke anaweza kukusaidia maana tunajua kabisa maisha ya sasa inabidi kusaidiana.

Huo ubahili wa huyu bwana ni hulka ya wanaume wenye umimi.Kitu hawajui ni kuwa unapompa mkeo support ndivyo unavyojipatia zaidi maana mkeo atakuwa na motisha wa kuchacharika zaidi ili afanye familia yenu iwe na maisha bora na ya furaha.

Wapo wanawake wenye kubweteka na kumtegemea mume kwa kila kitu.Hawa nao ni wajinga kwa maana hawana mkataba na Mungu.Hawajui kuna kifo, ugonjwa, kuachana etc.Ikitokea hali hii ndipo huadhirika maana hawajui kutafuta.Kama ulivyosema wako radhi kufanya lolote hata kama ni kinyume na maadili ili tu waweze ku survive.
 
omba usikutane na kademu ka mizinga....utajuuta kukafahamu mpaka utaanza kujiuliza kama mwanajf mmoja alivyo jiuliza....''WHY I GET MARRIED''utadhani alilazimishwa.
 
eeeeh jamani huyo mwanaume ana matatizo ya kisaikolojia hivi haoni hata bible imeandikwa enyi wanaume watunzeni wake zenu na enyi wanawake wapendeni waume zenu..hayo maneno yana utofauti kabisa ingawa sometimez tunasaidiana kukidhi maisha
Huyu dada hatakiwi kukaa kimya kwani tatizo litakuwa sugu na atakapoamua kusema itakuwa too late ..itabidi amuite mme wake na aongelee hayo yanayomkwaza ili wapate muafaka amwambie mmewe vile anavyojisikia na anaona kama hatendewi haki
Kuna watu wengine wanafumbuliwa macho kwa kuambia..Je anamuogopa mme wake ???????

Ni kweli FL 1 maandiko yaeleza wazi kabisa tuwatunze wake zetu nao watupende lakini the kinyume chake pia kinawezekana, kama umtunzi mkeo basi sahau kupendwa vivyo hivyo kama humpendi mumeo sahau kutunzwa.nadhani kwa kesi hii mkewe jamaa haoneshi upendo kwa mumeo ndio maana hatunzwi.
 
Si ni bora mkaweka utaratibu wa kutoa pasu kwa pasu? wengine wamezoea kunyonya tu utakuta mkitu unamlisha, wewe unajituma kumnunulia zawadi kama ngou, pants n.k lakini bado linakuuliza mshahara wako unatumia vipi wakati linajua haliachi hata senti tano nyekundu ya zamani kwa ajili ya matumizi
 
hiyo pesa ya zawadi unahihamishia kwenye mambo yako ya matumizi ya ndani...kama wa hivyo zawadi ya nini.
 
Huyo jamaa ametuaibisha wanaume wote hapa. In fact hakuna mpwa mwenye tabia hizo, tukizigundua tutahoji uanaume wake....
 
Waungwana hii issue ni kweli kabisaa mimi naifahamu, maana kuna wakati ilimtokea mtu wa karibu yangu, lakini yeye alijaribu kumnyima nani hii kila mzee alipohitaji, akadai kuwa anaonewa, mzee ilibidi aanze kubadilika taratibu, na hadi sasa hakuna kitu kinachoitwa ubahili kwa wanandoa hao. Mimi namshauri huyo bibi ajaribu hiyo anaweza kuwini, lakini atumie mbinu hasa maana mzee anaweza kumpoteza jumla, na wajanja wakamdaka nje!
 
kasheshe!
 
Si ni bora mkaweka utaratibu wa kutoa pasu kwa pasu? wengine wamezoea kunyonya tu utakuta mkitu unamlisha, wewe unajituma kumnunulia zawadi kama ngou, pants n.k lakini bado linakuuliza mshahara wako unatumia vipi wakati linajua haliachi hata senti tano nyekundu ya zamani kwa ajili ya matumizi
una hasira, i understand!
 
Back
Top Bottom