Uasi wanukia CCM

CCM kuna viongoz wa ajabu sana, kwenye uchaguzi mkuu huwa wanaungana wote kuchakachua kura za wapinzani ila kwenye chaguzi za ndani ya chama huwa hawaangaliani usoni kabisa kila mtu na nafasi yake' utaskia huyu katishia huku, huyu kabeba bastola anataka kumuua mwenzake mara huyu kahama chama au anataka kuanzisha chama chake baada ya kuchezewa mchezo mchafu, wao huwa wanadai ni upepo tu utapita.
 
Bado sijaona mpamabanaji wa UFISADI wa ukweli ndani ya CCM, walio wengi ni wanafiki baada ya kukosa aina ya maslahi wanayoyata basi huhamia kupiga vita wenzao kwa njia ya kudai wanatetea wananchi .WOTE NI WEZI,WAONGO ,WANAFIKI .
 
Mpambanaji mwenyewe ni sita eti!

Huyu naye (Sitta) anatia kichefuchefu. Kila kukicha anajidai anapambana na ufisadi, ni ufisadi upi anaopingana nao? Ajipime kama anaweza kupambana na chama kizima cha magamba ilhali akiwa ndani ya hicho hicho chama anachopingana nacho. Aache kutuona watanzania kuwa ni majuha. Kama ana nia ya dhati ahame chama akapambane nje ya ccm tutamwelewa. La sivyo akae kimya tutamwelewa zaidi.
 
Tatizo wanafanya uchaguzi wakiwa wamegandamizwa na jinamizi la uchaguzi 2015!!
 
Ndoto za alinacha hiki ni chama cha mapinduzi; waliondoka kina Mrema hapo mwendo mdundo asiyekubali maamuzi sahihi ya chama na aanze!

Chama
Gongo la mboto DSM
Hayo ni maneno ya kujifaliji, uliza kenya wapi KANU siku hizi
 
ccm ndio mwisho wake wake huu sina imani kama watanusuka kwenye kiama hiki laana za watanzania lazima zionekane hapa hapa dunia wala si CDM/CUF bali wao kwa wao
 
Siyo tu CCM itasambaratika bali hata Engine yao inayoongoza nchi itawaka moto hewani na mara wote mtashangaa how come! Butwaa yaja sooner than I anticipated duuh!..Hollygost over to you am tired of my country being led by witches in their coven.

I set ablaze all the altars raised to baal the godes of Pharaoh by fire by force in the name of the most high Jesus Christ of Nazareth!

In Jesus name I claim back my country and its people.....Father from now on expose all who by their doings are against your good will of prosperity to the people of Tanzania. I command all the fisad to start eating their flesh and drink from their own blood...Angels of God do your work from east, west, south and north gather them all; bind them and burn them to the ashes like you did in the days of Lutu and Abraham in the Cities of Sodoma and Gomora. God as you are the same yesterday today and forever; let your Glory prevail in Tanzania. Amen!

Am in the Race to destiny - YouTube
 
Wameyataka wenyewe ya kumkabidhi chama DHAIFU sasa chama kinasambaratika na nchi inazidi kudidimia kiuchumi. Halafu cha ajabu hakuna hata anayemkemea kwa UDHAIFU wake. Bora kizikwe rasmi tu na 2015 tupate utawala mpya nchini.

ccm ndio mwisho wake wake huu sina imani kama watanusuka kwenye kiama hiki laana za watanzania lazima zionekane hapa hapa dunia wala si CDM/CUF bali wao kwa wao
 
............. Kiongozi tangu miaka 40 iliyopita ..... tatizo ni kwamba wanaendelea kung'ang'ania madaraka wanajua hakuna kujiuzuru hata kama wakifanya madudu katika uongozi huku wakijisahau kwamba kuna mwisho wa uongozi, pamoja na wizi walioufanya bila kufikishwa mahakamani ndani ya miaka 60 bado wanataka kukaa humo humo.... mwisho ndio huu
 
“Msione nimenyamaza, mkadhani sijui kile mnachokifanya dhidi yangu. Jaribuni kufuta jina langu, muone kama nanyi sitawaanika kwa Watanzania, wawajue mlivyo wachafu na sijui mtaweka wapi nyuso zenu,” alisikika akisema kabla hajapanda gari lake na kuondoka.

Hivi hawa ndiyo viongozi tunaowategemea, kwa hiyo anajua mauozo ya CCM lakini kwa kuwa ana cheo ndo hataki kusema huo uozo mpaka atoswe? Hii ni aibu kubwa sana kwa chama cha ki-ukoo!
 

CCM yawasuta Sitta, Lembeli
• Nape asema kauli zao haziwezi kusikilizwa kwani hawajiamini

na Waandishi wetu
Tanzania Daima


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitishwi na baadhi ya viongozi wake ambao wamekuwa wakitoa kauli zao barabarani kwa ajili ya kulalamika na kukikosoa chama badala ya kupeleka malalamiko yao katika vikao husika.

Kitendo cha viongozi hao kuendelea kutoa taarifa zao za malalamiko barabarani ni dalili za kutojiamini na kuonyesha udhaifu wa kuhimili mikiki ya uchaguzi ndani ya chama hicho na inawezekana wana agenda zao za siri.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ya chama hicho, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya vikao vya chama ambavyo vinaendelea mjini hapa.

Licha ya Nape kutowataja vigogo hao kwa majina, lakini ni wazi kuwa walengwa ni pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye kwa siku za karibuni amenukuliwa akilalamikia vitendo vya ufisadi kwenye mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM na hivyo kuibua mjadala mzito kwa baadhi ya makada akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, wakimtaka awataje kwa majina anaowatuhumu.

Wengine waliosikika hivi karibuni wakilalamikia mchakato huo wa uchaguzi unaoendelea ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Nimrod Mkono wa Musoma Vijijini ambao inasemekena majina yao yamekatwa kwenye orodha ya wagombea, huku wakisema hapatatosha iwapo wataenguliwa kweli kimizengwe.

Nape alisema kuwa CCM inashangazwa na baadhi ya wanachama wake ambao wanaonyesha woga wa kushindwa kuhimili mikiki ndani ya chama, hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake wamekuwa wakitishia kujitoa kama majina yao hayatarudishwa kwa ajili ya kuchaguliwa katika nafasi zao walizoomba.

Alisema kuwa chama hakiwezi kuwasikiliza viongozi ambao wamekuwa na tabia ya kutoa matamshi yao barabarani na kwamba kama wanataka kutoa kauli hizo, watumie fursa ya kuwasilisha hoja zao katika vikao.
"Chama hakiwezi kusikiliza kauli za barabarani ambazo zinatolewa na viongozi hao, kama wana hoja wazilete katika vikao kwa maana nao ni viongozi, wasipofanya hivyo basi huenda wana agenda zao za siri, ambazo wanazijua wao," alisema.

Kuhusu baadhi ya wagombea ambao walisikika wakidai kuwa majina yao yasiporudishwa patachimbika, alisema kuwa inaonyesha ni jinsi gani hawajiamini kwani kiongozi ni lazima awe mvumilivu na mwenye kuhimili mikiki ya siasa za sasa ambazo zina ushindani mkubwa.
"Kama kiongozi anaanza kusikia tetesi kuwa jina lake halitarudishwa halafu anaanza kusimama barabarani na kudai kuwa hapatatosha, ni wazi kuwa ni mwoga wa kuhimili ushindani, lakini nataka kusema kuwa haki itatendeka na busara zitatumika.
"Hakuna mtu ambaye jina lake litakatwa kwa ajili ya mizengwe, bali vigezo vitazingatiwa ili kila mmoja apate haki yake, na lazima wagombea watambue kuwa kwa vyovyote vile lazima apatikane kiongozi ambaye ataweza kuongoza jumuiya husika," alisisitiza Nape.

Aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa wingi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, kuna uwezekano wa kutokea msuguano mkubwa kwa wanachama kutokana na kila mmoja kutamani kushika nafasi aliyoiomba.
"Kimsingi wanachama waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ni wengi zaidi ya mahitaji, hii ni ishara kuwa chama bado kinapendwa… kunawezekana kukatokea msuguano wa ndani kutokana na wingi wa wagombea, lakini chama kina utaratibu wa kumaliza mambo kama hayo," alisema.

Kuhusu vikao kwenda kinyume na ratiba, Nape alisema kuwa kutokana na wingi wa wagombea wa nafasi mbalimbali, imelazimika sekretalieti kukaa siku tatu badala ya moja na kamati ya maadili ilitakiwa ikae siku moja, lakini imekaa mbili tofauti na matarajio.

Nape alisema kutokana na wingi wa wagombea, imewalazimu vikao kuchukua muda mwingi kujadili kwa makini ili kuhakikisha haki inatendeka na kuongeza kuwa, kwa nafasi ya wenyeviti wa mikoa zinazotakiwa ni nafasi 31 ila walioomba ni 187, katibu siasa na uenezi mkoa zinatakiwa nafsi 31 walioomba pia ni 187.

Alisema kuwa makatibu wa uchumi/fedha wa mkoa nafasi zinazohitajika ni 31 ila walioomba ni 170, wenyeviti wa wilaya nafasi ni 31 walioomba 148, wenyeviti wa wilaya wanahitajika 161 walioomba ni 965, wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 221, lakini walioomba ni 1,380 na wajumbe wa NEC taifa wanahitajika 20 bali walioomba ni 89.

Nape alisema kuwa nafasi nyingine ni wenyeviti wa Jumuiya Taifa ya UVCCM ambayo inahitajika nafasi moja ila imeombwa na wagombea 47, UWT nafasi moja nayo inagombewa na watu 9, Jumuiya ya Wazazi nafasi moja imeombwa na watu 22 na makamu mwenyekiti UVCCM inahitajika nafasi moja, lakini walioomba ni 27, UWT nafasi ya makamu imeombwa na watu watatu huku ile ya wazazi ikiombwa na watu 10.

Hata hivyo, Nape alisema kuwa hatua ya mwisho ya kupitisha majina ya wagombea hao ni NEC na kwamba vikao vingine vinapitisha na kutoa alama za sifa ya wagombea.

Kinana ang'atuka
Mwanasiasa nguli na kada maarufu wa CCM, Abdulrahman Kinana, ametangaza kung'atuka kuwania nafasi yoyote ndani ya chama hicho tawala.
Kinana ambaye amekuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC) kwa miaka 25 sasa, ametoa kauli hiyo jana alipoulizwa sababu za kutogombea nafasi yoyote ya uongozi katika uchaguzi unaoendelea ndani ya CCM.

Kada huyo maarufu ambaye amepata kuwa Meneja Kampeni wa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Jakaya Kikwete, alisema miaka 25 ya kushiriki katika vikao vya juu inatosha na ni vizuri kung'atuka.

"Naamini kuna wana-CCM wengi wazuri wenye sifa na uwezo wa kuongoza chama. Uongozi ni kupokezana vijiti na ni wakati wangu kukabidhi wengine kijiti hiki," alisema Kinana.
Hata hivyo hakuwa tayari kueleza kama mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete atamteua kuwa mjumbe wa NEC atakubali au la.

Kinana amekuwa kada anayeheshimika sana ndani ya CCM, mwenye ushawishi mkubwa hasa wakati wa vikao vya juu vya chama.
Wakati Kinana aking'atuka, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kada huyo amekuwa msaada mkubwa kwa chama.

Hata hivyo alisema licha ya kung'atuka, Rais Kikwete anaweza kumteua akitaka kupitia nafasi kumi alizonazo kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
"Kinana ameng'atuka wakati bado chama kinahitaji mchango wake. Hata hivyo mwenyekiti wetu wa taifa, Rais Kikwete hazuiwi akitaka kumteua," alisema Nape.

Katika hatua nyingine, Nape amesema kuwa yeye hajagombea nafasi yoyote ya uongozi ili kujipa nafasi ya kusimamia vizuri uchaguzi huo.
"CCM ina watu wengi sana wenye sifa na uchaguzi umekuwa na changamoto kubwa. Hivyo nimejipa nafasi kuweza kusimamia uchaguzi huo kwa karibu zaidi," alisema Nape.

Katika hatua nyingine, kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichotarajiwa kuanza jana na kumalizika leo, huenda kikamalizika kesho baada ya kuchelewa kuanza.
Kikao hicho chini ya Rais Kikwete, kilitarajiwa kuanza jana saa tatu asubuhi, lakini kilikwama na kuanza saa 11 jioni.

Habari kutoka ndani ya CCM zilisema kuwa hali hiyo ilitokana na kikao cha Kamati ya Maadili kuchelewa kumalizika kutokana na mvutano mkubwa wa kupitia majina ya wagombea.

Wazee wamvaa Sitta
Wazee wa CCM mkoani Shinyanga, wametishia kufanya maandamano ya amani kuhusiana na kauli tata zinazoendelea kutolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Katika tamko lao, wazee hao walisema wakati umefika sasa Sitta awaeleze Watanzania juu ya kauli zake hizo, ikiwemo ile ya kuwepo kwa mafisadi ndani ya chama na aliyoitoa hivi karibuni akiwa Karagwe, ya maisha bora kwa kila Mtanzania hayatawezekana.

Kwa niaba yao, Shomvi Ibrahimu Saidi, alisema kuwa waziri huyo ambaye pia ni mjumbe wa NEC na mbunge wa Urambo Mashariki, amekuwa akikaririwa akitoa tuhuma nzito ndani ya serikali na chama, hivyo ni vema akaweka wazi majina ya watuhumiwa wa ufisadi.

Pia walikumbushia jinsi kiongozi huyo alivyowahi kuitolea maneno makali Kamati Kuu ya CCM katika kipindi cha ‘Dakika 45' kinachurushwa na Televisheni ya ITV, akisema kwamba ilihongwa na mafisadi ikabadili utaratibu wa kuchagua Spika wa Bunge.

Wazee hao wamemuomba Waziri Sitta kama hana ushahidi wa kutosha wa kuupeleka kwenye vikao vya chama na vyombo vya dola kama TAKUKURU, polisi na mahakama, ni afadhali akae kimya kuliko kuendelea kuwachanganya watu.
 
Back
Top Bottom