Ubabe wa mgambo wa jiji hadi lini....??

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Hii ni hoja binafsi....

Kwa kweli nasikitishwa sana na hili 'jeshi' la mgambo wa jiji.,sipingi uwepo wao kwani limetoa ajira kwa vijana wengi tu wa Tanzania.,kinachonikwaza mimi ni utendaji wao wa kazi, sina hakika kama wanapatiwa mafunzo ya kutosha ikiwa ni pamoja na hata basic knowledge ya sheria na haki za binadamu au ndio wanaokotwa tu hovyo hovyo na baada ya siku mbili tatu wanapewa magwanda na kuingia mitaani.
Hawa jamaa naona wao ndio wanakuwa kero badala ya kutusaidia kupunguza kero hapa jijini.,sina shaka kuwa ni mambumbumbu wa sheria ndiyo maana utendaji kazi wao una walakini sana hebu angalia jinsi wanavyowavamia wafanya biashara na kuwapora vitu vyao, ona jinsi wanavyobeba masufuria ya mama lishe na hata wasiyafikishe huko ofisi za jiji badala yake wanazunguka kona na kula chakula chote.,wale wanaozunguka na breakdowns ndio usiseme wananuka rushwa kupita kiasi.
Nahisi walioanzisha 'jeshi' hili hawakujipanga vizuri, ndio maana wala hawaheshimiki, inabidi waangalie upya hii kada ambayo naona ikitumiwa vizuri inaweza sana kusaidia walau kuwapunguzia mzigo polisi.,naomba tu Mungu wakuu wasijiloge wakawapa hawa jamaa bunduki tutaisha wote huku mitaani.
Nawasilisha.
 

Attachments

  • machinga.jpg
    machinga.jpg
    27.3 KB · Views: 91
attachment.php


Hivi yupi ananyanyasika hapa?

Ukiona hali hii ujue kuna tatizo sehemu.,si kawaida sana kwa raia kutunishiana misuli na vyombo vya dola.,hapa inawezekana kila mtu ananyanyasika kivyake, lakini tujiulize ni kwanini hali hii itokee?.,mbona si kawaida kuona taswira za namna hii pale ambapo polisi huwa wanahusika kwenye operesheni mbalimbali.,tafakari ni kwa nini hawa jamaa wanadharaulika kama siyo kutokana na mapungufu ya utendaji wao wa kazi.
 
attachment.php


Hivi yupi ananyanyasika hapa?

Unajua katika kukabiliana na watu unatakiwa jua kuwa kuna vitu viwili navyo ni trigger (Kichochea hasira) na Inhibitor (Kipunguza hasira). Kwa mgambo aliye fundishwa vizuri anatakiwa jua kuwa behaviour yake ndiyo itakayomfanya raia kubehave the same. Mgambo na polisi huku kwa wenzetu always wanakuwa katika nafasi ya inhibition na kuacha raia kuchagua upande ambao mwisho wa siku anajikuta yupo kwenye upande wa polisi (inhibition side).

Mgambo na Polisi wa Bongo wao always ni side ya "trigger" kama kumtukana mtu, kumkunja shati, kumpiga virungu na kufanya kila awezacho ili kum-provoke raia aje upande wake wa trigger. Sababu kubwa ni kuwa wanajiona wao wana authority kwa kupewa ama rungu ama bunduki. Umefikia wakati sasa tuwafunze Polisi na Migambo wanaokabiliana na watu mbalimbali (Wehu , wazima, wasiojiweza) jinsi ya kudeal na watu.

Nina uhakika hapo aliyeanzisha timbwili ni Mgambo tu no way na sasa anajidhalilisha matokeo yake anaona aibu kumwachia jamaa kwani ataonekana hawezi kazi, what next?ni assault tu hapo.
 
Back
Top Bottom