Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
KWA WANANCHI KIGAMBONI ALIONGEA HIVI:
Kauli inayodaiwa kuwaudhi wananchi hao ni ile iliyotolewa na Waziri Magufuli Januari Mosi, mwaka huu, alipozungumza na wananchi wa Kigamboni kuhusu nauli hiyo mpya na kuwaambia kuwa
asiyetaka kulipa nauli hiyo
- apige mbizi baharini
- kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au
- arudi kijijini akalime.
KWA WAANDISHI WA HABARI ALIONGEA HIVI
Pia baadaye siku hiyo hiyo, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo, alisema
yeyote asiyetaka nauli hiyo mpya kutozwa,
anunue kivuko chake na akitaka akipe jina la chama chake cha siasa kisha atoe huduma hiyo kwa Sh. 100 au bure ilimradi aende kwake (waziri) kupata kibali cha kutoa huduma hiyo.
Mtazamo wangu juu ya Magufuli
Nilivyokuwa namfikiria Magufuli kwa sasa nimeanza kubadili msimamo, maana mambo ya uongozi si shauri ya kufanya utakavyo na kutojali wananchi unaowatumikia. Na mtazamo wake kila kinachopingwa anasukumia vyama vya siasa kama alivyoongea na waandishi wa habari. Huu ni upeo wa kidikteta, Magufuli ni mwanaharakati wa mfumo wa kidikteta.