Ubadhilifu malisili -halmashauri ya bagamoyo mtushi mmoja atolewa kafara

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,274
9,911
Mtumishi wa mmoja wa Halmashauri ya Bagamoyo Erick Mnon'gona ambaye alikuwa ni mkusanya ushuru wa wamzao ya miti jana amepandishwa kizimbani kwa makosa ya udhadhilifu wa fedha zaidi ya sh mil 60.

Amekutwa na mashitaka yapatayo 300 na alitakiwa kulipa dhamana ya sh mil 30 au hati ya nyumba iliyofanyiwa tathimini hata hivyo mshitakiwa aliekana mashitaka na kupelekwa lupango kwani alishindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Binafsi nimekuwa nikifuatilia sana sakata hili la ubadhilifu wa idara ya maliasili almashauri ya Bagamoyo, Huyu kijana watakuwa wamemtoa kafara kwani kwa mujibu wa habari nilizonazo sinasema TAKUKURU Waligundua zaidi ya milioni 100 zilitafunwa na wakuu wa idara lakini walitembeza mlungula kwa maafisa hao wa TAKUKURU na ndupo walipoamua kutoa kafara kijana huyo ili kuwalinda wabwana wakubwa.

Mfano mkuu wa idara hiyo anayejulikana kwa jina la Msaki anavijana wake ambao wapo kwenye mapori ya bagamoyo wakishirki katika ufanikishaji wa uvunaji wa miti na mkaa kinyume na taratibu.

Huyu jamaa kwa pale bagamoyo ni mmoja wa wanaojulikana wanautajiri mkubwa unaotokana na kutumia cheo chake kwa maslahi yake, anamiliki mashamba karibu vijiji vyote bagamoyo mfano pale kidomole anaheakari zaidi ya mia 600.
 
Back
Top Bottom