Ubadhirifu halmashauri ya Hai

KISANTILITEDI

Member
Dec 31, 2009
96
27
Maafisa waandamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wanatuhumiwa kumshauri vibaya Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Norman Sigalla, na Mkurugenzi Mtendaji, Melkizedek Humbe, na kuisababisha halmashauri hiyo hasara ya Sh. bilioni 3.1.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Meja Jenerali Mstaafu Saidi Kalembo, alisema atamuagiza katibu tawala wa mkoa huo kuchunguza kesi hizo kama uko uwezekano wa kushinda au la ili wachukue hatua kwa wanaoendelea kuihujumu serikali.
Maafisa hao (majina yao yanahifadhiwa) wanadaiwa kushauri kuvunja mkataba kihuni na kampuni ya Community Development Corporation Ltd ya Jijini Dar es Salaam na hata baada ya kushindwa mahakamani wanaendelea kumshauri mkuu wa wilaya na mkurugenzi ili wasuluhishe nje ya mahakama ili azima yao ya kuchota bilioni 3.1 itimie wagawane na mwekezaji.
Hata hivyo, mkurugenzi wa kampuni inayodai halimashauri hiyo, Amini Kimaro, alikana kuwepo kwa njama hizo.
Wakili Elikunda George Kipoko anayewakilisha kampuni hiyo alisema atawasilisha Mahakama Kuu hati ya kukaza hukumu kwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Hai ameonyesha kutotaka maelewano na mteja wake nje ya mahakama. “Tumefika hapa na mteja wangu kufanya mazungumzo baada ya kuitwa lakini hakuna kikao chochote…mteja wangu anarudi Malawi alipokuwa akiendelea na shughuli zake,” alisema.
Sigalla alisema alimuagiza mkurugenzi kukutana na mwekezaji huyo kuzungumza nje ya mahakama kama kesi hizo zimeibana halmashauri na pia alitishia kuchukua hatua kali endepo atabaini kuna watendaji wanaochochea halmashauri kushindwa kesi mahakamani.
Kesi zinazokaziwa hukumu mahakama kuu kanda ya Kilimanjaro zidi ya halmashauri hiyo ni namba 10/2005 ya kuvunja mkataba kihuni, kesi Namba 11/2005 ya udhalilishaji, kesi Namba 6/2005 ni ya kutoa viwanja mara mbili.
Alipotakiwa kutoa mapendekezo yake endapo halimashauri ina uwezo wakukata rufaa au kutumia njia yoyote kuepusha halimashauri hiyo kufilisiwa Mwanasheria wa halmashauri, Ndegi Marwa alisema kuwa yeye hatoi maoni kwa waandishi wa habari ila atatoa kwa mkurugenzi wake ambaye ndiye mkuu wake kikazi na kwamba anawajibika kumshauri masuala ya kisheria.
Humbe alisema anakusudia kumaliza suala hilo kwa maslahi ya halmashauri pia amekanusha kuwepo maafisa nyuma ya kesi hizo kwa masilahi yao.
Amesema kuwa yeye kama mkurugenzi mtendaji maafisa hao wanawajiba kumshauri ila maamuzi anayo yeye mwenyewe.
“Mimi sio wakuamuliwa nimeshamueleza mkurugenzi wa kampuni inayotudai aniletee vielelezo maana mimi ni mgeni na ameshanipatia nitatoa maamuzi subiri,” alisema.
CHANZO: NIPASHE
 
Tulishazoea kuliwa pesa zetu, kila kona ya nchi zinaliwa,imekuwa wimbo wa CAG!

Mmmh ........................................
NAWAONEA HURUMA WAHASIBU WOTE KWANI HAWATAINGIA MBINGUNI MAANA UFISADI NI VIGUMU KUUEPUKA!
 
Back
Top Bottom