Ubaguzi Wa Wajerumani Tanzania

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Hivi serikali yetu hiko wapi wakati hawa wakoloni wanarudi na mambo yao ya kikoloni na ubaguzi kwa Watanzania?

Wafanyakazi wa kampuni ya STRABAG wananyanyaswa kama mbwa. Hawana haki mbele ya hawa wazungu, tena kwenye nchi yao.

Serikali iko wapi jamani?

Source MICHUZI: NAKALA YA TAMICO KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Hatuna serikali. Tunajipendekeza kwa wawekezaji. Angalia hata katika viwanda vinavyomilikiwa na Wahindi jinsi ndugu zetu wanavyonyanyaswa. Kikwete ameturudisha katika ukoloni mamboleo.
 
Manyanyaso si huko tu bali kila sehemu ambapo 'wawekezwaji' wamepewa nafasi.Wananci wengi wanateswa na hata kuuawa migodini,viwandani na maeneo jirani na serikali yetu ikijitahidi sana basi itaunda tume ya kulipana posho na usafiri wanapewa na mwekezwaji ili waende kuchunguza 'ukweli' ambao hautajulikana kamwe.Walivamiwa wageni wachache, mawaziri wawili wakakimbilia huko haraka na polisi wakaagizwa kufanyia kazi haraka na punde tu watuhumiwa wakakamatwa.Hapa maslahi ndio yanapewa kipaumbele si wananchi.
 
Hamna jipya zaidi ya muendelezo wa yaleyale ya kila siku kulialia tu kama watoto!

Hatujitumi kufanya kazi tukionywa au kufukuzwa tunanyanyaswa.
Ni mara ngapi umeshakwenda ofisini iwe ya Serikali au Benki au hotelini au hata Duka la mtu binafsi kutaka huduma na ukapatwa na hasira kiasi kwamba ungeomba hata yule mhudumu afukuzwe kazi mara moja? Na kama jibu ni ndio sasa kwa nini unategemea waajiri hao mnaowashutumu kwa ubaguzi wawe tofauti?

Tuache kulialia tuu kila siku tujitume tutafanikiwa hata kama mtu hakupendi akiona unajituma na unampatia faida mwisho wa siku atakukubali tu, vinginenvyo basi tutakuwa watu wa ajabu sana Dunia hii kila siku tunyanyaswe sisi tu... manake waliokuwa ulaya nao ukiongea nao malalamiko ni hayo hayo waliokuwa China nao malalamiko ni hayo, waliokuwa Malaysia nao malalamiko ni hayohayo tunanyanyaswa, waliokuwa Afrika Kusini nao hayo hayo, acheni utoto wa kulilia hovyo, kazi tu ndio itatuokoa!
 
Manyanyaso si huko tu bali kila sehemu ambapo 'wawekezwaji' wamepewa nafasi.Wananci wengi wanateswa na hata kuuawa migodini,viwandani na maeneo jirani na serikali yetu ikijitahidi sana basi itaunda tume ya kulipana posho na usafiri wanapewa na mwekezwaji ili waende kuchunguza 'ukweli' ambao hautajulikana kamwe.Walivamiwa wageni wachache, mawaziri wawili wakakimbilia huko haraka na polisi wakaagizwa kufanyia kazi haraka na punde tu watuhumiwa wakakamatwa.Hapa maslahi ndio yanapewa kipaumbele si wananchi.

Sasa hapo wa kulaumu ni nani? Mwekezaji au sisi wenyewe? Na ngoja usiende mbali sana na kutaka kusukumia tatizo kwingineko achana na mambo ya wawekezaji wa kigeni, sisi wenyewe kwa wenyewe mambo yakoje? wasichana wetu wa kazi tunawapa haki zao stahiki? kama sio kwa nini unaona ya wageni tu?
Mbona tunawadharau na kuwakashifu wamasai kila siku na kuwatania unafikiri wao wanapenda mbona hakuna mtu anajitokeza kuwatetea si tunaona kawaida tu?
Mbona tunadharau na kudhihaki makondakta wa daladal kila siku na hakuna mtu anawatetea wakati wako kazini na wanategemewa na familia zao kama sisi wengine tu? tofauti iko wapi?

Hivi serikali yetu hiko wapi wakati hawa wakoloni wanarudi na mambo yao ya kikoloni na ubaguzi kwa Watanzania?

Wafanyakazi wa kampuni ya STRABAG wananyanyaswa kama mbwa. Hawana haki mbele ya hawa wazungu, tena kwenye nchi yao.

Serikali iko wapi jamani?

Source MICHUZI: NAKALA YA TAMICO KWA VYOMBO VYA HABARI
waambie hao watz wenzangu waache uvivu, waache kupenda kuonewa huruma, waache malalamiko wakifikiri kwasababu nchi hii ya kwao basi mwekezaji anayewekeza hapa hatawaendesha, wanatakiwa wakubali kuendeshwa alimradi wanapata kazi..kama wameshindwa kazi waache kuna watu wengi bongo wanahitaji kufanya kazi hizo...hao wajerumani wanatujengea barabara, shirikianeni nao ili sisi wa kimara na ubungu tusichelewe kwenda posta....tunahitaji hiyo barabara iishe haraka....wavivu waachishwe kazi kama wapo....tutalalamika hadi lini? halafu unaandika kuwa watu wananyanyaswa bila hata kuelezea hayo manyanyaso hayo ni yepi...unaeleweka kweli wewe? ndo maana watz tunadharaurika.
 
ukifanya kazi kwa bidii hakuna baguliwa, ila kwa asili tukubali tu wavivu, bahati mbaya zaidi ukijituma sana kazini hasa serikalini utasikia wanasema anatafuta sifa. kaazi kweli kweli.
 
Hatuna serikali. Tunajipendekeza kwa wawekezaji. Angalia hata katika viwanda vinavyomilikiwa na Wahindi jinsi ndugu zetu wanavyonyanyaswa. Kikwete ameturudisha katika ukoloni mamboleo.

kweli wewe unayejiita jasusi nimekushusha thamani maana unaongea kama MS..NGE aliyechoka . sasa hapo kikwete ameingiaje au ulitaka kikwete afanyeje. hivyo viwanda vya wahindi vilikuwepo tokea utawala wa nyerere , mwinyi na mkapa. kwenye vikao vya wanaume usijipitishe utabakwa
 
Hawana kosa wanatekeleza ilani ya CCM isiyomjali Mwananchi. ukifika China zile sheria zao ukizikuta pale unaanza kunyoka mwenyewe kabla hata hujaambiwa. haya ndio matunda ya dhaifu, tena nimeona mpaka zile pickup wanaendesha wazungu.
 
Back
Top Bottom